Nini hasa dhumuni la nchi kuwa Huru?

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,777
8,964
Kwa muda mrefu sana imekuwa ikinisumbua kuelewa hasa dhumuni la nchi hasa za kiafrika kudai uhuru wetu ikiwa matokeo ya uhuru huo umekuwa na matunda mabaya sana kwa raia wake kisiasa na kiuchumi.

Je, dhumuni hasa lilikuwa kumwondoa mtawala mlowezi na badala yake kumweka mzawa?

Je, ilikuwa mategemeo ya wengi kubadilisha mkono wa mtawala wa uchumi toka mlowezi na badala yake kushikwa na mzawa?

Je, uhuru ulitakiwa kwa sababu ya haki za kibinadamu baada ya matokeo mabaya ya vita kuu ya pili duniani?

Hadi leo ndugu zangu sifahamu kabisa maana ya UHURU ikiwa wananchi wengi wa nchi zilizotawaliwa wamekuwa na maisha mabaya zaidi chini ya utawala wa mzawa. Adui mkubwa wa maendeleo ya mwafrika imekuwa mwafrika mwenzake. Umaskini wa mwafrika unazidi kukua baada ya Uhuru huohuo kuzua matabaka baina yetu. Kuna hao wanaosema afadhali hata mkoloni kwani alitutawala na bado alihakikisha uchumi wetu upo jtk hali nzuri kuondokana na balaa la njaa. Kifupi tulitawaliwa lakini bado jukumu la kuhakikisha tunakula vizuri lilikuwa bado la mtawala! Mwananchi mwenye njaa ni sawa na gari lisilokuwa na mafuta... haliwezi kwenda popote!

Msinielewe vibaya kwamba napendekeza kutawaliwa zaidi ya kujitawala! lakini nachoshindwa kuelewa ni maana ya kujitawala -uhuru! ikiwa kiongozi mzawa mwenyewe hana tofauti kwa mabaya na huyo mtawala mlowezi.

Umaskini afrika ni maradhi ya kujitakia na yawezekana kabisa kuwa UHURU wetu umetafsirika vibaya hivyo kupoteza malengo yake. Haya maswala ya utandawazi yatawezekana tu pale tutakapo weza kutambua sisi tumetoka wapi na malengo yetu ni kwenda wapi.!.. Nje ya hapo Uhuru kwa mwafrika ni mabadiliko ya sura ya mtawala. Mateso na dhulma zipo palepale isipokuwa tu anayekunyonya ni chawa sio kunguni!

Kwa mtazamo wangu naomba sana mchango wenu wanabodi kwa upeo wenye matumaini... upeo ambao unatutakia mabadiliko ndani ya vyombo vyetu vya siasa na uchumi ili kuboresha maisha ya wananchi.

Haki na amani isimame kama ilivyokusudiwa tulipokuwa tukigombea uhuru wetu...

Haki na amani iwe juu yetu sote!

Mwalimu Nyerere alisema haya:-


"Tuna maana gani tunapozungumzia UHURU? kuna mambo matatu, Kwanza ni Uhuru wa nchi kujitawala yaani uwezo wa wananchi wa Tanzania kujipangia maisha yao, wakijitawala wenyewe pasipo kuingiliwa na mtu yeyote asiyekuwa Mtanzania.

Pili, Uhuru wa kutosumbuliwa na njaa, Maradhi na umaskini na Tatu ni Uhuru wa mtu binafsi, yaani haki yake ya kuishi akiheshimika sawa na watu wengine wote, Uhuru wake wa kusema na kushiriki katika maaamuzi ya mambo yote yanayohusu maisha yake, na uhuru wa kutokamatwa ovyo na kutiwa ndani kwa kuwa tu kamuudhi mkubwa japo hakuvunja sheria.

