Nini hatma ya nafasi 2 za CHADEMA Afrika Mashariki

Nini hatma ya nafasi 2 za CHADEMA Afrika Mashariki

We ndio Bashite maana unafuata mkumbo, chance ni mbili from CHADEMA but wangepaswa kuegesha hata mtu(Mwanamke) mmoja ili kuepuka kuangukia katika kundi la Kupigwa Kura za NDIO au HAPANA(jambo ambalo ni mbaya kwao kutokana na namba kubwa ya wabunge wa Ccm) n hence labda WENJE na Masha wangepita kwa Kura za kawaida . Ila kwakua Mtukufu mwenyekiti aliona apeleke fixed Number Yaani 2 ili apite bila kupingwa na Akasahau kwamba utaratibu wa Bunge haupo hivyo, basi matokeo ndio hayo. KURA za HAPANA zilizidi na ...[emoji28]
Kwa nini uwapangie?! Wamevunja sheria gani kuwaleta hao wagombea? Wewe ulitegemea mabashite wapige kura za ndio kwa wapinzani wao...wale wana itikadi mbili tofauti ndio mana nafasi hizi walipewa kivyama kuepusha hayo yote.
 
Nafasi mbili hizo hawawezi kuzipata kwasabb wao wenyewe wanajitenga hata kukaa bungeni kwahyo wanakuwa wanaonyesha hisia za uchama kuanzia mapema kabsa
 
Jitafakarini sana CHADEMA. Hayo makundi mawili ni muhimu sana. Katika kuwahadaa watanzania angalau mngetafuta mwanamke ambaye kwa akili zenu ni dhaifu kabisa na mzanzibari mnaodhani kwa akli zenu ni dhaifu sana wakawasindikiza Wenje na Masha, yote hayo yasingetokea. Mnakwenda kuwaweka watu wa kutoka MWANZA tu wakati Tanzania hii ni kubwa sana, inatoka Namanga hadi mbambabei, inatoka Pemba hadi kigoma, inatoka Tunduma hadi Sirari.
Mkuu ndo maana kilio chetu mbowe atoke ktk uenyekeiti
 
Wamezidi kuweka upendeleo mbele. Inamaana ukanda wa kusini au kati hakuna mtu wa kumsimamisha hadi wachukue mwanza pekeee? Ngoja waonje joto la jiwe
 
chama kinachojipambanua kutetea wananchi

Wanakosa umakini kisa kutawaliwa na kuendekeza ubinafsi.

Kila siku wanahubiri democracy kumbe wenyewe wala hawaijui, wala hawaitaki hiyo democracy. Iweje kwenye uchaguzi wa BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI wamepata nafasi mbili;

1)Wameshindwa kutoa Fursa kwa Idadi kubwa ya wagombea ili kuwapa wapiga kura wigo mpana wa maamuzi kama CCM na CUF walivyofanya.Wao nafasi mbili wanatoa kwa watu wawili na kutaka kulazimisha bunge kuwapitisha bila kupingwa na hivyo kuikanyaga demokrasia. AIBU!!

2)CDM inaundwa na wanachama wa jinsia zote,wanawake na wanaume lakini kuna jumuia ya vijana (bavicha). Wao kwa wananchi wanahubiri Fursa Sawa kwa jinsia zote, lakini linapokuja suala la Fursa za ubunge wa afrika mashariki wanawake hawana nafasi kabisa. AIBU!!

3)Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania inaundwa na nchi mbili - Tanganyika/Tanzania bara na Zanzibar /Tanzania visiwani. CCM wameweka wagombea wao kwenye uchaguzi wa bunge la Afrika mashariki kwa kuzingatia pande zote mbili,wao Chadema wanajinasibu kuwa ni chama cha kitaifa! lakini wameleta majina ya wagombea wawili,wote kutoka mkoa mmoja,wote kutoka MWANZA..... Hii tunaitaje? .. AIBU.

Uchaguzi huu unafuatiliwa kote Afrika mashariki, kwa kuwa Tanzania ni taifa kubwa na lenye ushawishi mwingi , hii ni aibu kwa chama kikuu cha upinzani, aibu,aibu aibu,aibu,aibu, aibu,aibu!!
Ha haaaaaa mkuu watalia basi waache
 
Lakini tulisema chadema wanapendelea kaskazini tu! Wamechukua mwanza na penyewe kumbe ni tatizo?
 
mkuu hebu nitajie achievement walau tatu tatu za kiuongozi kwa kila mmoja wa hawa viongozi wawili make mi nimekaa nyamagana kwenye vipindi vyao vya ubunge na kusema kweli hakuna cha maana ambacho wamefanya zaidi ya kung'oleana mapazia ofisini na kufanya tu fujo bungeni
Watu wengi wana fikra hafifu kudhani kuwa kukiwa na barabara nzuri, umeme au maji, basi mbunge wa eneo hilo ni mchapa kazi wakati mambo hayo hufanywa na serikali na siyo mbunge.

