Nini chimbuko la Vita vya Uhujumu Uchumi - 1983-84? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini chimbuko la Vita vya Uhujumu Uchumi - 1983-84?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Dec 25, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  "Mikingamo... Sasa vita vimetangazwa jama, wananchi wote tuwe imara, vijijini na mijini tusisite kuwafichua wahujumu na walanguzi"

  Nini kulikuwa chimbuko la kuanzishwa kwa vita dhidi ya wahujumu uchumi, walanguzi na wafanya magendo?

  Sheria ya Uhujumu Taifa ya mwaka 1984 bado iko hai, kwa nini haitumiki?

  Nini kilisababisha kukawa na mshike mshike wa watu waliohodhi mali, kuwa na fedha za kigeni au bidhaa za kigeni? Je kulikuwa na uhujumu wa kiasi gani, Ulanguzi na Magendo ya kiasi gani?

  Faida na hasara za soesi zima zilikuwa ni nini?
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Dec 25, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,765
  Likes Received: 4,980
  Trophy Points: 280
  ..sheria ya wahujumu uchumi ilitungwa wakati "wahujumu" tayari wako rumande.

  ..hebu jiulize heshima ya Bunge letu ilikuwa ya kiwango gani wakati huo. pia jiulize kama kulikuwa kuna kitu kinaitwa rule of law.

  ..chimbuko la sheria ile na harakati za kuwakamata "wahujumu" uchumi ilitokana na imani ya Mwalimu na Sokoine kwamba wakikamata "wahujumu" basi matatizo yetu ya uchumi yatapotea.
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Dec 25, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,765
  Likes Received: 4,980
  Trophy Points: 280
  Rev.Kishoka,

  ..huwezi kuelewa kilichosababisha kampeni ya wahujumu uchumi bila kuzingatia hali ya uzalishaji wa bidhaa na uchumi ya wakati ule.

  ..kulikuwa na uhaba mkubwa wa bidhaa za viwandani. hiyo ikasababisha wananchi kutafuta njia mbadala za kukabiliana na hali hiyo. mojawapo ni wafanyabiashara kuingiza kinyemela/kimagendo bidhaa hizo toka nchi jirani.

  ..pia katika mazingira ya uzalishaji mdogo na uhaba wa bidhaa serikali ilikuwa ikipanga na kudhibiti[enforce] bei ya bidhaa. hali na mazingira ya namna hiyo husababisha wafanyabiashara kuficha bidhaa ili kulazimisha bei kupanda na kupata faida.

  ..matatizo hayo au challenges hizo ndizo zilizosababisha Nyerere na Sokoine kubuni mpango wa kukamata wahujumu uchumi kama remedy ya matatizo ya uchumi wetu.

  ..kampeni ya wahujumu uchumi ilishindwa kuondoa tatizo la uhaba wa bidhaa, actually kampeni hiyo ilizidisha machungu ya uchumi kwa umma wa wa-Tanzania.

  ..serikali iliumbuka, na badala yake wananchi wakaruhusiwa kuagiza bidhaa toka nje.

  NB:

  ..serikali imeingia hasara kwa kulazimika kuwalipa fidia watuhumiwa wa kimakosa wa kampeni ya uhujumu. zaidi ongeza gharama za kiutendaji za zoezi hilo. inasemekana kuna askari waliagizwa na serikali toka Msumbiji.

  ..vilevile kitendo cha serikali kulilazimisha bunge kutunga sheria ya makosa ya uhujumu uchumi wakati tayari inawashikilia rumande watuhumiwa wa kosa hilo ililitia dosari kubwa Bunge na demokrasia yetu.
   
 4. M

  Mama JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Hiyo sheria ya uhujumu uchumi imefunikwa na Azimio la Zanzibar (I hate this thing, I am sorry)
   
 5. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Rev. Kishoka,

  Ukweli wa mambo vita vya uhujumu wa uchumi vilikuwa ni siasa ya serikali kupata umaarufu at the expense of private business community.