Yote haya ni mambo yanayohusu Uhuru na hatuwezi kusema wananchi wa Tanzania wako huru mpaka tumehakikisha wana Uhuru wa mambo yote haya"
 
Ebu jamani tujiulize kitu kimoja. Ikiwa wakati tunaomba Uhuru wetu hatukuwa na wasomi:

Je, tuliutaka Uhuru kwa malengo gani?... yaani Objective ya huo Uhuru. Sasa ikiwa baada ya miaka 40 + bado wananchi wengi tuna-struggle kuupata huo uhuru uliokusudiwa iwe kiuchumi, Utawala ama haki za binadamu.

Je, kuna uwezekano hapa katikati tumebadilisha malengo? na sijawahi kuona hata siku moja wasomi wetu wakitupa statistics zinazohusiana na malengo ya Uhuru huo, mathalan toka mkoloni tumefanikisha hiki zaidi kwa kiwango kikubwa. nakumbuka huko kwetu Ukerewe tulikuwa na maji ya bomba miaka hiyo! leo hii ni hadithi tena kisiwa kilichopo lake victoria..Mpunga na matunda yalisafirishwa nje mikoani. samaki wa kila namna walipatikana leo hii yote haya ni hadithi tupu kwani hata historia yake hatuna.

Haya ukiangalia vita, hapa Afrika ndio kwanza vimekomaa na kuvunja record. Leo hii tunaambiwa watu waliokufa Kongo ni millioni 3.5 ambayo ni hesabu kubwa sana ikizidiwa tu na vita kuu ya pili ya dunia.

Sasa ebu nambieni hawa jamaa wapo uwani petu na madhara yake yanaonekana jinsi majambazi walivyojaa nchini. Tumeweza kupigana kuikomboa Msumbiji, Zimbabwe, Angola na hata Afrika ya kusini, nchi ambazo kiuchumi hazikutuathiri moja kwa moja kama ilivyotokea Rwanda, Burundi na sasa hivi Kongo. Wakimbizi wamejaa nchi hata miundombinu yetu ya toka uhuru haiwezi kabisa kuhimili uzito wa majukumu yanayotokana na ongezeko la watu. Sio Umeme wala maji nguvu zake zina kipimo... Huwezi kutegemea miundombinu iliyojengwa kwa kufuata hesabu ya watu millioni kumi leo hii kuifanyia kazi ongezeko la watu mara tatu.

Mwisho, ningependa zaidi kuelewa serikali yetu na hasa mashirika kama haya ya NGO yanashirikishwa vipi na maswala kama haya?.. Leo hii hatuwezi kuendelea kudai kwamba wananchi hawana elimu ya kutosha kuweza kuelewa ama kurudia upya dira ya Uhuru wetu ili tufikie malengo yaliyokusudiwa toka mwanzo. Kuwaelimisha wananchi biashara na taratibu za utandawazi ni hatua moja wapo ambayo kusema kweli inatuvuta wengine hapa lakini elimu pekee bila kuwepo nyenzo na hasa kwetu waswahili mifano bora huchukuliwa kama hadithi za simulizi.

JF sijui ina mikakati gani ktk kuanzisha vituo vya elimu ya uzalishaji na Biashara kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuanzisha Union ambazo zitawapa mwongozo na kuwa mfano hai kwa wananchi wengine.
 
Willo,

Karibu sana ndugu yangu. Nashukuru sana kwa kunipa mwanga huo kwani kila napojaribu kutafuta dawa ya radhi hili la umaskini huwa nashindwa kabisa kuelewa chanzo chake! Na hasa maradhi haya yanaambukizwa na virusi gani!

kwa hiyo ndugu yangu, swala la uchumi wetu haliwezi kuwa rahisi kwa mtanzania myonge ikiwa hakuna sheria ya kiuchumi inayomlinda. Na hao wanaoshika nguzo zote za uchumi wetu ni watu wa kuja yaani wageni, jambo ambalo kwa mshangao nimeona kichwa cha habari ktk jarida - maskani ya tovuti hii limepongeza sana juhudi za Mkapa na hali ambayo TZ ipo leo hii. Kwa mtazamo wa haraka naweza kusema kweli kuna mabadiliko mengi ya kiuchumi na mikakati mingi imeanzishwa lakini kama ulivyosema hapo juu.

