Nini chimbuko la Vita vya Uhujumu Uchumi - 1983-84?

Zakumi,

..MKANDARA alikuwa MLANGUZI ndiyo maana hatuelewani. tena ame-confess kwamba hakuwahi kupanga mawe kwa ajili ya foleni. inawezekana hata habari ya maduka ya kaya ni ya kusimuliwa Jamii Forums.

Mkandara,

..wa-Tanzania walikuwa wanavusha magendo ya mafuta ya kupikia na sabuni[rexona,life bouy] toka Kenya. sasa uliwahi kusikia Nairobi kuna Wakenya wamepanga foleni ya mafuta ya kupikia, au sabuni ya kuogea?

Kichuguu,

..damn!! umenikumbusha vitambaa vya crimpline. yaani sina mbavu hapa.

..lakini pia lazima tukubali kwamba kulikuwa na uendeshaji mbaya wa viwanda na mashirika yetu. kuna kampuni kama TBL na UFI hazikutakiwa ziwe na matatizo hata kidogo.
 
Kichuguu,
Mkuu unataka kunambia tulitengeneza ngozi za ng'ombe pasipo kuwepo demand?.. na iweje Kenya wazinunue bila kuwepo demand hapa unatumia mfumo hgani wa uchumi. Kama Kenya wangekuwa wanazo za kuwatosheleza wasingenunua hata kidogo unless quality ya ngozi yetu ilikuwa juu zaidi..
Na wewe umekwenda Kenya kununua hizo Colgate na sabuni kwa sababu kulikuwa na demand nchini usitake kunambia hata Tanzania hatukuwa na Uhaba huo..hii ndiyo principal ya biashara haiwezi kuwa tofauti hata kidogo.
Hii yako ni lugha ya kujihami mkuu, ukweli ni kwamba tumeuza ngozi za ngombe ambazo Bora walizihitaji kutengeneza viatu vyetu kwa kuchukua Colgate toka Kenya ikatulazimu sisi kuvaa viatu vya kimasai matairi na kanda mbili tukilaumu Bora wameshindwa kutosheleza mahitaji yetu.
 
Jokakuu,
Kenya hawakuweza kupanga mawe kwa sababu supply ilikuwa inatoka Tanzania.. Ni sawa na leo hii tuna maduka ambayo vitu vyote vinatoka nje hakuna hata kimoja kintengenezwa nchini na wananchi hawapangi mawe...Kupanga mawe haina maana wameshindwa kutengeneza..it's about demand na supply haijalishi vitu vinatoka wapi.
Kumbuka tu kwamba vitu tulivyokuwa tukitengeneza nchini vilikuwa marufuku kuingizwa nchini toka nje hivyo tulibakia ktk limbo.
 
Kichuguu,
Ulanguzi haukuwa ndani nchini hivyo siwezi kuhusisha na demand na supply kwa kupima mahitaji ya wananchi kushindikana kwa sababu supply haikuweza kutosheleza. Ulanguzi ulikuwa nchi za jirani ambazo walikuwa na Uhaba wa vitu hivyo na waliweza kutoa bei ya juu mara mbili ama tatu zaidi yetu. Kisheria haikuruhusiwa kupeleka mali hizo nje lakini watu walivumbua njia haramu. Price control ya mwalimu pia ilikuwa sababu kubwa ya kuongeza tamaa ya kuuza vitu hivyo nje. Kumbuka mwalimu aliweka bei za vitu vyetu chini ili kila mwananchi aweze ku afford..Mkuu nauli ya Uda ilikuwa shilingi umeona wapi biashara hiyo duniani!

Hivyo badala ya supply kukidhi mahitaji yetu ilikwenda nje kwenye bei nzuri zaidi na kusababisha Uhaba hapa ndani nchini..wewe huwezi kuelewa hili kama mwanachi mnunuzi upande (consumer) wa pili isipokuwa watu kama sisi (middlemen) tuliweza kuona kwa ndani jinsi game lilivyokuwa likichezwa ndio nawambia hivyo!