  Principal ndogo tu ya supply and demand ndio iliyokuwa inaongeza bei ya vitu. Sera ya uzalishaji wa bidhaa za viwanda haikutosheleza mahitaji ya nchi na kusababisha uhaba wa bidhaa mbalimbali.

  Vita viliendesha na watu kutiwa ndani lakini bidhaa ziliendelea kuwa adimu. Na kitu kilichopunguza uhaba wa vitu ni kuruhusu uagizaji wa bidhaa kutoka nje.
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hata kama sheria ilitumika vibaya bado nadhani tunahitaji sheria kama hiyo (ambayo bado ipo) lakini ni lazima kuwepo na uadilifu katika vyombo vyetu vya sheria ikiwa ni pamoja na vyombo vya dola (PCCB, Polisi, UWT, Magereza) na mahakama ili kuhakikisha HAKI inatendeka kwa wahujumu uchumi wa kweli kuchukuliwa hatua na watu wema wote kutendewa haki bila kubughudhiwa.

  Nasema hayo kwa sababu WAHUJUMU uchumi bado wapo wengi na hawachukuliwi hatua na pengine wanaochukuliwa hatua wanalegezewa na baadaye wataonekana mashujaa walioonewa kwa sababu za kisiasa. Hii ni hatari kwani hakuna dalili za serikali ya sasa kufanikiwa kuwachukuliwa hatua WAHUJUMU wa KWELI kwani ni miongoni mwao
   
 7. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mada ni Vita vya uhujumu uchumi. Unajua kwanini watanzania mnashindwa katika masuala yenu?

  Kwa sababu mnafikiri kuna siku mtapata watu wema wa kuongoza vyombo vya umma na kujali maslahi ya Taifa.
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Now wait a minute, wakuu not that fast eti hii kitu ilikuwa idea ya nani hasa kati ya Mwalimu na Sokoine? I thought ilikuwa kitu ya Sokoine ndio maana ika-fail kwa sababu kwanza a sitting president was not on board, na the whole thing ilikuwa ni kusaidikika anyways maana hakukuwa na uhakika exactly kinachotafutwa kufanikishwa hasa kwa kuwarundika jela masikini wauza dawa za miswaki na sabuni mitaani tu, au!
   
 9. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  zilikua frustrations za a failing socialist economy. nadhani the word economy doesnt even begin to describe the situation, labda tuiite "eco.." maana ilikua kipande.
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Dec 26, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,765
  Likes Received: 4,980
  Trophy Points: 280
  FMES,

  ..idea ya kukamata wahujumu uchumi ilifeli kwasababu it was wrong to begin with. haijalishi who was on board with the idea, and who was not.

  ..Mwalimu na Sokoine walikuwa na mtazamo kwamba kamata-kamata ya "wahujumu uchumi" itajaza bidhaa madukani. baada ya muda hali ilizidi kuwa mbaya na ya kutisha.

  ..lawama za madhila yaliyotokana na kamata-kamata ile zinapaswa kubebwa na hao wawili. yalifanyika maandamano mwanzoni mwa kampeni hizo na Mwalimu akahutubia na kusema mwaka 83 hakuna lingine ila kuwafichua maadui wa ndani. hata John Komba aliimba wimbo kusisitiza kauli mbiu ya Mwalimu Nyerere.

  NB:

  ..kinachosikitisha ni ile hali ya wasiwasi iliyotanda wakati ule. wananchi waliigopa serikali yao wenyewe.

  ..kulikuwa na hofu kubwa kwamba hata katon moja ya sabuni iliweza kukupeleka jela na uhakika wa kutoka haukuwepo. kamata-kamata ile ilikuwa ikifanyika zaidi usiku wa manane!!
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Dec 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wanabodi,

  Wakuu zangu mbona mnasema vitu bila kumbukumbu ya matatizo tuliyokuwa nayo kisha mnazusha sababu kutokana na jinsi mnavyofikiria.

  Pamoja na ku fail kwa Uhujumu uchumi ni lazima tukumbuke kwamba Tanzania tulikuwa na matatizo makubwa ya ugawaji..halikuwa swala la demand na supply iliyotokana na uzalishaji bali matatizo yote yalitokana na magendo yaliyokuwa yakiendelea nchini.