Wananchi hawakuandaliwa KABLA ya zoezi zima kuanza. Je, kuna uwezekano jamaa zetu akina Idd Simba sio waathirika wa mfumo mzima wa uchumi nchini. Na ikiwa ndivyo ilivyotakiwa kuwa isipokuwa kosa ni elimu ya Utandawazi kwa wananchi... Je, hao wananchi baada ya elimu wataanzia wapi ikiwa nguzo hizo bado zimeshikwa na baadhi warithi wachache? Je malengo yetu ni kuongeza nguvu ipi hasa na kwa faida ya nani?

Ni matumaini yangu bodi hii ya JF itawalenga sana wananchi wenye uwezo wa kuzalisha isipokuwa wamekandamizwa na hawa warithi wasiokuwa na uchungu. Wavuvi wa Sangara huko Mwanza, Wachimba madini huko Arusha na Songea, wafugaji wa ng'ombe, Wakulima wa mazao wote wapatiwe chombo ambacho kitawasaidia kujiendeleza. Isiwe kabisa dhumuni la JF ni kutoa elimu kwa wananchi hali sheria haiwalindi! wala hakuna chombo ambacho kinaweza kuwapa taarifa za soko huria! na wapi pa kuuza mali zao bila kupitia kwa wahindi. Mfano wa zao la Korosho kupitia India na sangara kununuliwa kwa bei hafifu hali inauzwa nje kwa bei mara mia nane ya bei ya mvuvi sii haki. Ikiwa kweli uwekezaji ni machine ambazo hazina gharama kubwa sana basi halmashauri za mikoa ziwe msitari wa mbele kuhakikisha wazawa wanapewa mikopo kupitia jumuiya zao ama chombo hiki.

Wakati umefika kwa wananchi tuweze kuziona tofauti kati ya ukoloni na Uhuru kwa mazuri yake...hasa tukizingatia utandawazi.
 
Jibu rahisi na la mkato la kukujibu ni kwamba "BADO HATUJAPATA UHURU" hivyo inabidi waafrika tupiganie upya uhuru wetu!

kwanza kabisa hakukuwa na kitu kunachoitwa uhuru pale mlipopewa huo 'uhuru hewa' mwanzoni mwa miaka ya sitini, bali kilichojitokeza ni "mabadiliko ya mfumo wa ki-uchumi wa dunia (wa wakoloni)"

Kikubwa kinachoiathiri Afrika ni "FIKRA" potofu na za hatari walizonazo "wazungu na wasio waafrika" (non-blacks/hasa wazungu), fikra za kwamba mwafrika si binadamu aliyekamilika hivyo hastahili kuishi katika mazingira mazuri. hizi ni fikra za ki-baguzi na za baadhi ya binadamu kujiona wao ni "binadamu walio kamilika au walio katika kiwango fulani cha u-binadamu kuliko wengine.

hili ni dhahiri pale tunaporejea katika historia, mifumo yote ya ki-uchumi iliyoanzishwa duniani na kufikia kiwango cha kimataifa ni mifumo inayomnyonya, inayomdhalilisha na kumtendea maovu yote mwafrika, ingwawa bara la afrika ndilo limekuwa bara lenya rasilimali nyingi na zinazoendeleza mabara mengine.

Kati ya hiyo mifumo, ipo iliyovuma na isiyosahaulika kama UTUMWA, UKOLONI, na UKOLONI MAMBO LEO, nayote hiyo ilikuwa ikibadilika toka mfumo mmoja hadi mwingine kulingana na maendeleo ya kijamii, kisayansi na kifikra ya watawala na watawaliwa. kwa sasa tunayo mifumo ya UBINAFSISHAJI na SOKO URIA chini ya UTANDAWAZI, mifumo ambayo inatokana na mabadiliko ya UKOLONI na UKOLONI MAMBO LEO, yaani utandawazi ni sawa na ukoloni wa kisasa!

Wakoloni waliwatumia wenyeji katika kutawala na kujipatia rasilimali, watu kama MANGUNGO WA MSOVERO tunajua nini alikifanya! Pale ambapo walikataliwa basi walitumia nguvu na tunakumbuka nini kiliwafika WAZAWA waliokataa kutawaliwa kama kina KINJEKITILE na MKWAWA nk.