Mkandara:

Ni lazima uwe makini hapa. Kwenye posti yangu moja nimesema kuwa vita hivi vay uhujumu vilianza 1983-84. Lakini uhaba wa vitu ulianza mara baada ya kumalizika vita vya Uganda.

Hipo correlation kati ya vita vya Uganda na uhaba wa vitu. Edwin Mtei hakuachia ngazi hivihivi tu kama waziri wa fedha.

Hipo correlation kuvunjika kwa jumuia ya Afrika mashariki na uhaba wa vitu.

Sisi tulioishi mipakani tulikuwa tunatumia sabuni, sukari na vitu vingi kutoka nje na sio Tanzania. Hivyo tueleze ni nchi gani ambazo wafanya biashara wetu walikuwa wanapeleka bidhaa zilizokuwa zinahitaji Tanzania.
 
Mkandara,

Mimi niliwahi kufanya magendo ya kuuza ngozi za ngombe Kenya kupitia Sirari. Sababu ilikuwa siyo kuwa Tanzania tulikuwa na ngozi nyingi, na kuwa kulikuwa na demand kubwa ya ngozi hizo huko Kenya, la hasha. Sababu kubwa iliyokuwa inatufanya kupeleka ngozi zile, na huenda hata kuziuza kwa bei nafuu ni kwa sababu zilikuwa zinatuwezesha kupata Shilingi za Moi na kuzitumia hizo kununua Colgate, Palmolive, Imperial Leather, vitambaa vya Crimpline na vitu kama hivyo ambavyo vilikuwa hadimu kwetu.

That's correct. Watu walikuwa wanapeleka malighafi nje ya nchi na sio bidhaa zenyewe. Kahawa ilikuwa inauzwa nje ya nchi na sababu kubwa ni mamlaka za mazao kushindwa kuwalipa watu kwa wakati unaotakiwa na kwa bei nzuri.
 
Kichuguu,
Mkuu unataka kunambia tulitengeneza ngozi za ng'ombe pasipo kuwepo demand?.. na iweje Kenya wazinunue bila kuwepo demand zaidi. kama Kenywa wangekuwa na za kuwatosheleza wasingenunua hata kidogo..Na wewe umekwenda Kenya kunua hizo Colgfate na sabuni kwa sababu kulikuwa na demand nchiniusitake kunambia hata Tanzania hatukuwa na Uhaba huo..
Hii ni lugha ya kujihami mkuu ukweli ni kwamba tumeuza ngozi za ngombe ambazo Bora walizihitaji kutengeneza viatu kwa kuchukua Colgate ikatuklzimu sisi kuvaa viatu vya kimasai matairi na kanda mbili..

Kaka Mkandara unakosea,

Tanzania tulikuwa na uhaba wa commodities nyingi kwa ajili ya mlaji (consumer goods.) Hivyo tulikuwa tunatafuta chochote tulicho nacho tukipeleke huko ili tupate hela ya moi kutuwezesha kupata shilingi ya Moi kununulia hizo commodites na kuzileta kwetu. Vitu tulivyokuwa tunapeleka kule ni raw materials mbalimbali kama ngozi za ng'ombe na kadhalika. Kuna watu walipeleka hata pamba na kahawa.

Tuwe wakweli na kukubali historia yetu kuwa tulikuwa na tatizo kubwa kwenye consumer goods na hivyo kutumia mianya tuliyokuwa tunaweza kupata ili kuuza raw materials huko Kenya (pamoja na Zambia, Malawi, na Burundi) kusudi tupate hizo consumer goods tulizokikuwa na njaa nazo. Wao hawakuwa na njaa kali sana na hizo raw materials tuliokuwa tunawauzia, kwani walikuwa wanazinunua kwa bei nafuu sana.
 
