Nini hatma ya nafasi 2 za CHADEMA Afrika Mashariki

Nini hatma ya nafasi 2 za CHADEMA Afrika Mashariki

Kwanza tukubaliane, uchaguzi wa wabunge wa EAC jana haukuwa strictly partisan, vinginevyo Masha na Wenje wangepata kura 40 za CHADEMA wenzao peke yao.

Kwa hiyo kama C.C.M. wengi sana waliweza kwa kiasi kikubwa kuweka vyama pembeni, kuna nini kingine kilichosababisha kukataliwa kwa wagombea wa CHADEMA?

Nataka kujikita kwa Lawrence Masha, Waziri na mtumishi wa umma mstaafu, mwanasiasa mzoefu, mwenye elimu na exposure kutoka ndani na nje ya nchi, mwenye uwezo mahiri wa kujieleza Kiingereza ( bahati mbaya sana bado tunatumia hii litmus test kupima weledi wa Mtanzania), na pia mtaalam mwanasheria wa moja ya most prestigious law firms in the nation (IMMMA), na pia mtu mwenye political pedigree, yani uzao wenye historia ya utumishi na uongozi (Baba yake Lawrence Masha ndie alikuwa Nape Nnauye wa Nyerere, msemaji wa TANU wakati wa kipindi kigumu cha kutangazwa, kuenezwa na kupingwa Azimio la Arusha, kabla hajafukuzwa kundini kama Nape.)

Sasa kwa nini Masha akataliwe kwa kura iliyosema "bora tusipeleke mtu EALA kuliko wewe"?

Ukipima kwa vigezo, uzoefu wa kisiasa, kiutawala, kitaalam, kibiashara, Lawrence Masha ana credentials ndefu kupita wote waliohojiwa jana pale in my book. Na katika kujieleza alinivutia kuliko hata kijana wa Maghembe aliyewakuna wabunge kwa Kiingereza laini na utani wa kusema ana sura changa kwa sababu ya vinasaba vyake. Utoto ambao Masha hakuufanya. Masha muda wote ali get to the issues, akiwa very serious minded na akawaomba wamchague japo ni CHADEMA, kwa sura ngumu lakini kwa unyenyekevu mkuu.

Tatizo lililomwamgusha Masha, ukiacha siasa za vyama, ni matatizo ya ujana siku za nyuma, Uwaziri wa Rose Garden!

Watu hawajasahau alivyodharau uongozi aliopewa na JK akageuza ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuwa ni kwenye ki restaurant cha Rose Garden. Au ki saloon cha Mikasi, kuhojiwa mambo ya nchi kwenye TV huku unafanyiwa pedicure na manicure na haircut. Sijawahi kuona hata huko nje kwenye uhuru wa kila kitu na ma fashion yanakotokea ukakuta Waziri anajibu masuala ya nchi yuko salon anafanyiwa pedicure and manicure na haircut. Unageuza ofisi kuwa vijiwe vya vijana wenzio na wapiga dili wa mjini wakati ule wa Kikwete, kushinda bar mmezungukwa na michepuko yenu mnakula Heineken na makange ya Tilapia wa Kienyeji. Mida ya kazi.

Angalizo kwa vijana madarakani, wamesoma au hawakusoma, wamechaguliwa au wamependwa na kulindwa na mamlaka za uteuzi, wakumbuke kuna kesho na kesho kutwa, na watu wanakumbuka, basi wajiheshimu na kuheshimu Wananchi.
Usitake kutuaminisha kwamba hamkumchagua Masha kwa sababu ya kujilia makange ya tilapia na kunywa bia ya hineken. Kama ni hivyo, basi mna vigezo vya ajabu kweli kweli. Nataka nikujuze tu kama ulikuwa hujui. Huko miaka ya nyuma palikuwepo na waziri mmoja aliyependa kunywa sana whisky na mara nyingi alikuwa hakosi Hugos kwa wanamasantula kujirusha, mwisho wa siku alikuja kuwa rais wa nchi hii.
 
Ungetafakari kidogo nilichoandika in respect to alichoandika mleta mada na hulka zake ungeelewa maana "iliyomo". Hukujipa muda kutafakari Kiongozi. Mwanzisha uzi unamfahamu vizuri lakini? Au u mgeni hapa jamvini?
Pamoja kiongozi nimekuelewa sawia
 
Ulichokiandika kitaalamu tunakiita
"Egg to chick theory"
Hikieleweki to make story short
 
Uliona cuf walileta wa nne wakati mwisho 3 ili tu watimize matakwa ya mafisi m...kanuni ya wanawake na zanzibar mnayo nyie..bunge la Afrika mashariki haina kanuni za kibaguzi hizo.
CUF walionekana 4 ingawa ukweli CUF Lipumba walipeleka 3 na CUF Maalim walipeleka 1 bahati mbaya au nzuri hili lilifukiwa kwani CUF ni moja tu na sio mbili. Lakini CCM kwa kuwalundika kapu moja waliamua kumtosa yule wa CUF Maalim kimkakati (si wao ni Ukawa) na kumchagua Mnyaa (CUF Lipumba). Kuna mbunge alijaribu kuuliza hili lakini Spika akamburuza na kumwambia barua aliyojibiwa imefutwa. Bado nasubiri kuwasikia CUF Maalim kuhusu kulichotoke jana.
 
