Kwanza tukubaliane, uchaguzi wa wabunge wa EAC jana haukuwa strictly partisan, vinginevyo Masha na Wenje wangepata kura 40 za CHADEMA wenzao peke yao.
Kwa hiyo kama C.C.M. kwa kiasi kikubwa waliweza kuweka vyama pembeni, kuna nini kingine kilichosababisha kukataliwa kwa wagombea wa CHADEMA?
Nataka kujikita kwa Lawrence Masha, Waziri na mtumishi wa umma mstaafu, mwanasiasa mzoefu, mwenye elimu na exposure kutoka ndani na nje ya nchi, mwenye uwezo mahiri wa kujieleza Kiingereza ( bahati mbaya sana bado tunatumia hii litmus test kupima weledi wa Mtanzania), na pia mtaalam mwanasheria wa moja ya most prestigious law firms in the nation (IMMMA), na pia mtu mwenye political pedigree, yani uzao wenye historia ya utumishi na uongozi (Baba yake Lawrence Masha ndie alikuwa Nape Nnauye wa Nyerere, msemaji wa TANU wakati wa kipindi kigumu cha kutangazwa, kuenezwa na kupingwa Azimio la Arusha, kabla hajafukuzwa kundini kama Nape.)
Sasa kwa nini Masha akataliwe kwa kura iliyosema "bora tusipeleke mtu EALA kuliko wewe"?
Ukipima kwa vigezo, uzoefu wa kisiasa, kiutawala, kitaalam, kibiashara, Lawrence Masha ana credentials ndefu kupita wote waliohojiwa jana pale in my book. Na katika kujieleza alinivutia kuliko hata kijana wa Maghembe aliyewakuna wabunge kwa Kiingereza laini na utani wa kusema ana sura changa kwa sababu ya vinasaba vyake. Utoto ambao Masha hakuufanya. Masha muda wote ali get to the issues, akiwa very serious minded na akawaomba wamchague japo ni CHADEMA, kwa sura ngumu lakini kwa unyenyekevu mkuu.
Tatizo lililomwamgusha Masha, ukiacha siasa za vyama, ni matatizo ya ujana siku za nyuma, Uwaziri wa Rose Garden!
Watu hawajasahau alivyodharau uongozi aliopewa na JK akageuza ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuwa ni kwenye ki restaurant cha Rose Garden. Au ki saloon cha Mikasi, kuhojiwa mambo ya nchi kwenye TV huku unafanyiwa pedicure na manicure na haircut. Sijawahi kuona hata huko nje kwenye uhuru wa kila kitu na ma fashion yanakotokea ukakuta Waziri anajibu masuala ya nchi yuko salon anafanyiwa pedicure and manicure na haircut. Unageuza ofisi kuwa vijiwe vya vijana wenzio na wapiga dili wa mjini wakati ule wa Kikwete, mmezungukwa na michepuko yenu mnakula Heineken na makange ya Tilapia wa Kienyeji. Mida ya kazi.
Angalizo kwa vijana madarakani, umesoma au hukusoma, umechaguliwa na wananchi au umependwa na kulindwa na mamlaka za uteuzi, mkumbuke kuna kesho na kesho kutwa, na watu wanakumbuka, basi mjiheshimu wenyewe na kuheshimu dhamana zenu na Wananchi.