Jokakuu,
Kenya hawakuweza kupanga mawe kwa sababu supply ilikuwa inatoka Tanzania.. Ni sawa na leo hii tuna maduka ambayo vitu vyote vinatoka nje hakuna hata kimoja kintengenezwa nchini na wananchi hawapangi mawe...Kupanga mawe haina maana wameshindwa kutengeneza..it's about demand na supply haijalishi vitu vinatoka wapi.
Kumbuka tu kwamba vitu tulivyokuwa tukitengeneza nchini vilikuwa marufuku kuingizwa nchini toka nje hivyo tulibakia ktk limbo.

Mkandara:

Sasa wewe umechanjia kwa ubishi. Kabla ya kuvunjika kwa jumuia ya Afrika mashariki 1977, bidhaa nyingi zilikuwa zinatoka Kenya. Sasa itakuwaje iwe vice versa katika kipindi kifupi tu Tanzania iwe inapeleka vitu Kenya.

Nchi ambayo Tanzania ili-supply vitu ni Uganda. Baada ya vita Uganda ilikuwa kwenye messy. Na waganda walianza kuwachukia watawala wa Kitanzania kwa kusababisha uadimu wa vitu. Hivyo bidhaa muhimu zilikuwa zinapelekwa Uganda badala ya kutumiwa na watanzania.

Na waganda walivyo corrupt wakawa wanaziuza Sudan ya Kusini.
 
Kichuguu,
Mkuu unataka kunambia tulitengeneza ngozi za ng'ombe pasipo kuwepo demand?.. na iweje Kenya wazinunue bila kuwepo demand hapa unatumia mfumo hgani wa uchumi. Kama Kenya wangekuwa wanazo za kuwatosheleza wasingenunua hata kidogo unless quality ya ngozi yetu ilikuwa juu zaidi..
Na wewe umekwenda Kenya kununua hizo Colgate na sabuni kwa sababu kulikuwa na demand nchini usitake kunambia hata Tanzania hatukuwa na Uhaba huo..hii ndiyo principal ya biashara haiwezi kuwa tofauti hata kidogo.
Hii yako ni lugha ya kujihami mkuu, ukweli ni kwamba tumeuza ngozi za ngombe ambazo Bora walizihitaji kutengeneza viatu vyetu kwa kuchukua Colgate toka Kenya ikatulazimu sisi kuvaa viatu vya kimasai matairi na kanda mbili tukilaumu Bora wameshindwa kutosheleza mahitaji yetu.

Sasa zilie kany@boya zilikuwa zinatoka wapi kazi sio uhaba wa vitu. Mtu anauziwa Palmolive na akifungua ndani anakuta kipande cha mhogo.
 
Zakumi,

..kuna mahali nilisoma kwamba Mtei alimuwahi Mwalimu na barua ya kujiuzulu kabla hajafukuzwa kazi.

..inasemekana Mtei alikuwa anakubaliana na mapendekezo ya IMF ambayo Mwalimu alikuwa akiyapinga.

..baadaye Mtei aliajiriwa na IMF ktk nafasi ambayo nadhani inahitaji baraka za serikali ya Tanzania.

NB:

..nadhani viwanda vyetu vilikuwa under-capitalised. inawezekana matumizi yetu ktk vita vya kagera yalisababisha hali hiyo.

..pia ulaji na ufujaji vinaweza kuwa vimechangia kuangusha viwanda vyetu.

..it doesnt make sense kiwanda au shirika liwe na monopoly halafu lishindwe kujiendesha.

..SAMAHANI KUTOKA NJE YA MADA. TURUDI KWENYE VITA DHIDI YA WAHUJUMU.
 