Usitake kutuaminisha kwamba hamkumchagua Masha kwa sababu ya kujilia makange ya tilapia na kunywa bia ya hineken. Kama ni hivyo, basi mna vigezo vya ajabu kweli kweli. Nataka nikujuze tu kama ulikuwa hujui. Huko miaka ya nyuma palikuwepo na waziri mmoja aliyependa kunywa sana whisky na mara nyingi alikuwa hakosi Hugos kwa wanamasantula kujirusha, mwisho wa siku alikuja kuwa rais wa nchi hii.

Huyo atakuwa Rais wa juzi juzi, kwa sababu Hugo Restaurant yenyewe ni ya juzi tu, kuna Rais alikuwa ni patron wa Palm Beach Hotel akiwa Waziri pamoja na rafiki yake aliyekuja kumfanya Waziri Mkuu.

Lakini alikuwa hanywi wakati wa kazi na kufanya ubishoo wa ujana kama Masha na Rose Garden. Obviously waziri wa Nyerere that did not cross your mind, usingethubutu.

Kuna mbunge jana amemuuliza kijana wa Waziri Maghembe, utaepuka vipi pitfalls za ujana, kwa sababu wanajua jinsi immaturity na vyeo vinavyovuruga akili za vijana. Shyrose Bhanji comes to mind as another victim of youthful indiscretion.
 
Piga ua hawa CHADEMA wakienda mahakamani watashinda.
Hakuna kura ya ndiyo au hapana
TUSUBIRI
 
CUF walikuwa na moja lakini wakatoa wagombea pande zote na jinsia zote. CHAMDOMO na nafasi 2 walishindwa nini?
Kwamba hujui kua cuf iko kambi mbili ya seif na pumba?, na aliyechaguliwa ni yule aliyetakiwa na walio ruhusu cuf ziwe makundi mawili
 
Piga ua hawa CHADEMA wakienda mahakamani watashinda.
Hakuna kura ya ndiyo au hapana
TUSUBIRI

Hapa Tanzania hicho kitu kinaitwa kuingilia uhuru wa bunge.

Labda mahakama ya EA.

Hakuna jaji nchi hii atatengua settled process ya Bunge na serikali. Hakuna kwenye balls hizo.

Jaji Lugakingira na Mwalusanya wameshakufa, wao wangeweza, sio hawa majaji wa Kikwete.
 
Kwa muda mchache nilioangalia mchakato wa uchaguzi jana nimegundua chadema wa kizazi hiki au awamu hii wepesi sana na wanazidiwa ujanja au mbinu kisiasa na CCM Bungeni.

Kwa chadema ya awamu zilizopita kilichotokea jana wangekiona hata kabla hawajachagua hao Watu wawili.

Bunge linakosa mvuto kuwa na wapinzani wanaolialia kwa udhaifu waliojitengenezea. Utumbukia kwenye shimo ulilochimba mwenyewe alafu unamlaumu mpita njia kwa nini hakujali...

"Chadema wa sasa Sio mitandaoni hata Bungeni wako Hatua moja nyuma ya CCM"
Ungemalizia kabisa umeposti kwa hisani ya .........
 
Tukisikia awamu hii makao makuu wanahamishia Kenya au Burundi tusishangae, manake tumechangua wenyewe watu wepesi mno, wabunge hawapo siriaz kabisa yan wanamwacha taslima wanampeleka yule jamaa wa mkanyageni hats kijieleza tu anajikanyaga, ataweza kweli kuchambua Sera? ccm wanasahau kuwa wabunge wa Tanzania wakivurinda huko ni aibu inapata serikali Yao ya ccm
 
chama kinachojipambanua kutetea wananchi

Wanakosa umakini kisa kutawaliwa na kuendekeza ubinafsi.

Kila siku wanahubiri democracy kumbe wenyewe wala hawaijui, wala hawaitaki hiyo democracy. Iweje kwenye uchaguzi wa BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI wamepata nafasi mbili;

1)Wameshindwa kutoa Fursa kwa Idadi kubwa ya wagombea ili kuwapa wapiga kura wigo mpana wa maamuzi kama CCM na CUF walivyofanya.Wao nafasi mbili wanatoa kwa watu wawili na kutaka kulazimisha bunge kuwapitisha bila kupingwa na hivyo kuikanyaga demokrasia. AIBU!!