Sasa katika utandawazi hali ni hiyo hiyo, wakiloni wa kisasa wanawatumia watawala WAZAWA kujipatia wanachokitaka, MKAPA na KINJEKITILE hawana tofauti isipokuwa tu enzi za kinjekitile hatukuwa na INTERNET!

Pili vita inayotokea mahala pote duniani, iwa ni ya wenyewe kwa wenyewe, au baina ya mataifa, haina tofauti kabisa na vita ya enzi za mkwawa na kinjekitile.

wakoloni waliwapiganisha au kuwagombanisha wenyeji na ndicho kinachoendelea kwa sasa barani afrika na mahala penginepo., inaendelea..........
 
Jamberi,

Ndugu yangu hakika umenipa somo!...

Maelezo yako yanatisha pamoja na kwamba ndio ukweli wenyewe...Kusema kweli Afrika kila kiongozi huingia Ikulu kutatua matatizo yaliyoachwa na kiongozi aliyemtangulia...Leo hii tunaona JK akijifunga kibwebwe kufagia machafu yote ya Mkapa, wala hatufahamu itachukua muda gani ufagizi huu na kwa kipindi gani patakuwa safi!... Hapo hapo hakuna maandalizi la kuhakikisha uchafu huo haurudi tena yaani ufagiaji unatupiwa chini ya uvungu. wakati zoezi la kusaka majambazi linaendelea Dar huko mikoani hakuna kitu.. yaani majambazi yanakimbia na kujichimbia bara. Hakuna mpango wa kuhakikisha wananchi wanapewa vitambulisho vya uraia nje ya passport!..hatuna data base ya aina yeyote zaidi ya akaunti ktk benki zetu. Hakuna jitihada za kuhakikisha mishahara haitolewi kwa fedha taslimu na wazawa wanapewa nafasi kwanza mbele ya mgeni. Vitu kama hivi vidogo vidogo lakini vinaweza kabisa kuleta mabadiliko makubwa.

Nafikiri, kulingana na maelezo yako hapo juu kuhusu Uhuru wetu, labda dawa - Watawala wa wilaya hadi mikoa wanatakiwa warudi ma-chief ambao walikuwa na uchungu na himaya zao na kulingana na tamaduni za mwafrika nimegundua kwamba kila kiongozi aliyeshika madaraka (rais na mawaziri) ameweza kuleta mabadiliko kwao zaidi. Sio rais wala waziri wote wamejenga makwao na wale ambao hawakufanya hivyo basi wamejenga kwa mke ambako kapewa ufalme mdogo wa nyumba. Kuna haja ya kuwa na senate inayoongozwa na machief badala ya viongizi wa vyama vya kisiasa ambao wanazidi kututenganisha siku hadi siku.
 
Mkandara, nakuongezea kitu kimoja walichokisahau kina Juliasi wakati wanakabidhiwa nchi.

VIONGOZI WA KIAFRIKA WALISAHAU (AMA WALINYAMAZISHWA) KUOMBA FIDIA ZA UKOLONI, yaani ukoloni unatakiwa ujulikane kwamba lilikuwa kosa la jinai na waliotenda wanatakiwa washitakiwe na walipe fidia.

Sio kila siku wanatuzuga eti tuna madeni, nasi tuwaeleze wazi kwamba walitukosea na kutuibia hivyo wao ndio wanastahili kulipa!
 
Nakubaliana na Jamberi kwamba huo uhuru unaouzungumzia bado kabisa hatujaupata, huu tulionaoni fantacy tupu lakini sio uhuru kwa maana ya uhuru.

Kwanza ni vyema tufahamu definition ya uhuru au kuwa huru, maana yangu ni kwamba kuwa huru ni uwezo wa wananchi wa nchi fulani kuwa na uwezo wa kutembea kifua mbele, ukiangalia hapa kwetu wengi hawana uwezo huo, unakuta mzawa haruhusiwi kuingia au kufika sehemu dfulani kwa sababu za kijinga kabisa eti ni sehemu za watalii,sasa hapa uhuru uko wapi?