Jokakuu,
Kenya hawakuweza kupanga mawe kwa sababu supply ilikuwa inatoka Tanzania.. Ni sawa na leo hii tuna maduka ambayo vitu vyote vinatoka nje hakuna hata kimoja kintengenezwa nchini na wananchi hawapangi mawe...Kupanga mawe haina maana wameshindwa kutengeneza..it's about demand na supply haijalishi vitu vinatoka wapi.
Kumbuka tu kwamba vitu tulivyokuwa tukitengeneza nchini vilikuwa marufuku kuingizwa nchini toka nje hivyo tulibakia ktk limbo.

Hapana, Kenya walikuwa wanaweza kupata vitu hivyo mdukani mwao kwa hiyo hawakuwa na haja ya kupiga foleni. Nakumbuka kuwa vitu ambavyo Tanzania hatukubabikia sana kutoka Kenya ni pamoja Blue Band Margarine kwa sababu tulikuwa na supply kubwa sana Tan-Bond Margarine kutoka pale Voil Mwanza, na bia za Tusker & Snow Caps kwa sababu tulikuwa na supply kubwa sana ya Safari kutoka Ilala.

Tanzania ilifikia kuwa muuazji wa duka la ushirika akawa anatetemekewa na kila mtu. Vijana waliokuwa wanafanya RTC wakawa kama miungu watu.

Wacha kaka tumetoka mbali sana kiuchumi.
 
zakumi,
hapana mkuu sipotoshi kitu. nadhani tunachozungumzia hapa ni operation ya Uhujumu uchumi na sio mwanzo wa biashara za magendo. Biashara hizo zimenza muda mrefu kabla ya vita yenyewe ilipoanza sawa na Kikwete leo kushughulikia mafisadi haina maana Ufisadi umenza kipindi hiki..
Mimi nimetoa historia kamili toka hoja ya rev hadi ya sababu za Uhaba kulingana na madai ya Jokakuu. ndio maana napoandika huwa najaribu ku cover sehemu kubwa ya hoja zilizotangulia.

Kisha umesema kwamba vitu vilivyokuwa vikisafirishwa kenya vilikuwa mali ghafi, mkuu sio kweli hata kidogo kwani wakulima wenyewe ndio walikuwa na taabu kubwa.. Huwezi kusafirisha ngozi ambayo haijawa processed na hata kahawa yetu labda huko Moshi lakini sijawahi kusafirisha kahawa Kenya ama Uganda kwa sababu hawa jamaa zetu walikuwa na kahawa bora kuliko sisi. yawezekana ulifanya biashara hivyo na ndio maana walitaka mali ghafi wakijua Tanzania tuna process vibaya ama sio ktk standard wanayoitaka. lakini sukari, sigara, matairi na vinginevyo mkuu wangu tanzania tuliweza kutengeneza vitu ktk hali ya juu sana na nimefanya biashara hiyo.. Washikaji wangu wametengeneza kichizi kwa mali hizo.
Nitarudia kusema hii sio habari ya kusimuliwa nimeifanya kama middleman na mitikasi yote iliyotembea wakati ule nimejaribu ama nimekuwa na watu waliokuwa wakiiendesha.
Kama ningekuwa askari kanzu wakati huo ningeweza kabisa kuangusha the mafia mob ya wale wote waliohusika ngazi za juu..
katika yote haya ninataka tu kuwataarifu kwamba viongozi waliokuwa wametumaliza enzi za mashirika ya Umma ndio leo mawaziri wetu kwa hiyo kila linalotokea leo sio jipya isipokuwa ni jipu ambalo tumeshindwa kulipasua kwa muda mrefu..
 
Zakumi,

..MKANDARA alikuwa MLANGUZI ndiyo maana hatuelewani. tena ame-confess kwamba hakuwahi kupanga mawe kwa ajili ya foleni. inawezekana hata habari ya maduka ya kaya ni ya kusimuliwa Jamii Forums.

Mkandara,

..wa-Tanzania walikuwa wanavusha magendo ya mafuta ya kupikia na sabuni[rexona,life bouy] toka Kenya. sasa uliwahi kusikia Nairobi kuna Wakenya wamepanga foleni ya mafuta ya kupikia, au sabuni ya kuogea?