Kazi ya mbunge ya kwanza ni kushiriki utungaji sheria bungeni. Jukumu la pili ni kuzitambua changamoto zilizopo jimboni mwake na kuzifikisha serikalini. Katika majukumu hayo makuu mawili, ni yapi ambayo Wenje hakuyatekeleza?
 
Chadema pelekeni sepetunga wakenya wakajitafunie
 
We ndio Bashite maana unafuata mkumbo, chance ni mbili from CHADEMA but wangepaswa kuegesha hata mtu(Mwanamke) mmoja ili kuepuka kuangukia katika kundi la Kupigwa Kura za NDIO au HAPANA(jambo ambalo ni mbaya kwao kutokana na namba kubwa ya wabunge wa Ccm) n hence labda WENJE na Masha wangepita kwa Kura za kawaida . Ila kwakua Mtukufu mwenyekiti aliona apeleke fixed Number Yaani 2 ili apite bila kupingwa na Akasahau kwamba utaratibu wa Bunge haupo hivyo, basi matokeo ndio hayo. KURA za HAPANA zilizidi na ...[emoji28]

Kama.ni hivyo sheria ilipaswa kusema 50/50 lakini sheria inasema 1/3.Niambie theluthi moja ya Mbili ni ngapi??
 
Wala mwislamu why? Halafu wote wachaga wakirisito.
Hateuliwi tu mtu kwa sababu ni mkriso au mwislam anateuliwa mtu mwenye experience na bunge, kama unaona kuna haja ya kuwepo muislam mpigie kura ww
 
Daaah,mkuu umemjibu vizuri sana,safiiii.Tatizo watu wengi huu mchakato hawauelewi.

Watanzania tunatakiwa tuamke mambo ya kupeleka watu kwa ajili ya kuuza sura ya kome.Tunatakiwa tuzitumie Mahakama za EAC vizuri.Huu ujinga wa kupeleka chakula vya wakubwa unatakiwa uishe sasa.

Hivi wamekosa kupeleka MTU mwenye Katiba ya maana zaidi ya hawa Mabashite?Si bora wangempeleka hata Angela Kairuki basi.Wametoa Shyrose Bhanji wanweka.muuza sura Binti Bashite.Upumbavu huu.

Issue ya EALA siyo ya Chama ni ya Taifa.I wish watanzania tuwe wamoja kwenye hili.Kuna wenzetu 50 wameuawa na askari wa Rwanda hakuna anayelisemea,leo unampeleka Fancy aliyefoji vyeti hana elimu ya sheria ati anawakilisha nchi kisa kijana.Ataweza.kubambana na AG wa Rwanda huyu??Basi watafute hata watu kule CHRAGG wako akina mama wenye uwezo.Akina Binti Sarakikya kuliko huu ujinga na Upumbavu wa CCM.

Jamani fikirieni Taifa siyo Mwili??Watawala wanafikiri Zinaa tu!Ati fancy stupid.
 
Nchi inachezewa na punguani wewe unasema niache hasira!? Mbona hujamwambia ShilawaDU aache hasira na vitisho dhidi ya Watanzania!? Wewe punguani kweli! Kuharibu nchi ni kitu rahisi sana lakini kuijenga ni kazi kubwa sana ya miaka chungu nzima. Tia akili kichwani na kuacha kupigia debe wahuni, majangili na mafisadi. Ni hasara kubwa kwa nchi kuwa na mapunguani kama wewe mnaopigia debe uovu wa kila aina unaoendelea nchini na kusababisha nchi kubaki nyuma kwenye kila sekta muhimu.

Kaka yangu hii mijitu haelewi hata uieleweshe vipi!Wamepewa mfano Kagame kata AG imagine,wanasheria ngumu waende kupambana.Unadhani wanaenda kudai.nini zaidi ya radhi na raslimali zetu ziwe shared amount the States? Unadhani Kagame mjinga na huu ushoga wake na Mkullu??