Au tunapotezeana muda tuu. Kama alivyosema Jamberi ipo siku tutaanza kuupigania huo uhuru wa kweli yaani uwezo wa mzawakutembea kifua mbele kama jamaa zetu Gikuyus walivyopigania kule Kenya, sijui kama bado mnakumbuka MauMau hawa watu ndio waliupigania uhuru kwa sababu kwamba nao waweze kutembea kifua mbele na matokeo yake wakajikuta wanarudia makosa yale yale ya muzungu kwa kujipa kipaumbele wenyewe wakikuyu ndio number one nchinio humo mpaka sasa, hayo ni makosa ambayo yafaa yaangaliwe kwani tusije tukajikuta tunapigania uhuru wa group fulani la watu na wengine kuachwa kama ilivyo Kenya, tatizo kubwa ninaloliona hivi leo ni class struggles kama alivyosema mtu mzima Max na Frederic Angels kwenye communist manifesto

Peace!
 
Willo,

Shukrani sana tena mifano kama Kenya ndio hasa hunifanya mimi kujiuliza mara mia nini hasa wazee wetu walipigania maanake matokeo ya uhuru huu hasa nchi za kiafrika ni mabaya zaidi. Leo hii kila kiongozi anayekuja kupinga ugandamizwaji wa wazawa wananchi wenyewe kwa faida ya wageni huonekana adui mkubwa!...

Kiongozi mzuri ni yule anayetetea wageni kuchukua upya urithi na uwezo wa kutembea kifua mbele. Tunafanya vita wenyewe kwa wenyewe kwa faida ya huyohuyo tuliyemfukuza, demokrasia na utandawazi umepewa sura mpya kuondoa kabisa UHURU wa mtu mweusi... Na kizazi hiki hakika sidhani kabisa kuna mmoja kati yetu anaweza ku-define UHURU kwa maana ambayo wazazi wetu walipigania.

Je, ina maana ndugu zetu walikufa bure kuutafuta huo uhuru usiojulikana? Na hiyo vita mpya ya kuutafuta upya UHURU itakuwa na tofauti gani ikiwa bado hatufahamu maana ya nchi kuwa huru.
 
Mkandara,

Nafikiri unatekiwa usome tena niliyosema awali, kwamba babu zetu (au baba zetu) walipigania uhuru wakijua maana ya kuwa huru kwani hawakuwa huru na walilijua hilo. Tatizo ni kuwa walidanganywa na wakoloni kuwa wamepewa uhuru na wachache waliojaribu kudai zaidi wakaonekana maadui wa demokrasia nk na hata wakapinduliwa au kuuwawa ( mfano ni jamaa wa kongo ya kinshasa kabla ya SESESEKO)

Sisi tunajua kwamba hatupo huru na siku tutakapoupigania uhuru wa kweli tutajua ni nini tunakipigania.
 
Jamberi,

Shukran za dhati nimekupata... ila tu nawe umeniacha nje!

Unaposema mazazi wetu walifahamu maana ya UHURU ni ipi hiyo maana.. Kutembea kifua mbele kama alivyosema Nd. Willo?... Na imekuwaje jamani hata huo Mfano wa Lumumba alipouawa ebu turudi nyuma! Watu hawa wamepigana kwa karne nzima dhidi ya mzungu kisha kaja mtu mweusi ambaye kawaweka chini sawasawa na mzungu waliyepigana nae lakini hapa walishindwa kuinua hata mkono zaidi ya huyo mmojammoja.

Toka Lumumba Wazaire walikaa kimya na kujisifia hali maisha yao mabaya kuliko hata Mkoloni, haya baada ya Mobutu mategemeo yalikuwa sasa UHURU wa kweli utapatikana maanake mabaya yote ya mtu mweusi na Mzungu yanajulikana... Matokeo yake ndio chaos kabisa wameuana zaidi kuliko hata mkoloni na Mobutu combined. Na ukiuliza wote watakwambia wanapigania kusimamisha demokrasia!