Kichuguu,

..damn!! umenikumbusha vitambaa vya crimpline. yaani sina mbavu hapa.

..lakini pia lazima tukubali kwamba kulikuwa na uendeshaji mbaya wa viwanda na mashirika yetu. kuna kampuni kama TBL na UFI hazikutakiwa ziwe na matatizo hata kidogo.

Hatuwezi kuelewana na Mkandara. Kufa kwa TBL na UFI kulisababishwa na mambo mengi.

Moja wapo haya yakiwa ni mashirika ya umma hayakuruhusiwa kuchukua advantage ya uhaba wa soko la ndani.

vilevile we lack cutting edge innovations katika masuala ya management na kiufundi. Mitambo hiyo hiyo akipewa mgeni anaweza kuendesha.

Mada ni ulanguzi. Tusipoichunga mada Mkandara atatua nje.
 
Kichuguu,
Mkuu unarudia niliyaandika.. watu wa RTC walikuwa wakitetemekewa kwa sababu mali ilikuwepo isipokuwa ilitoka kwa kujuana. Na mara zote asilimia kubwa ilichukuliwa na walanguzi ambao waliweza kuipeleka nje kuuza kwa bei kubwa.. Uwezo wa Mtanzania ulikuwa mdogo na kwa mazoea ya Ujamaa ilikuwa haramu kushindana bei ndani ya nchi kwanza utakamatwa..
Kumbuka tu vita ya Uhujumu uchumi ilipotangazwa unakumbuka watu walivyokwenda kufukia mali wengine kutupa baharini.. sasa kama supply haikuwepo waliweza vipi kukamatwa na wengine kutupa mali hizo.. walizipata wapi?.
 
Ninachofurahia ni kuwa Mkandara ana uzalendo wa hali ya juu sana kiasi kuwa hapendi kujikumbusha uchafu uliolikabiri taifa letu kutokana na historia halisi ya uchumi wetu.
 
Zakumi,
Mbona mimi nawaelewa nyie.. Na najibu maswali yenu kutokana na jinsi mnavyouliza..somo hapa ni Uhujumu uchumi.. Mkuu majembe ya UFI yameendelea kutumika hadi kipindi cha Mwinyi katikati sema tatizo la kiuchumi nchini ni kuendekeza kilimo asilia cha majembe ya mkono...
TBL haikufa hata kidogo isipokuwa ni tamaa ya serikali kuuza mradi huo ili kupata asilimia 10 na hisa kwani ni watawala hao hao kisheria tumewapa uwezo wa kufanya biashara...
 
Kichuguu,
Mkuu nashukuru umenielewa kwa sababu naelewa nini na wapi tulikosea hasa nikijua madhambi tuliyoyafanya. I was among them na inauma kuona kwamba tunarudia makosa yale yale ya kutazama mchawi nje ya sisi wenyewe...
nani hapa JF anaweza ku confess makosa yake ktk mtandao wazi kama huu!.. sii jambo dogo lakini huo ndio ukweli sipendi lakini kwa manufaa ya Umma na taifa zima ni muhimu kwangu kuelezea experience yangu na uhuni niliopitia.
 
zakumi,
hapana mkuu sipotoshi kitu. nadhani tunachozungumzia hapa ni operation ya Uhujumu uchumi na sio mwanzo wa biashara za magendo. Biashara hizo zimenza muda mrefu kabla ya vita yenyewe si sawa na Kikwete leo kushughulikia mafisadi haina maana Ufisadi umenza kipindi hiki..
Mimi nimetoa historia kamili toka hoja ya rev hadi ya sababu za Uhaba kulingana na madai ya Jokakuu. ndio maana napoandika huwa najaribu ku cover sehemu kubwa ya hoja zilizotangulia.