  Nakumbuka vizuri sana mwaka huo na adha zote tulizozipata lakini ukweli ni kwamba viwanda vyote vya Tanzania vilikuwa vikizalisha kmali ambayo ilichukuliwa toka milango ya nyuma na kusambazwa nchi jirani. Toka sukari, matairi ya gneral Tyre, Korosho, Karafuu, sigara, pombe, Kahawa, Khanga, ,vitenge na hata sabuni za mbuni vyote vilikuwa mali ya kusafirisha nchi jirani iwe Kenya, Uganda, Rwanda na hata Arabuni.

  Ni kutokana na hali hiyo Tanzania tuliingiwa na upungufu mkubwa wa bidhaa ambazo kwa siasa za mwalimu zilikuwa kutuwezesha sisi wenyewe kuzalisha bidhaa muhimu ndani bila kutegemea nchi za nje. Ni wakati ambao mashirika makubwa ya ugawaji kama RTC, Gafco, BIT, Nasaco na mengine mengi tu yalikuwa sehemu za misheni town..Na kibaya zaidi wafadhili wakubwa wa misheni hizo za kupora mali zile walikuwa wahindi ambao ndio walikuwa wamiliki wa maduka.

  Jamani mtanisamehe lakini kila anapokuwepo mhindi kila siku tumeshuhudia uharibifu mkubwa wa sheria za biashara na bila kiongozi kutazama nyendo za hawa watu ktk uchumi wa nchi nina hakika kabisa wanaweza kuangusha nchi nzima kiuchumi..
  Uganda ambayo ilikwenda hatua moja zadi yetu na kuwafukuza wahindi, leo hii wamejiandaa vizuri kisheria na watu hawa kwa sababu waliweza kusafisha nyumba yao mhindi akiwa nje. Waliporudi wahindi wamekuta nchi ipo ktk hatua nyingine kabisa ktk kupigana na Hujuma za uchumi. waganda wenyewe ndio wamiliki wa mali nyingi na wao ndio wakulima, walanguzi na wauzaji wa mali zao iwe ndani ya nchi ama nje.

  Kwa hiyo wahindi wanajipanga kama sehemu ya kundi la wafanyabiashara badala ya nchi nzima kutegemea wahindi kuuza mali zao. Uganda wanapiga hatua haraka sana kuliko sisi na hata rwanda ambako wahindi wamekimbia vita wameanza kujijenga vizuri bila kuwepo wahindi.

  Kweli Sokoine alishindwa kwa sababu wezi wa mali zile hawakuwa wahindi bali sisi wenyewe tena wananchi wa hali ya chini wakitumiwa kusafirisha ama kupora mali zile.

  Sababu nyingine kubwa ni kwamba vita hivyo vilianza wakati tayari nchi imekwisha anza kuzama kama vile mashua iliyoingia maji ktk iinjini zake.. Huwezi kuziba tobo na kuondoa maji ukafikiria kwamba kazi imekwisha wakati injini nzima inahitaji kufanyiwa Ukarabati...

  Kwa hiyo sidhani kama tutakuwa tunazungumzia ukweli wa tukio hilo kwa sababu wakati vita hiyo ikiendelea Mwalimu Nyerere mwenyewe aliinua mikono kusalimu amri kiuchumi na kukubali kwamba Ujamaa umeshindwa...

  Ni kosa letu sisi wenyewe tulipoingia Ubepari wakati wa Mwinyi tulishindwa kufikiria kwamba Uhujumu uchumi pia ni kikwazo kikubwa cha Ubepari hivyo ulitakiwa kufutwa kabisa wakati injini mpya ya kuendesha meli yetu ikiwekwa...

  Kwa hiyi kifupi nitasema hivi Nyerere alisdhindwa kwa sababu alitaka kuziba tobo za hujuma bila kuisafisha injini ya kuendesha uchumi wetu kwa huko ndiko ma CEO wa mashirika hayo walitumaliza.