Ndugu zangu, mimi naamini ya kwamba AMANI hupatikana kwa taabu iwe vita ama maelewano lakini Demokrasia haiwezi kusimamishwa hata siku moja kwa kupitia vita.
 
Jamani eeh, naona mnasema mengi, hadi mambo mengine yanaleta tafsiri kana kwamba waasisi na waliotuongoza kupigania uhuru walifanya kazi bure.

Uhuru ni kujitawala, kujipangia mambo bila kuingiliwa. Tatizo kubwa ni umasikini. Hili ni lazima tulikubali.Siyo kwamba viongozi hawa hawakuwa wabunifu wa mambo, siyo kweli kama walitaka tuendelee kuwa masikini, la hasha! wakati ule kama mfavyojua, weupe walitaka kuendelea kututawala, walitufundisha kusoma na kuhesabu tu ili tuishie hapo. Hawakuwa wametoa fursa ya elimu kwa wote tukawa na mainjinia, madaktari, wachumi na wengine wengi wenye taaluma ambazo zingechangia mawazo huku viongozi husika wakasimamia mipango ya maendeleo kwa vitendo.

Baada ya uhuru mambo yalibadilika, Wengi walipata fursa ya kwenda shule, wakati ule mambo ya siasa ya ujamaa na kujitegemea ambayo baadaye wachache walidhani inawadondosha, lakinini wakajikuta wanadondoka wao na wananchi wote, waliamua kufuata mifumo mingine. Hili naona kuwa ni tatizo.

Kuna dhana iliyokuwa inatuelekeza kuwa ili tuendelee pamoja na uhuru wetu tunahitaji vitu vitatu, Watu, Ardhi siasa safi na uongozi bora. Pengine kulingana na mabadiliko ya maisha ningeongeza jambo la nne, fedha ambayo sasa imekuwa ndiyo msingi wa maendeleo. Sasa kwanini hatuendelei, tatizo li wapi? naona hili ndilo la kujadili zaidi badala ya kujadili uhuru.

Mchana mwema, nyonyo
 
Jamani eeh, naona mnasema mengi, hadi mambo mengine yanaleta tafsiri kana kwamba waasisi na waliotuongoza kupigania uhuru walifanya kazi bure.

Uhuru ni kujitawala, kujipangia mambo bila kuingiliwa. Tatizo kubwa ni umasikini. Hili ni lazima tulikubali.Siyo kwamba viongozi hawa hawakuwa wabunifu wa mambo, siyo kweli kama walitaka tuendelee kuwa masikini, la hasha! wakati ule kama mfavyojua, weupe walitaka kuendelea kututawala, walitufundisha kusoma na kuhesabu tu ili tuishie hapo. Hawakuwa wametoa fursa ya elimu kwa wote tukawa na mainjinia, madaktari, wachumi na wengine wengi wenye taaluma ambazo zingechangia mawazo huku viongozi husika wakasimamia mipango ya maendeleo kwa vitendo.

Baada ya uhuru mambo yalibadilika, Wengi walipata fursa ya kwenda shule, wakati ule mambo ya siasa ya ujamaa na kujitegemea ambayo baadaye wachache walidhani inawadondosha, lakinini wakajikuta wanadondoka wao na wananchi wote, waliamua kufuata mifumo mingine. Hili naona kuwa ni tatizo.

Kuna dhana iliyokuwa inatuelekeza kuwa ili tuendelee pamoja na uhuru wetu tunahitaji vitu vitatu, Watu, Ardhi siasa safi na uongozi bora. Pengine kulingana na mabadiliko ya maisha ningeongeza jambo la nne, fedha ambayo sasa imekuwa ndiyo msingi wa maendeleo. Sasa kwanini hatuendelei, tatizo li wapi? naona hili ndilo la kujadili zaidi badala ya kujadili uhuru.

