MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 850
Wakuu macho_mdiliko na Rwabugiri nawapa asante kwa maoni yenu. Kama kuna kitu kinachonikera kikweli kweli ni misimamo na maoni ya watu kama MwanaFaslsafa1. MwanaFalsafa1 anadai kuwa CCM ina nguvu kubwa vijijini na ndiyo maana ni rahisi sana kwao kushinda iwe kwenye ubunge au uraisi, je kwa nini wameweza kushinda nafasi zote za Ubunge mjini Dar es Salaam. Kwa nini yeye MwanaFalsafa1 licha ya kuwa na uelewa kuliko hao wa vijijini bado anakaa pembeni na eti kuwashauri wengine namna ya kuiondoa CCM.
Yaonekana MwanaFalsafa1 anaridhika na uongozi wa CCM nchini uliojaa ubabaishaji, ufisadi na ulaghai wa kiwango cha juu na kama ni hivyo kwa nini ashauri namna ya kuiondoa CCM ? Na kama haridhiki na hali hii kwa nini akae pembeni kusubiri watanzania wengine (yeye anawaita wapinzani lakini mimi nawaita wazalendo wenye uchungu na taifa lao) ndio walikomboe taifa ? Kama ni unafiki, hapa MwanaFalsafa1 anaonyesha kiwango cha juu kabisa kama walivyo wengi wanaotetea status quo.
MwanaFalsafa1 anatetea kuwa wizi peke yake hauwezi kuwanyima wazalendo ushindi lakini anasahau kuwa huo wizi ni sera ya CCM inayolindwa na dola. Hiyo asilimia 80% ni idadi ya walioweza kupiga kura kama ilivyotangazwa na dola kwa mdomo wa kinachoitwa tume ya uchaguzi. Je, ni asilimia ngapi ya watanzania walinyimwa fursa ya kupiga kura ama kwa shahada zao kununuliwa, vitisho vya dola, rushwa, wizi, udanganyifu, ulaghai na uzembe wa wasimamizi wanaoteuliwa na CCM.
Tuache kudanganyana hapa, ama umepiga kambi kwenye bonde la kashfa na harufu ya uvundo si tatizo tena kwako au uko kando na unakerwa na hiyo harufu kiasi cha kusogea mbali. MwanaFalsafa1 ameamua kulifanya hilo bonde kuwa makao yake ya kudumu na kwa kuwa katiba inalinda kuwepo kwa bonde haoni kasoro yoyote na kuwepo kwake. NI lini tutakuwa wakweli kwa nafsi zetu na kutambua nguvu halisi alizonazo hili zimwi la CCM. Kila siku tunashuhudia haya mambo hadi kwa jirani zetu lakini hatujifunzi, tuna nini ?
Huu ni ulaghai - CCM ingetaka kuona upinzani wenye nguvu, hivi sasa tungekuwa na katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na dola inayofanya kazi bila uonevu, upendeleo na kwa maelekezo ya CCM. Kwa hali hiyo vitendo tulivyovishuhudia Busanda havingepata nafasi.
MwanaFalsafa1, unajua hatari ya kila chama kuunda kikosi cha vijana,
je, umesikia walichokuwa wanafanya vijana wa CCM huko Busanda ?
Kaka Es:
Sikujua kama na wewe ni propagandist, nimekuzoea zaidi kama protaganist ama walau propoundist!
Maandiko yako umeyavika ukada na umeshindwa kutazama pande mbili za shilingi. Ukienda Karatu ukawasomea maneno hayo, watakunyooshea vidole vya macho kama walivyofanya kwa mkapa(joke)
Najua wewe unaingia baadhi ya vikao vya CCM, kwa hiyo unajua hofu ya chama chako kuhusu upinzani kinyume na unachotaka kusema hapa.
Si vyama vyote 18 vi sawa. Vingine ni TUMAINI JIPYA, na vingine ni AIBU kwa Taifa. Tuko katika chekecheke hivi sasa.
Kaa karibu na Kaka yako Lowasa, utajua jinsi anavyoiona CHADEMA kama nightmare kwa ndoto zake za kifisadi.
Ufisadi wa CCM si sawa na udhaifu wa upinzani-na kubwa zaidi ni kuwa vipo vyama vinavyoongezeka nguvu kila kukicha.
Toa mifano ya allegation zako kuwa kuna vyama ambavyo badala ya kuwa kwenye kampeni vijijini wakati wa uchaguzi wako kwenye JF.
Pigia chapuo CUF chambelecho cha divided attention. Lakini jua kwamba watu makini wako focused. Wanajua adui wa kumlenga ni yupi na alengwe vipi kwa kutumia silaha gani.
Ipo siku utakumbuka haya maneno, hata kama nimeyaandika kwa uchache wa hoja.
Upo udhaifu katika upinzani;lakini zipo nguvu zinazoonekana na kuu kuliko yote ni kwamba uko mwelekeo uliyo bayana katika baadhi ya vyama na sehemu ya wanasiasa wa KIZAZI KIPYA.
Kuwa wakala wa mabadiliko unayotaka kuyaona kaka- bahari ni muunganiko wa matone madogo madogo ya maji. Kama kila mpenda mageuzi akitimiza wajibu wake, udhaifu ulioko katika upinzani utazidi kutoweka na nguvu inayoongezeka itatamalaki.
Time kills, Time Heals, Time Tells.
Mdogo wako,
JJ
Unajua kama wewe ni kiongozi na maarufu basi ujue kuna watu nao wanakinyemelea pale ulipo ,hivyo akiondoka mmoja wale wanaonyemelea na kukodolea macho huwa wapo tayari kurithi cheo chako ,kwa hivyo basi mtaji si kiongozi mtaji ni watu wanaokiunga mkono Chama chao,ikiwa hao wataondoka basi tunaweza kusema CUF inaporomoka ,ila kumbuka tu hawa wanaoondoka jana na leo si wa mwanzo ,watu wanakufa na wengine kuzaliwa.
Hivi karibuni mh Lipumba alisema "
Hivi sasa CUF haipambani na chama tawala pekee bali hata chama kimoja cha upinzani Chadema hivi sasa kinajikusanyia wimbi wa wanachama na hata kuwa ni chama kinachopambana kwa karibu na CCM katika chaguzi. Hilo limejidhihirisha katika uchaguzi wa Tarime, Busanda na hata uchaguzi uliofanyika hivi karibuni wa Biharamulo" jee kupambana na Chadema nini kukiimarisha Chama au kukua chama (CUF)
Mchukia Ufisadi naomba utupe habari kwani inapokuja habari za Lwakatare unazijua vyema kama Field marshal ES na habari za Kilango.
Kwa nini unatilia mashaka kuhusu wanaCUF ndugu?mashabiki wenyewe wa CUF kina maralia Sugu, wala ndio maana hasa hawajui nani ni nani katika siasa za nyumbani, hakika mtu akiisha kuwa mwana CUF kuna mambo natilia shaka juu ya uelewa wake.