  Na Mwinyi alipoingia na kukuta injini zimeshika kutu alifikiria uamuzi wa busara ni kubadilisha injini nzima na kuweka mpya (Ubepari, lakini alishindwa kufikiria kubadilisha bodi zima la meli yetu ambalo lilikuwa tayari limeoza na tobo kibao za kuingiza maji.

  Matatiuzo ya Uhujumu uchumi yaliendelea kama kawaida na yamezidi kuendelea kwa sababu nchi yetu haina mwongozo kama nchi nyinginezo. Kama leo tunaona Azimio la Zanzibar halina kasoro na hakuna kiongozi hata mmoja anayefikiria kuna hitilafu kubwa ktk azimio hilo basi Tanzania nitabakia kuwa meli iliyotia nanga bahari kuu.

  Azimio la Zanzibar kama alivyosema Mama hapo juu linaudhi kwa sababu ni Azimio hili lililokuja kuondoa Maadili ya viongozi bila kuweka masharti magumu ktk kulinda maslahi ya taifa..masharti ambayo yanaweza kuleta Conflict of interest na sasa hvi tumesimama mahala pabaya zaidi kwani wahujumu wa Uchumi ni viongozi wenyewe watunga sheria. Wenye mamlaka ya Utawala watu ambao tumewaamini kushika madaraka ktk sehemu muhimu za Uchumi wetu...The Untouchbles!

  Tuwe wakweli ndugu zangu tusifanye chuki na hasira kufikiria kwamba Mwalimu ndiye chanzo cha kila mabaya kwani hata Mungu alioyetuumba unaweza kabisa kufikira kwamba ndiye chanzo cha madhambi yote..Kwa nini alituumba na Tamaa!..
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Dec 27, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,765
  Likes Received: 4,980
  Trophy Points: 280
  Mkandara,

  ..mashirika hayo yaligeuka misheni town kwasababu kulikuwa na uhaba wa bidhaa.

  ..mfano: leo hii Tanzania Breweries siyo kijiwe cha walanguzi kwasababu wanazalisha kwa kiwango cha juu. hakuna m-Tanzania aliyeko tayari kununua bia ya magendo.

  ..na kuonyesha kwamba kauli zako ni za kupotosha hivi unafikiri leo hii wananchi wakianza kupelekea bei Zambia,Congo,Rwanda,na Burundi, Tanzania Breweries watalalamika au ndiyo watazidi kufurahia kwa kuongezeka kwa soko lao?

  ..kama viwanda vya enzi zile vilikuwa imara basi vingeongeza uzalishaji. soko la ndani lilikuwepo, na umesema bidhaa zao zilikuwa na soko[magendo] mpaka nchi jirani.

  ..hapa siyo siasa, dini, it is simple economic theories. ukiwa na uhaba wa bidhaa na juu yake ukawa unapanga bei[price control] basi matokeo yake na ulanguzi. that is exactly what happened during those days.

  ..kama tatizo lilikuwa ni ulanguzi na magendo, basi operesheni ile ingeleta unafuu. badala yake wananchi tuliendelea kutaabika.
   
 13. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mkandara,

  Kwanini unalinganisha mapera na mikwaju? Azimio la Zanzibar halitakiwi kuwepo kwenye mjadala huu au ufisadi.

  Vita hivi vilitokea 1983-1984 pale Sokoine alipochukua nafasi ya uwaziri mkuu kwa mara ya pili.

  Lakini matatizo ya uhujumu yalitokea baada ya kumaliza kwa vita vya Kagera. Baada ya vita vya kagera vitu vilipotea madukani na Mwalimu JKN akasema tufunge mikanda kwa miezi 18. Na baada ya mwaka mmoja akaligeuka jiwe na kusema miaka 18.

  Nasikia humu yupo Mzee Mtei labda angetueleza kwanini alitimuliwa uwaziri wa fedha. Maana baada ya kutimuliwa kwake kila kitu kilichoweza kwenda kombo kilikwenda kombo.
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Dec 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  JokaKuu,

  Mkuu nazungumza yote haya kutokana na experience sio habari ya kusimuliwa.

  Kifupi najua wengi wenu miaka hiyo mlikuwa shule iwe Chuo kikuu ama sekondari lakini mimi nilikuwa tayari mitaani nikibangaiza.