2)CDM inaundwa na wanachama wa jinsia zote,wanawake na wanaume lakini kuna jumuia ya vijana (bavicha). Wao kwa wananchi wanahubiri Fursa Sawa kwa jinsia zote, lakini linapokuja suala la Fursa za ubunge wa afrika mashariki wanawake hawana nafasi kabisa. AIBU!!

3)Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania inaundwa na nchi mbili - Tanganyika/Tanzania bara na Zanzibar /Tanzania visiwani. CCM wameweka wagombea wao kwenye uchaguzi wa bunge la Afrika mashariki kwa kuzingatia pande zote mbili,wao Chadema wanajinasibu kuwa ni chama cha kitaifa! lakini wameleta majina ya wagombea wawili,wote kutoka mkoa mmoja,wote kutoka MWANZA..... Hii tunaitaje? .. AIBU.

Uchaguzi huu unafuatiliwa kote Afrika mashariki, kwa kuwa Tanzania ni taifa kubwa na lenye ushawishi mwingi , hii ni aibu kwa chama kikuu cha upinzani, aibu,aibu aibu,aibu,aibu, aibu,aibu!!
Daaah na wangekua wanatoka ukanda wakaskazin nalo lingekua tatzo
Wallah kuwa mtanzania yataka moyo....
 
Hivi kwa mini hoja za ccem Jana bungeni zilikuwa zinafanana, yani kila anayesimama anasema hchohicho had mawaziri wao
 
Acha ccm waendelee kuchelewesha, natamani chadema nao wasiteue mapema halafu bunge la EALA liseme tumechelewa halafu wafute uwakilishi wa Tanzania, yaani natamani kweli ingekuwa hivyo ili viwavi jeshi wa kumaliza wengine waipate chungu ya hujuma.
Mjomba usijipe Matumaini hewa. Soma kanuni za bunge la EALA vizuri
 
Hapa Tanzania hicho kitu kinaitwa kuingilia uhuru wa bunge.

Labda mahakama ya EA.

Hakuna jaji nchi hii atatengua settled process ya Bunge na serikali. Hakuna kwenye balls hizo.

Jaji Lugakingira na Mwalusanya wameshakufa, wao wangeweza, sio hawa majaji wa Kikwete.
Lakini tukubaliane CHADEMA wasipopeleka wabunge,hata hao wa CCM na CUF hawataapishwa kwenye bunge la EALA mpaka wafike wote tisa na huapishwa wote kwa mpigo kama nchi siyo kila mtu peke yake
 
Kwa muda mchache nilioangalia mchakato wa uchaguzi jana nimegundua chadema wa kizazi hiki au awamu hii wepesi sana na wanazidiwa ujanja au mbinu kisiasa na CCM Bungeni.

Kwa chadema ya awamu zilizopita kilichotokea jana wangekiona hata kabla hawajachagua hao Watu wawili.

Bunge linakosa mvuto kuwa na wapinzani wanaolialia kwa udhaifu waliojitengenezea. Utumbukia kwenye shimo ulilochimba mwenyewe alafu unamlaumu mpita njia kwa nini hakujali...

"Chadema wa sasa Sio mitandaoni hata Bungeni wako Hatua moja nyuma ya CCM"


Labda nikuulize chadema wamevunja kanuni gani?
 
Keep in mind kuna mwenzao wa C.C.M. wamempa kura 23, kundi la Tanzania Bara C.C.M, his presentation was so horrendous mpaka wakasema hawataki hata kumuuliza swali hata moja. Hawakuweka u-chama mbele

Masha amepata kura 126, Wenje 124. Hapa C.C.M wangeleta uchama kina Masha wangepata kura za kina Mnyika na Mbowe na Heche, hazifiki 40. Ma rekodi machafu ofisini na mtaani ndio yamewaangusha.
Kama hawajaweka uchama mbele hao wabunge 7 wataapishwa? bila kua na idadi kamili ya watu 9..rekodi chafu ofisini na mtaani inahusika vipi kwani wananchi wamepiga kura huko bungeni au hao wabunge..pia naomba uniambie waliopiga hizo kura za hapana..narudia Tanzania kuendelea haiwezekani watu wanapeleka AG huko EALA sisi tunapeleka watu wasioweza hata kutoa ushawishi...
 
Waende tu pungufu hivyo hivyo.Si wamejina wanatosha#Chuki za kijinga
Tanzania haiwezi kuendelea hata siku moja na mpaka leo hakuna hata kiwanda kimoja kilichoanzishwa..
 
Back
Top Bottom