Mchana mwema, nyonyo

Mkuu wangu nakusikia sana ila tu nashindwa kuyaunganisha mawazo yako na Ukweli...Unaposema Kujitawala una maana gani?..Maanake mfumo wa uongozi kiutawala hauna tofauti baina ya mkoloni na leo hii. Na unapozungumzia Umaskini pia sii kweli kwamba tulipokuwa tumetawaliwa swala la umaskini lilikuwa sababu ya kuutafuta UHURU..Hili halikuwa sababu wala sii tatizo linaloweza kusukuma maana nzima ya nchi kuwa huru UHURU isipokuwa umaskini ni MATOKEO ya utawala dhalimu.. hakuna alama nzuri ya kuonyesha utawala bora zaidi ya kufuta Umaskini..kwani utawala dhalimu wowote mkubwa umaskinisha watawaliwa. hili elewa, nani somo zuri sana la kupima uhuru na utawala bora

Kinachogomba hapa nadhani ni kuipoteza ile azma iliyowekwa ktk kuutafuta Uhuru... Kama sababu kubwa ya Uhuru ilikuwa kujitawala na kupanga mambo yetu wenyewe nadhani ipo haja kubwa ya kutafsiri vizuri hili neno KUJITAWALA.. kwa sababu matumizi ya kuwepo kwa serikali na viongozi ngazi ya chama inaondoa kabisa maana ya kujitawala. Chama tawala ndicho kinachotawa na chama hicho kinaweza tumia sababu zote za kiutawala kuwakilisha kundi lao liwe la kabila, dini ama rangi..
Maadam ipo serikali chini ya chama kinayotawala, basi wananchi watakuwa bado wanatawaliwa na serikali ya chama hicho iwe CCM ama Mkoloni. Tofauti baina ya CCM na mkoloni inakuwa ni baina ya mtawala mzawa na mtawala mlowezi..

Siwezi kuweka madai kwamba leo hii tunajitawala na kuamua mambo yetu wenyewe hali maamuzi yote makubwa ya maendeleo ya nchi hii yanafanywa na kundi dogo sana la Watawala..
Sasa ieleweke kwamba kisiasa hata mkoloni alifanya maamuzi mengi kwa faida ya nchi hali ukweli unaonyesha wazi ilikuwa kwa faida yao ama malkia, leo hii kinachotokea pia ni uongozi wa nchi zetu unafanywa na viongozi wenye rangi ya chama ambao pia wanatazama maslahi yao, chama na wafuasi zaidi ya maslahi ya nchi..

Badala ya mkoloni akitetea maslahi ya Malkia, leo hii tuna viongozi wanatetea maslahi ya chama mbele ya taifa. Na nina hakika ukiwauliza nafsi za viongozi wengi kuhusiana na yapi maslahi tangulizi baina ya nchi na chama watasema ya Taifa (Siasa) lakini ukweli ni kwamba maslahi ya chama hutangulia yale ya Taifa hadi leo hii..Hivyo Malkia wetu wa sasa hivi anakuwa chama tawala. Sheria zote zinatungwa na kupitishwa kulinda maslahi ya chama na viongozi wake kama walivyokuwa wakijilinda wakoloni.

Mfano mdogo ni huyu Mpendazoe, leo kujitoa kwake CCM imeonekana kama ni msaliti wa nchi nzima na sii chama, yaani kashindwa kulinda na kutetea maslahi ya chama..hakuna mtu anayejali nini malengo ya kujiengua kwake na wala hayana mjadala. Nguvu kubwa ya vyama vya upinzani ni kumwondoa CCM kama vile juhudi zilizotumika kumwondoa Mkoloni, na ukisoma hoja zao kwa makini, utaona sababu kubwa zinazotumika hazina tofauti na zile zilizotumika wakati wa mkoloni.

Kinachoninda mimi kuelewa ni pale chama tawala kinaposhindwa kuliona kalio lao wenyewe...chama kinaweza kueleza mabaya yote ya mkoloni lakini wakati huo huo kinaendeleza mabaya yaleyale ya mkoloni. Leo historia inajirudia kama vitabu vya dini vinavyosema (kuran)...tunaanza kuuza ardhi zetu kwa wageni kama walivyofanya mababu zetu tukitumia neno ukoloni mamboleo...tena kwa makusudi tunaitangaza nchi yetu,ardhi yetu kuwa ipo huru na kubwa kutawaliwa kiuchumi..Aint we going back in history?
 
