ukiwaweka waajiriwa kwenye kapu moja la uadilifu,wenye kukosa uwezo wa kujenga hawatakuwa askari na waalimu peke yao,hapo ndio utajua bado tz kwa ujumla wake haijafika popote.
kama mtu analipwa mil 1.5 na anajiona analipwa vizuri hili ni tatizo,tafuta sasa hawa wanaolipwa 1.5 mln ni wangapi nchini.
ndio maana mentle wangu kiduku lilo huwa analalamika kwamba hata huko barabarani anakutana na vifaa vimebeba watu ndani vikitembea,vimeandikwa vits,noah,toyota,carina nk[emoji1][emoji1][emoji1].anajiuliza inakuwaje watu wananunua hivyo??jibu ni kwamba ndio msuli wao umeishia hapo.
Mimi kwangu nina kanuni kadhaa.
Kwanza kabisa, Waingereza wanasema "live and let live".
Maana yake, wewe ishi unavyoona sawa, na waache wengine waishi wanavyoona sawa. Hususan kama hawajakuingilia katika reli zako. Sijui kwa nini mtu kaamua kuwa muajiriwa. Pengine ndiyo mwisho wa uwezo wake, pengine karithi kazi waliyofanya wazazi wake, pengine ni ajali ya kihistoria.
Watu tofauti huwa wanatafuta vitu tofauti katika maisha. Mtu mwingine anatafuta fedha na umaarufu. Mimi nilipata nafasi ya kuwa maarufu sana, nikaikimbia, kwa sababu katika maisha yangu sitaki umaarufu. Kuna wengine wanataka waguse maisha ya watu wengi kwa kuwafundisha, wanakuwa walimu huku wakijua ualimu hauna malipo sana, ni kazi ya wito. Sasa mtu aliyeamua kufanya kazi ya wito yenye mshahara mdogo, ukim judge hajajenga nyumba, mwisho wake utaenda kuwa judge watawa waliokana mali na familia kwamba nao hawajajenga nyumba.
Kwa hivyo naishi ninavyoona mimi sawa, na wengine nawaacha waishi kivyao bila kutaka kuwaona wamefeli maisha.
Lakini pia, katika kukubali kila mtu na tofauti zake, hata mleta mada naye namkubali.
Mleta mada ni kama mtafiti wa somo la uchumi au sosholojia anayeuliza maswali kuhusu jamii na ni kwa nini watu fulani wanaamua kufanya mambo fulani. Hili ni jambo zuri, kimsingi ni jambo la kisomi. Ila inabidi lifanywe kwa umaridadi wa hali ya juu na weledi wa kutonyanyapaa watu, maana ni rahisi kumlaumu mtu ambaye humjui na hujui masumbuko yake, matatizo yake.
Unaweza kujikuta unamlaumu muhanga, waingereza hili wanaliita "blaming the victim".
Yani, watu wamekandamizwa kimfumo, hawalipwi mishahara stahiki, mpaka kampuni za nje zinakuja nchini zinataka kuwalipa watu mishahara mikubwa zaidi (kwa sababu zinaona mishahara ya Tanzania iko chini sana) halafu Waziri wa serikali ya Tanzania anayakaripia makampuni ya nje kwamba yasiwalipe Watanzania mishahara mikubwa sana (true story).
Sasa katika nchi ambayo watu wanakuwa victimized hivi, na mishahara ni midogo, na gharama za maisha zinapanda sana kila mwaka, mimi kuwalaumu watu wasioweza kujenga napata tabu sana. Si waajiriwa tu, hata wasio waajiriwa.
Ukielewa uzito wa swali hili, utaliheshimu zaidi na kujua kwamba, hakuna jibu moja la jumla linalokuwa kweli kwa watu wote, na ili kupata jibu la maana, uchunguzi wa makini wa "case by case basis" unatakiwa.
There is a Ph.D thesis in the questions raised by this thread.
Kwa nini kwa mfano, watu wanaamua kusomea ualimu, wakati taaluma ya ualimu inadhalilika sana kwa kipato, licha ya kuwa muhimu sana.
Wanakosa nafasi nyingine na wanaamua kujishikiza tu? Wnataka kufunza wanafunzi wengi watakaosaidia sana baadaye? Wanapenda kuchapa wanafunzi na kuogopwa?
Je, ukiwa unafanya kazi ngumu inayohatarisha maisha, ambayo inadharaulika na jamii, kama polisi, ukalipwa mshahara duni, katika jitihada za kuitunza familia yako, ukichukua hela kinyume cha sheria (rushwa) ili ujikimu, hilo ni jambo baya?