Kisha umesema kwamba vitu vilivyokuwa vikisafirishwa kenya vilikuwa mali ghafi, mkuu sio kweli hata kidogo kwani wakulima wenyewe ndio walikuwa na taabu kubwa.. Huwezi kusafirisha ngozi ambayo haijawa processed na hata kahawa yetu labda huko Moshi lakini sijawahi kusafirisha kahawa Kenya ama Uganda kwa sababu hawa jamaa zetu walikuwa na kahawa bora kuliko sisi. yawezekana ulifanya biashara hivyo na ndio maana walitaka mali ghafi wakijua Tanzania tuna process vibaya ama sio ktk standard wanayoitaka. lakini sukari, sigara, matairi na vinginevyo mkuu wangu tanzania tuliweza kutengeneza vitu ktk hali ya juu sana na nimefanya biashara hiyo.. Washikaji wangu wametengeneza kichizi kwa mali hizo.
Nitarudia kusema hii sio habari ya kusimuliwa nimeifanya kama middleman na mitikasi yote iliyotembea wakati ule nimejaribu ama nimekuwa na watu waliokuwa wakiiendesha.
Kama ningekuwa askari kanzu wakati huo ningeweza kabisa kuangusha the mafia mob ya wale wote waliohusika ngazi za juu..
katika yote haya ninataka tu kuwataarifu kwamba viongozi waliokuwa wametumaliza enzi za mashirika ya Umma ndio leo mawaziri wetu kwa hiyo kila linalotokea leo sio jipya isipokuwa ni jipu ambalo tumeshindwa kulipasua kwa muda mrefu..

Mkandara:

Kama Mbeya inalima mahindi mengi na wakati huo huo nchi nzima ina wingi wa chakula basi serikali haiwezi kuwazuia wananchi wa Mbeya kuuza mazao yao Malawi au Zambia. Kuuza kwao nje ya nchi hakuna athari yoyote hile na vilevile kutainua uchumi wa wananchi Mbeya.

Wananchi wa Mbeya wanapokatazwa kuuza chakula Malawi na Zambia ni kwa sababu ndani ya nchi kuna uhaba wa chakula.

Kwa mtaji huu bidhaa zilizotengenezwa Tanzania na kuuzwa nje bado zilikuwa azitoshelezi mahitaji ya ndani hiyo ni fact mkuu.

Suala la kuwa bidhaa zetu zilikuwa bora ndio maana tulikuwa na uhaba wa bidhaa doesn't make sense to me. Tunachozungumza hapa ni quantity.

Viwanda vya Tanzania tunavijua na matatizo yaliovikabili viwanda hivyo yanajulikana.
 
Hapana, Kenya walikuwa wanaweza kupata vitu hivyo mdukani mwao kwa hiyo hawakuwa na haja ya kupiga foleni. Nakumbuka kuwa vitu ambavyo Tanzania hatukubabikia sana kutoka Kenya ni pamoja Blue Band Margarine kwa sababu tulikuwa na supply kubwa sana Tan-Bond Margarine kutoka pale Voil Mwanza, na bia za Tusker & Snow Caps kwa sababu tulikuwa na supply kubwa sana ya Safari kutoka Ilala.

Tanzania ilifikia kuwa muuazji wa duka la ushirika akawa anatetemekewa na kila mtu. Vijana waliokuwa wanafanya RTC wakawa kama miungu watu.

Wacha kaka tumetoka mbali sana kiuchumi.

Nakumbuka nikiwa Mwanafunzi tulitembelea Kenya. Na kwa miaka mingi tulikuwa hatujala maandazi. Basi hotelini wache tuagize maandazi.

Wakati mKenya akienda hotelini anataka kikombe kimoja na maandazi mawili. Sisi tulikuwa tunaondoka na matano matano.

