Nini hatma ya nafasi 2 za CHADEMA Afrika Mashariki

Mungu pekee ndiye anayejua majaaliwa ya akina Masha na Wenje.. ..

We as human beings can't predict anything.....
 
Kwa muda mchache nilioangalia mchakato wa uchaguzi jana nimegundua chadema wa kizazi hiki au awamu hii wepesi sana na wanazidiwa ujanja au mbinu kisiasa na CCM Bungeni.

Kwa chadema ya awamu zilizopita kilichotokea jana wangekiona hata kabla hawajachagua hao Watu wawili.

Bunge linakosa mvuto kuwa na wapinzani wanaolialia kwa udhaifu waliojitengenezea. Utumbukia kwenye shimo ulilochimba mwenyewe alafu unamlaumu mpita njia kwa nini hakujali...

"Chadema wa sasa Sio mitandaoni hata Bungeni wako Hatua moja nyuma ya CCM"
 
Jitafakarini sana CHADEMA. Hayo makundi mawili ni muhimu sana. Katika kuwahadaa watanzania angalau mngetafuta mwanamke ambaye kwa akili zenu ni dhaifu kabisa na mzanzibari mnaodhani kwa akli zenu ni dhaifu sana wakawasindikiza Wenje na Masha, yote hayo yasingetokea. Mnakwenda kuwaweka watu wa kutoka MWANZA tu wakati Tanzania hii ni kubwa sana, inatoka Namanga hadi mbambabei, inatoka Pemba hadi kigoma, inatoka Tunduma hadi Sirari.
 
chama kinachojipambanua kutetea wananchi

Wanakosa umakini kisa kutawaliwa na kuendekeza ubinafsi.

Kila siku wanahubiri democracy kumbe wenyewe wala hawaijui, wala hawaitaki hiyo democracy. Iweje kwenye uchaguzi wa BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI wamepata nafasi mbili;

1)Wameshindwa kutoa Fursa kwa Idadi kubwa ya wagombea ili kuwapa wapiga kura wigo mpana wa maamuzi kama CCM na CUF walivyofanya.Wao nafasi mbili wanatoa kwa watu wawili na kutaka kulazimisha bunge kuwapitisha bila kupingwa na hivyo kuikanyaga demokrasia. AIBU!!

2)CDM inaundwa na wanachama wa jinsia zote,wanawake na wanaume lakini kuna jumuia ya vijana (bavicha). Wao kwa wananchi wanahubiri Fursa Sawa kwa jinsia zote, lakini linapokuja suala la Fursa za ubunge wa afrika mashariki wanawake hawana nafasi kabisa. AIBU!!

3)Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania inaundwa na nchi mbili - Tanganyika/Tanzania bara na Zanzibar /Tanzania visiwani. CCM wameweka wagombea wao kwenye uchaguzi wa bunge la Afrika mashariki kwa kuzingatia pande zote mbili,wao Chadema wanajinasibu kuwa ni chama cha kitaifa! lakini wameleta majina ya wagombea wawili,wote kutoka mkoa mmoja,wote kutoka MWANZA..... Hii tunaitaje? .. AIBU.

Uchaguzi huu unafuatiliwa kote Afrika mashariki, kwa kuwa Tanzania ni taifa kubwa na lenye ushawishi mwingi , hii ni aibu kwa chama kikuu cha upinzani, aibu,aibu aibu,aibu,aibu, aibu,aibu!!
 
Uliona cuf walileta wa nne wakati mwisho 3 ili tu watimize matakwa ya mafisi m...kanuni ya wanawake na zanzibar mnayo nyie..bunge la Afrika mashariki haina kanuni za kibaguzi hizo.
 
Acha ccm waendelee kuchelewesha, natamani chadema nao wasiteue mapema halafu bunge la EALA liseme tumechelewa halafu wafute uwakilishi wa Tanzania, yaani natamani kweli ingekuwa hivyo ili viwavi jeshi wa kumaliza wengine waipate chungu ya hujuma.
 
Uliona cuf walileta wa nne wakati mwisho 3 ili tu watimize matakwa ya mafisi m...kanuni ya wanawake na zanzibar mnayo nyie..bunge la Afrika mashariki haina kanuni za kibaguzi hizo.
Kasome vizuri Mkataba Wa EAC kuhusu Wabunge Wa EALA ndo useme huu ujinga wako
 
Halafu uchaguzi Wa ndani ukifika utaona CHADEMA wanavyojipitisha Zanzibar na ngonjera za UKAWA. wanawaona Wazanzibari Mazuzu yao ya kupitia kutafuta madaraka
 
Mimi nimeelewa kati ya wabunge 9... 1/3 wawe jinsia tofauti..chadema wana viti 2 ccm 6, cuf moja..tatizo mna kariri..ccm wakifanya mnataka na wapinzani wafanye..
 
Mimi nimeelewa kati ya wabunge 9... 1/3 wawe jinsia tofauti..chadema wana viti 2 ccm 6, cuf moja..tatizo mna kariri..ccm wakifanya mnataka na wapinzani wafanye..
Lini CHADEMA watafanya? Wao kila siku wanafanyiwa?
 
Back
Top Bottom