Nini hatma ya TCU baada ya kauli ya Rais Magufuli?

Nini hatma ya TCU baada ya kauli ya Rais Magufuli?

Unawezaje ku control doublication ya wanafunzi? Ya mwanafumzi kuchaguliwa zaid ya chuo kimoja? Nadhani hii ilikuwa moja ya msingi wa CAS sasa tunaotoa kawqzo yetu jukwaani tufikiri na hii

Hili ni moja kati ya maswali ya msingi sana. Na nashangaa inakuwaje watu walioko vyuoni hawaelewi umuhimu wa hili na kwamba TCU hawafanyi enrolment?
 
Wanafunzi wengi watakosa nafasi, hasa baada ya idadi lengwa kutimia na vigezo kufikiwa katika chuo husika.suala syo kuvuruga mifumo, hapa ni kushauri na kusimamia ipasavyo, No research no right to talk, TCU came after research na matokeo yameonekana, pia imekuwa huru kwa wanafunzi kubadili vyuo na program watakazo, kwangu naona TCU aendelee kusimamia kama miaka mingine.
 
Grades za kujiunga na chuo hazipangwi na wizara na wala Waziri hana mamlaka yoyote ya kuvipangia vyuo grades. Pili TCU hawapangi grades wala enrolment ya mwanafunzi yoyote, Senate ya chuo husika hufanya hivyo.

TCU walitengeneza common pool ya wanafunzi kuapply chuo kwa mujibu wa sifa ulizonazo ila jukumu la enrolment lilibakia kuwa la chuo husika.

Kama ulikosa chuo ulichokitaka ni kwamba Senate ilikukataa ( taarifa anapewa TCU ya waliochukuliwa) hivyo TCU ikakutafutia mahala pengine walipokukubali.

Hata ungeruhusiwa kuomba moja kwa moja bado Senate ya UDSM ingekukataa vile vile na chuo ungekosa kwa kuwa usingeomba tena popote pale.

Dhana ya kuwa kusoma UDSM ndio umekwenda chuo kikuu ni ya kipumbavu na inapaswa kulaaniwa. Vijana waambiwe kabisa elimu ya chuo inategemea innovation na creativity uliyonayo sio umesoma wapi.
dah pole sana sijuh unaelewa ulichokiandika ama una mihemko yako ya kibashite bashite
 
Hapa wangefuata uwazi wa UDSM ingesaidia, kwani kwa kila anaedahiliwa utaona ufaulu wake wa O na A level. Wanaweka point zake kuanzia wajuu hadi wa mwisho. Hivyo kama uliachwa una uwezo wa kuuliza kunani kama unapoint juu ya cut off. Na UDSM wakipelekewa jina na TCU halafu wakaamua kuliacha wanatoa sababu. Basi vyuo vyote vinelazimishwa kufanya hivyo na ingekuwa rahisi kuona nani kaomba wapi na kapelekwa wapi kwa nguvu.
Lakini pia vijana wetu wengi hawapati ushauri mzuri kwani unaweza kuwaona wamejazana mahali ambapo ufaulu wao haukidhi hivyo bila TCU kuwasaidia wengi watakosa nafasi kabisa.

TCU hawafanyi enrolment, Senate ndio inafanya enrolment. Uamuzi wa Senate kumuacha mtu sio kosa la TCU ni mtu mwenyewe kutotimiza entry requirements.
 
dah pole sana sijuh unaelewa ulichokiandika ama una mihemko yako ya kibashite bashite

Boss nikupe pole kwa sababu inaonekana hujui taratibu zozote za mfumo wa elimu ya juu. Nakushauri pitia sheria ya Vyuo Vikuu na University Charters ujue majukumu ya TCU yanapoishia na Senate inapoanzia.

Ni wazi course uliyoomba ilikuwa very competitive na maksi zako hazikutosha.
 
Boss nikupe pole kwa sababu inaonekana hujui taratibu zozote za mfumo wa elimu ya juu. Nakushauri pitia sheria ya Vyuo Vikuu na University Charters ujue majukumu ya TCU yanapoishia na Senate inapoanzia.

Ni wazi course uliyoomba ilikuwa very competitive na maksi zako hazikutosha.
naomba unijibu jukumu la kubadilishwa kwa grades za kujiunga chuo ni la wizara ama ni tcu maana tusije tukaonana wehu hapa...
 