Watu wasio na hatia wataendelea kumwaga Dau mpaka waishe Mjini Arusha na Wataendelea kupata Suport kutoka kona zote za Tanzania zinazopenda Maendeleo kuyapinga Maamuzi ya CCM ya kuzuia Maendeleo Nchini kiujumla,

Mapambano yanaendelea na SLaa hataki Tena mazungumzo na CCM
 
Iliyopata Uhuru 1961 NI TANGANYIKA!...na ndiyo hiyo inayotakiwa!
Hii nchi iliyotengenezwa mezani(Tanzania) bado ni koloni-kongwe la neo-colonialists!
Nadhani tunapoongelea katiba tuanze Taratibu kuongelea nchi yetu TANGANYIKA!
Tusimsahau Mc.Mtikila kwenye mikusanyiko yetu yoyote inayohusu katiba!
 
Iliyopata Uhuru 1961 NI TANGANYIKA!...na ndiyo hiyo inayotakiwa!
Hii nchi iliyotengenezwa mezani(Tanzania) bado ni koloni-kongwe la neo-colonialists!
Nadhani tunapoongelea katiba tuanze Taratibu kuongelea nchi yetu TANGANYIKA!
Tusimsahau Mc.Mtikila kwenye mikusanyiko yetu yoyote inayohusu katiba!

nadhani hapa suala siyo Tanganyika wala Tanzania suala letu la msingi tuchukue hoja za msingi kumi tuandike makala kwa nini tunahitaji katiba tuzisambaze kwa wananchi wazisome wazielewe ili ikifika nyakati muafaka tukitangaza maandamano nchi nzima ya kudai katiba watu wawe na msingi wa kujua amani ya maandamano hayo yatatuletea nini hapo siku zijazo

hivyo napenda kupendekeza kwa wakati huu tuandike makala tuombe nafasi katika magazeti yenye uthubutu kama Mwanahalisi na Raia Mwema kutupa nafasi ya kusambaza nia yetu hizi

asante
 
kuboronga kwa uchaguzi wa Miaka yote toka ianzishwe Vyama vingi, kula rushwa bila kushitakiwa, Kuiba pesa za Uma na Kula na Vigogo,, kuwaacha viongozi mafisadi wale Bata hakuna uhuru hapa
 
Tanzania si Nchi huru kabisa kwasababu hata vitu vingi sana vinakwenda kidicteta, Sasa hivi imetolewa Amri kwa Watumaji wa umeme wa Tanesco, ambao ni 99.09, wa tanzania ni watumiaji wa Tazesko tuongezewa Gharama za kulipia umeme,
Viongozi tulio wachagua kwa mbwembwe wapo na hawakulitetea wala kulitolea mawazo ili kupunguza Gharama za maisha za wananchi wao wanao wategemea,
yaani mimi naona kama hatuna selikali ni uchafu tu ulio kaa huko
 
Sasa nafikiri watu wameelewa kwanini nasema Tanzania si nchi huru,, yaliyo fanyika Arusha yamedhihirisha kabisa kuwa Hii si nchi huru jamani,, hii ni hatari Je Wananchi tuandamane kwa kile walichokifanya Askali wa Selikali ya CCM kwa wananchi wake?
 
Watu wasio na hatia wataendelea kumwaga Dau mpaka waishe Mjini Arusha na Wataendelea kupata Suport kutoka kona zote za Tanzania zinazopenda Maendeleo kuyapinga Maamuzi ya CCM ya kuzuia Maendeleo Nchini kiujumla,

Mapambano yanaendelea na SLaa hataki Tena mazungumzo na CCM

uhuru wa mamwinyi.

uhuru wa bendera na kushinda chini ya gorofa za wahindi kariakoo wakicheza bao na kunywa kahawa. na kanzu zao.
 
Back
Top Bottom