Ningependa Tundu Lissu apokelewe hivi

Ningependa Tundu Lissu apokelewe hivi

Ingekuwa na faida zaidi angerudi kipindi kile kuwatumikia wananchi wake walipokuwa wanamuhitaji ilihali sasa anarudi kama mzigo!
Nenda kaonge maneno hayo mbele ya umati!uone hcho kipara kitaota nywele

Ova
 
Hizi no taarifa ambazo ni chungu sana kwa Jiwe na naamini pia pale Ikulu, usingizi hapati

Kwa kuwa yeye kama binadamu, alipania Tundu Lissu afe..........

Lakini kwa neema kuu ya Mungu, akamnusuru kwa njia ya muujiza mkubwa
Mungu si mwanadamu mkuu!!
 
Tunashukuru ndugu yetu na Mtanzania mwenzetu anarudi, tunaomba aje na nia ya ujenzi wa nchi, uzalendo, kupigania haki na kuhakikisha ykweli unapatikana kuhusu dhulma aliofanyiwa, na tuombe asije na uchochezi wa kuwatenganisha watanzania.

Japokuwa tuko nae chama tofauti, nitaunga mkono juhudi za kesi yake kupata haki na kujulikana waliompiga risasi na wachukuliwe hatua stahiki.
 
Mimi ni mwanaccm nitakuwa mstari wa mbele kumpokea na nitavaa tisheti yangu ya chama changu bila kujificha .
Kwani Lissu anapigania haki ya kikatiba bila kuangalia Itikadi ndo maana TLS walimwamini kwa ubinadamu aliowahi kuuonyesha ktk ile mgodi wa Noth Mara
 
Figisu litakalotokea litakua sio la nchi hii kama vile mugabe na morgan tsavangirai au kizza besigye
 
Atapokelewa na wanamtandao huku mtandaoni... nani apoteze muda wake kwenda kumpokea msaliti wa nchi.

Tupo wengi ile mbaya, na tuna uwezo wa kujua nani ni msaliti na nani ni mtetezi wetu. Wakati Lissu anapambana kuhusu raslimali za nchi na mikataba mibovu, wazalendo academia walikuwa kimya wanalinda vyeo.
 
Kwa mtazamo wangu sidhani kama ni busara sana kwa Lisu kurudi nchini kipindi hiki.Nafikiri ni si wakati sahihi sana kwake kurudi nchini.Ukizingatia aina za viongozi tulio nao wakati huu.Si wakati sahihi kwake kufanya harakati yoyote.
 
Back
Top Bottom