Kuna ukweli hapo, jpm umeona kitu japo wadau wakae waone hiyo kitu imekaaje
 
Kila chuo kiwe na limit no ya kudahili na kuenroll wanafunzi , say wasizidi wanf 500 chuo X nk
 
TCU hawafanyi enrolment, Senate ndio inafanya enrolment. Uamuzi wa Senate kumuacha mtu sio kosa la TCU ni mtu mwenyewe kutotimiza entry requirements.
Uzuri wa uwazi wa UDSM wewe uliachwa utajua kwa nini wamekuacha. Wengine wote hawafanyi hivyo.
 
naomba unijibu jukumu la kubadilishwa kwa grades za kujiunga chuo ni la wizara ama ni tcu maana tusije tukaonana wehu hapa...

Grades za kuingilia chuo zinapangwa na Senate za vyuo husika si Wizara wala TCU. Majukumu ya wizara ya elimu kwa elimu ya juu ni kusimamia allocation of funds na mambo ya utawala za vyuo sio academics. Na jukumu la TCU kwa vyuo ni kusimamia ubora wa elimu (ubora huu unasimamiwa kwa kuhakikisha vyuo vinaendesha kozi zilizopo kwenye ithibati)

Masuala yote ya kielimu (academics) yanasimamiwa na vyuo husika kufuatia miongozi iliyowekwa. Hiyo ni pamoja na enrolment, university prospectus and cariculum, academic awards (aina za degree zitolewazo hata Bachelor zina makundi, honors, cum laude, laude etc na bila shaka unafahamu pia kuwa kuna degree zinakuwa awarded na schools, colleges na universities) , structure ya schools etc.

Maamuzi yote kuhusu elimu vyuoni yanafanyika huko huko chuoni sio wizarani, entry requirements (cutoff) hujadiliwa level ya department to boards of school/college na mwisho kabisa senate hufanya uamuzi wa mwisho. Utaratibu huo huo hufuatwa wakati wa kupitisha curriculum na wakati wa kuondoa walioshindwa masomo.
 
Hivi mmepata kujiuliza ni kwa nini mfumo wa udahili wa pamoja ulianzishwa. Wengi humu mmekuwa mnalaumu MUM kwa muda mrefu kwa kuwa tu haikuwa ikidahili wanafunzi kupitia TCU kwanini?
 
Naombeni tuchangie hatma ya TCU juu ya kufutwa kwake..
Wajisahihishe. Maana anayosema Rais ni kweli tupu. Na ndiyo maana hata watumishi wake wana ukwasi wa kutosha kabisa. Mkurungenzi wa habari tu kajaza magari makubwa na maghorofa huko Goba. Rushwa rushwa rushwa nchi hii too much. Namuunga mkono Rais.
 
Hapana, wazo la Rais ni sahihi sana kwenye hili.Mwanafunzi aombe chuo anachokitaka fullstop. Kuna watu wengine kama mie, kwa Tanzania kama ungenichagua nje ya UDSM ungekuwa umeishaniharibia ndoto zangu.

Jina la chuo linamatter.Ndio maana kuna rank za vyuo kwa ubora wao, na kwa mtindo huu, ushindani wa vyuo utaongezeka maana usipokuwa na jina hutapata wanafunzi.
Hata sasa hivi watu huomba chuo wanachotaka (kuna restriction ya course mbili kwa chuo kimoja), issue kubwa ni grades /point za waombaji. Kama huna point nzuri na chuo kina competition hata ukiomba chuo moja kwa moja hutapata. Sioni kama wazo au agizo la raisi litasaidia na tusipoangalia wengi watatoka na vilio na wataishia kuikumbuka CAS. Wenye ufaulu mzuri watapata watakacho (watachaguliwa kule walikoomba na kujaza nafasi kwenye vyuo vyote walivyo omba, wale wa kawaida itabidi wasubiri vyuo vikifunguliwa wajaze nafasi zilizo achwa na hilo kundi la kwanza, bahati mbaya vyuo vina dead line ya kudahili na ku-register hivo kundi hili kama sio makini watahangaika na admission.
 
Back
Top Bottom