Jamaa yangu kutoka Zimbabwe alicheka sana nilimpompa stori hiyo. Naye akasema kuwa WaZambia walikuwa wanajulikana wakiingia Zimbabwe. Mzambia akiingia bar alikuwa anaagiza bia kumi kwa mara moja akifikiri kuwa bia Zimbabwe ni za mgao.
 
zakumi,
Mkuu bado nitakataa hoja yako kwa sababu nimefanya biashara hiyo... Tanzania tulikuwa tukisafirisha mazao zambia kwa kificho sana na haikuruhusiwa hata kidogo. Tulikuwa na njia za maporini pale Tunduma wakija mabebaji kuchukua mali usiku wa manane. Wenye mali walipita border kama kawaida huku mali imeshapakiwa ktk mabus tayari kwenda Lusaka..
Mimi hapa nimewahi kupeleka Zambia hiriki toka Tukuyu ambako ndio tulikokuwa tukizifuata kwa wakulima. Kwa mara ya kwanza nimekula Ugali na Maparachich ktk kusaka hirikii..
Hata siku moja hatukuwa na shida ya hiriki lakini ilikuwa hairuhusiwi kusafirisha unless una kibali ambacho process yake tu unaweza kukata tamaa..
Pia Ujamaa ulitulemaza tukashindwa kuelewa biashara kwa mapana ya soko na na bei kupanda. Price control ilikuwa moja ya sababu kubwa sana ya walanguzi kutafuta soko nje. haiwezekani wala haiwezi kuingia akilini unaposema vitu hivi kuuzwa nje wakati kuna uhaba na soko lipo Tanzania. Kama kulikuwa na Uhaba inawezekana vipi tukasafirisha mali ambayo kwa uhaba wake ingekuwa na soko nchini?..Umejaribu kufikiria hilo. Then itakuwaje tuseme viwanda vilishindwa kuzalisha ikiwa tuliweza kupata mali za kusafirisha nje!
Yaani mtu asafirishe mazao yake kwenda Zambia wakati kuna soko (uhaba) nchini!..haiwezekani isipokuwa kwa sababu nje ya somo hilo na nimesema kwamba price control nchini na bei kubwa zilizotolewa nje ziliwafanya walanguzi kutojali mahitaji ya ndani..
Na nashndwa kuelewa mnaposema uhaba hapa nchini kamam kweli ilikuwa vile kwa nini mlipeleka mahindi Zambia msirudi na mchele ama ngano badala yake ilikuwa nguo na sabuni za kuogea..!
 
Zakumi,
Mbona mimi nawaelewa nyie.. Na najibu maswali yenu kutokana na jinsi mnavyouliza..somo hapa ni Uhujumu uchumi.. Mkuu majembe ya UFI yameendelea kutumika hadi kipindi cha Mwinyi katikati sema tatizo la kiuchumi nchini ni kuendekeza kilimo asilia cha majembe ya mkono...
TBL haikufa hata kidogo isipokuwa ni tamaa ya serikali kuuza mradi huo ili kupata asilimia 10 na hisa kwani ni watawala hao hao kisheria tumewapa uwezo wa kufanya biashara...

Mkandara:

Una hisia tu kuwa unatuelewa lakini somo halipandi
icon10.gif
. Unachozungumza wewe ni exprience yako kama mlanguzi na una-generalize kama ndio lilikuwa tatizo nzima na kusahau principal za uchumi.

Kuna bidhaa za Tanzania zilizokuwa zinazouzwa nje. Lakini volume ya bidhaa hizo ilikuwa ni ndogo kuliko mahitaji ya bidhaa za mtanzania.

Kwa mfano kiwanda cha sigara kiliendelea kuwa msambazaji mkubwa wa sigara ata baada ya nchi kufungua mipaka. Na ata sasa mitambo ikisimama upungufu wa bidhaa utatokeo.

Bidhaa kama chumvi inapokosekana ujue hapo suala ni kubwa na uchambuzi wake ni wa kina.

Chumvi, mafuta ya taa, viwembe, nguo, yaani mpaka nguo za ndani watu wakaanza kujishonea.
 
Back
Top Bottom