Halafu tunapeleka wauza sura na Makalio.Ushenzi huu.mpaka lini??
Ni lini CCM itafikira Tanzania kama.Taifa na si Chama Cha Majangili.

Wakati mwingine ninawish hawa wazee wa CCM wote wachukuliwe labda tutapata CCM yenye akili.CCM itakayofikiria Taifa na kuacha ufala.Tutakapompata Spika atakayeona Taifa kwanza Chama baadaye.Siyo hawa maSpika wanaotegemea.matumbo yao.
 
mkuu hebu nitajie achievement walau tatu tatu za kiuongozi kwa kila mmoja wa hawa viongozi wawili make mi nimekaa nyamagana kwenye vipindi vyao vya ubunge na kusema kweli hakuna cha maana ambacho wamefanya zaidi ya kung'oleana mapazia ofisini na kufanya tu fujo bungeni

Niambie Mazuri aliyefanya Fancy mpaka apelekwe EALA.??

Kwa Wenje tumeona Michango yake.mzuri.Bungeni na siye wapiga kura wake tunajua mangapi ametusaidia.kuliko.Huyu Bashite mliyotulazimisha naye.
 
Viongozi wa sasa wa CHADEMA ni short-sighted. Maneno na mikwara mingi, lakini logic na vision hawana. Yaani viongozi wa CHADEMA wanawachukulia wabunge wote kuwa hawaelewi. CHADEMA walifanya ujinga wa hali ya juu sana. Halafu eti wanalazimisha watu wao wapite bila kupingwa. Walitaka wapigiwe kura za ndiyo tu. Bahati nzuri wabunge wabunge wanaelewa.
 
Niambie Mazuri aliyefanya Fancy mpaka apelekwe EALA.??

Kwa Wenje tumeona Michango yake.mzuri.Bungeni na siye wapiga kura wake tunajua mangapi ametusaidia.kuliko.Huyu Bashite mliyotulazimisha naye.

Sasa mbona hamkumchagua tena ili arudi bungeni?
 
CCM yenye wapiga kura wengi bungeni isingewakubali wateule wa CHADEMA kwa nia ya kuwakomesha. Tuseme kwa mfano, Halima Mdee na Esta Bulaya wasingekuwa wabunge wa bunge la Jamhuri na hivyo kukidhi sifa za kugombea ubunge wa East Africa, na majina yao yakaletwa na majina mengine mawili ya wanaume ya Lema na Msigwa (ambao nao wanakidhi vigezo vya kuwa wabunge wa East Africa) hoja ya kuchagua wanawake ingetekelezeka? Je, majina hayo yote yasingekataliwa? Na kama hoja ya waliokataliwa ni kwa sababu ya kutokuwa na mwanamke kwenye orodha iliyoletwa, kwa nini yule mwanamke wa CUF hakuchagulika ili kukidhi theluthi moja ya nafasi tatu za upinzani? Mnapojadili muweke akiba kuwa kuna wanaofikiri na kuona mbali. Hoja iliyokwamisha mchakato si hiyo inayolazimishwa kwenye vichwa vya watu. Ni chuki dhidi ya wapinzani ambao ni wachache bungeni. Matokeo yake ni kuwa ama tutaenda na idadi ndogo ya wabunge ambayo ni kama tutakuwa tumejinyonga wenyewe ama tutachelewesha mchakato kwa jambo lisilo na tija yoyote kwa taifa. Tunajichora sana mbele ya wenzetu.
 
Hateuliwi tu mtu kwa sababu ni mkriso au mwislam anateuliwa mtu mwenye experience na bunge, kama unaona kuna haja ya kuwepo muislam mpigie kura ww
Endelea kufikiria kwa makalio. Hujiulizi kwanini nimemjibu hivyo mleta mada; hata mwandiko wenyewe nilioandika ulitosha kuku-alert something.
 
They have blunt political tactics. Kazi ingekuwa nyepesi sana kama wangeweka washindani watatu very competent na wasiopendwa na CCM. Hapo wangeokoa muda na fedha za kuendea mahakamani.
Chadema hawajavunja kanuni, wala bunge hawajavunja kanuni na pia Wabunge wawili wa chadema wamefeli kikanuni. Ila kimbinu walizidiwa na mahasimu wao.


Wewe kwa mtazamo wako Ni sahihi kuchagua wabunge ambao lazima ccm waridhike nao?, Ni bora ungeniambia kuwa wabunge wote watoke ccm
 
Back
Top Bottom