  Nakwambia hapakuwa na Ubaha wakitu chochote ktk uzalishaji isipokuwa vitu vyote hivi vilizalishwa kwa minajiri ya biashara ya ndani kutosheleza mahitaji yetu..Unapozungumzia swala la Bia nakumbuka vizuri Breweries walikuwa na matawi hadi vijijini na kuna jamaa mmoja Mganda akiitwa Peter alikuwa mlanguzi mkubwa wa bia hizi kuzipeleka Uganda.

  Miaka hiyo usafiri wa meli za abiria na mizigo ulikuwa ulikuwa ukienda Uganda na Kenya kila week mara tatu na mizigo minmgi ilikuwa bidhaa zetu wenyewe. Huku kusini Mbeya pia vijana walichemka kupitisha mali kwenda Zambia na ni wakati huo nimekaa sana Mbeya mjini na kuja fahamiana na vijana wa Mbeya ambao nilikuja kuwa mwenyeji wao mjini wakikaa pale Hotel Continental..Najua watashangaa sana kusikia mimi ndio Mkandara yule mhuni wa Holiday.

  Hivi wewe unafikiria wale machinga wa Kichagga wenye mabanda ya michubuo na madawa ya nywele waliweza vipi kuyaingiza nchini wakati mgumu kama ule...Mkuu, Uhaba ulitokea kwa sababu mali nyingi zilisafirishwa nje, fedha ya kigeni kwetu ilikuwa shilingi ya Kenya..Dollar ilikuwa haipatikani benki kuu hivyo kuuza mali zetu nje ndio njia pekee ya watu kukusanya dollar bila kupitia benki kuu na wahindi ambao walikuwa wateja wakubwa wa dollar..Nitarudia kusema ni maisha ambayo nimeyapitia na nafahamu kwa upana zaidi ya haya nayoandika hapa..

  Sema tu ktk operation hiyo walidhurika wengi.. Askari wetu badala ya ku target sehemu zinazotakiwa walianza kufanya wao biashara ya mshiko. Ukikutwa na kifuko tu unasimamishwa na kuulizwa umebeba nini.. Ikiwa mali wanachukua na utarushwa kichura kwa chupi moja ya toka mtoni. Ikafikia kwamba tulikuwa tumepoteza maana ya vita ile na kuwa kila mwanancvhi ni mkisiwa wa Uhujumu.

  Kuna marafiki zangu wakija Mbowe na kutanua enzi hizo kutokana na uuzaji wa sigara, Khanga za Urafiki, zana za Ufi, Besco, Gafco, Bima na kadhalika wote walikuwa wakitanua kwa uuzaji wa mali na ma deal ya serikali kwa walanguzi chini ya meza na sio kwa minajiri ya kuwafikia wananchi bali kusafirisha nje kiasi kwamba ilikuwa vigumu kumshika mtu na mali hizo.

  Ziwa victoria lilikuwa uwanja wa mapambano na ni katika wakati huo jeshi letu liliweka meli za kivita kufukuzia makalua yaliyojaa mali..Mkuu vijana wote miaka hiyo tumeishi kwa kubangaiza, Ukame ulikuwepo lakini hata siku moja sikuwahi kupanga jiwe dukani kwa mhindi tulijua wapi mali inapatikana. Tulijimwaga Mermaid na Salamander kila siku kama vile hakuna shida na jambo moja muhimu sana la kujiuliza wewe ni hili..

  Kwa nini pamoja na Ukame wote ule kuna bar zilikuwa hazikosi Pombe..Hata siku moja tulipokuwa disco sio Mbowe, Africana, New Afrika, Vision, Silversand, Rungwe na sehemu kibao hatukuwahi kuona ukosefu wa bia hizo! wala kusikia kwamba Breweries walishindwa ku supply. Kuna hotels ambazo kila siku zilikuwa na chakula kama kawaida tena kwa bei nafuu ajabu. Lini ulikwenda Azam ukakosa Pilau na Biriani! Au Mermeid ukakosa Chips..

