1.Kimaadili waandishi hutakiwa kuhifadhi majina mpaka baada ya kuthibitishwa na vyombo husika hivyo walichofanya Mwananchi ni right.
2. Mke wa Chagonja naye ametapeliwa Sh.1.5 kwa ajili ya mwanae na nduguze wawili.
3. Kuna uwezekano Mke wa Chagonja naye aliwatonya rafiki zake nao wakawatonya rafiki zao na chain ikaendelea kama upatu, hivyo wote walio tapeliwa kwenye chain ya Mke wa Chagonja kudhania tapeli ni mke wa Chagonja kumbe sivyo bali na yeye ametapeliwa!.
4. Kwa vile mpango mzima sio tuu unahusisha utapeli bali ni rushwa ya wazi, mtoaji na mpokeaji wote ni wala rushwa, hivyo baada ya kukamilika uchunguzi wa kesi ya utapeli, wahusika wote wafunguliwe mashitaka ya kesi ya kutoa rushwa!.
5. Mke wa Chagonja athibitishe source yake ya fund, kama hana kazi yoyote ya maana au biashara yoyote ya maana, ya kumpatia Sh. 1.5 lump sum, inamaanisha source ya fund ni mumewe Chagonja, hivyo Afisa Polisi ametoa fedha ili kumpa mkewe huku akijua wazi zitatumika kwa rushwa, nalo ni kosa kisheria hivyo litamcost mumewe kazi yake under morals na sio legal.
6. Kwenye jinai, kila mtu anasimama kama yeye hivyo baada ya kujulikana ni mke wa Changonja, sasa atajwe kama Mrs. Chagonja na sio tena kumtaja kigogo wa polisi ni kumchafulia jina lake bure, Chagonja hahusiki kwa lolote hata kama ni yeye alimpa mkewe fedha hizo za rushwa!.
7. Sheria zetu za jinai zinatoa kinga kwa mume au mke hawezi kutumiwa na mahakama kutoa ushahidi au utetezi unamhusu mwenza wake, hivyo Chagonja haguswi kwa namna yoyote na nyendo zozote za kijinai za mkewe wala hatakiwi kuchunguzwa kijinai bali ni jukumu la jeshi la polisi kumchunguza ki morals kama kiongozi!.
8. Chagonja anaweza kulishitaki Gazeti la Mwananchi kwa kesi inayoitwa "defamation by innuendo" kwamba kosa ni la mkewe, kitendo cha gazeti hilo kushadidia "Mke wa Kigogo wa Polisi" na kigogo huyo ni yeye by implication anayechafuliwa jina ni yeye na sii mkewe!.
9. Enzi za Nyerere, Chagonja angekwenda na maji kwa kuitumia ile formular ya "Mke wa Kaisari".
Pasco.