  Nakumbuka wakati mmoja nikienda Uganda kwa hayo makalua ilibidi tutupe magunia ya sukari kupunguza uzito kwani kalua lilikuwa likiingiza maji...Na kibaya zaidi basi walanguzi wote waliokuwa wakichukua mali hizo adimu walirudi nchini na Mitumba, vipodozi na mashati ya Juliana toka toka Dubai..
  Kwa hiyo tatizo la nguo, vipodozi, sabuni, dawa za miswaki nchini ilikuja sababisha uhaba wa vitu muhimu sana kama chakula..kwa ubadilishaji wa mali kwa njia haramu na wakati huo huo supply kutoweza kutosheleza demand.

  Kila Nyerere alijaribu kuweka ngumu ktk kuhakikisha bei nafuu kwa wananchi ndio kwanza wafanya biashara walificha mali hizo. Demand iko palepale na supply ikaonekana hakuna.. Nakumbuka maduka mengi waliweza kuuza asilimia 20 ya stock yao na kudai kwamba mali imekwisha.. usiku wanakuja walanguzi na kupewa mali iliyobakia kwa bei ya juu zaidi ya ile ya serikali, hivyo price control pia iilichangia sana..Mkuu yote haya nazungumza kiuchumi na economics inakubali kabisa sababu nilizoziweka hapa.. It's the fact sio najaribu kutumia kitabu kama wasomi wengi wanavyotaka watu kuamini kuwa uchumi wetu ulianguka kutokana na Ujamaa peke yake.

  Kweli kabisa Ujamaa ulichangia sehemu kubwa kwani mashirika yote yaliyokuwa yakizalisha mali nchini yalikuwa hayawezi kujiendesha zaidi ya kutegemea bajeti ya serikali. Kama yangepata mfumo fulani wa biashara biashara na somehow kama China ya leo, yakawa private with some regulation and govt control in policies za responsibility kwa viongozi wake, yakaweza kujiendasha yenyewe labda pengine tungeweza kutokana na tatizo la Uhaba wa vitu.

  Kama nilivyosema hapo awali mwalimu Nyerere alishindwa kuziba tobo za Uhujumu uchumi ktk Ujamaa kwa sababu hakufahamu shina la Uhujumu uchumi lilitokana na watu aliowaweka madarakani kuendesha mashirka hayo.. Muulize hata FMES atakwambia viongozi wetu wa leo ktk serikali ndio wale wale waliokuwa viongozi ktk mashirika ya Umma na ndio wao waliotufikisha hapa tulipo. Ndio mafisadi wakubwa wa Ujamaa wenyewe walioiba na kufilisi mashirika hayo..Mtindo wa kuziba tobo haukulenga wahujumu isipokuwa mabangusilo na samaki wadogo. ukweli ni kwamba mashirika ya Umma yalikufa kutokana na viongozi wake ambao kwa wakati ule ndio walikuwa matajiri wetu.

  Kitu kimoja tu ambacho namsifia mwalimu ni kwamba hata baada ya kushindwa kwake na Ujamaa lakini siku zote hakuisha kutukumbusha na kusisitiza kwamba Corruption ndio UFA mkubwa wa maendeleo yetu na tusipoweza kuziba Ufa huo basi tutakuja jenga nyumba nzima. Mwinyi hakuweza kuziba ufa zaidi ya kuweka fanicha mpya ambazo hazikuwa na faida kwetu ila mapambo ya nyumba.

  Mkapa hakuweza kuziba Ufa zaidi ya kutuletea wezi wengine ndani ya nyumba yetu...Ufa umepanuka zaidi na nyumba inaanza kuingiza maji ya mvua ambayo kimazingira yetu mvua ni neema...Hiyo hiyo mvua itakuja kuwa Tsunami na hatutaweza kuokolewa kirahisi.

  Uhujumu uchumi unatakiwa kupigwa vita kwa nguvu zote pamoja na kwamba ni crime ambayo haiwezi kwisha. Tukumbuke tu kwamba hujuma za uchumi nchini leo hii tunakula hata mbegu za uchumi wenyewe. Mbegu zikija kwisha nadhani tanzania itakuwa sehemu mbaya zaidi kuliko wakati wa Mwalimu.
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Dec 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Zakumi,
  Mkuu labda hukusoma hoja Ya Rev. Kishoka vizuri. Nimeweka Azimio la Zanzibar kumjibu rev na pia kuunga mkono hoja ilizotangulia...
  Rev. Kishoka kafungua mada kwa kusema hivi:-

  "Mikingamo... Sasa vita vimetangazwa jama, wananchi wote tuwe imara, vijijini na mijini tusisite kuwafichua wahujumu na walanguzi"
  Nini kulikuwa chimbuko la kuanzishwa kwa vita dhidi ya wahujumu uchumi, walanguzi na wafanya magendo?

  Sheria ya Uhujumu Taifa ya mwaka 1984 bado iko hai, kwa nini haitumiki?
   
 16. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #16
  Dec 27, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Jokakuu:

  Unakazi hapa. Hapa ni lazima directly au indirectly umtaja Nyerere na Mkandara atakuja Full Speed.

  Lakini ukweli wa mambo unabakia palepale. Ulanguzi ulisababishwa na uhaba wa vitu na hii ni principal ya Supply and Demand tu.

  Vilevile sio kazi ya serikali ku-produce na kumachinga vitu.
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Dec 27, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Chimbuko la vita ya uhujumu uchumi ilikuwa ni mambo mawili:
  (a) imbalance kati ya supply na demand ya commodities mbalimbali kwenye jamii;
  (b) Wrong imagination ya serikali kuwa supply ya commodities iliyokuwepo ilikuwa inaweza kukidhi demand ya wakati huo kwenye jamii.

  Magendo, bei za kuruka na vitendo vya aina hiyo vyote ni matokeo ya imbalance kati ya supply na demand
   
 18. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #18
  Dec 27, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180

  Mahakama za Uhujumu taifa zilikuwa Kangaroo courts. Ndio maana kuzitumia sheria zake inakuwa creepy.
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Dec 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kichuguu,

  Ulanguzi haukuwa ndani nchini hivyo siwezi kuhusisha na demand na supply kwa kupima mahitaji ya wananchi kushindikana kwa sababu supply haikuweza kutosheleza. Ulanguzi ulikuwa nchi za jirani ambazo walikuwa na Uhaba wa vitu hivyo na waliweza kutoa bei ya juu mara mbili ama tatu zaidi yetu.

  Kisheria haikuruhusiwa kupeleka mali hizo nje lakini watu walivumbua njia haramu. Price control ya mwalimu pia ilikuwa sababu kubwa ya kuongeza tamaa ya kuuza vitu hivyo nje. Kumbuka mwalimu aliweka bei za vitu vyetu chini ili kila mwananchi aweze ku afford..Mkuu nauli ya UDA ilikuwa shilingi, umeona wapi biashara hiyo duniani!

  Hivyo badala ya supply kukidhi mahitaji yetu ilikwenda nje kwenye bei nzuri zaidi na kusababisha Uhaba hapa ndani nchini..wewe huwezi kuelewa hili kama mwanachi mnunuzi upande (consumer) wa pili isipokuwa watu kama sisi (middlemen) tuliweza kuona kwa ndani jinsi game lilivyokuwa likichezwa ndio nawambia hivyo!
   
 20. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #20
  Dec 27, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Mkandara,

  Mimi niliwahi kufanya magendo ya kuuza ngozi za ngombe Kenya kupitia Sirari. Sababu ilikuwa siyo kuwa Tanzania tulikuwa na ngozi nyingi, na kuwa kulikuwa na demand kubwa ya ngozi hizo huko Kenya, la hasha. Sababu kubwa iliyokuwa inatufanya kupeleka ngozi zile, na huenda hata kuziuza kwa bei nafuu ni kwa sababu zilikuwa zinatuwezesha kupata Shilingi za Moi na kuzitumia hizo kununua Colgate, Palmolive, Imperial Leather, vitambaa vya Crimpline na vitu kama hivyo ambavyo vilikuwa hadimu kwetu.
   
Loading...