Mallia
JF-Expert Member
- Jan 31, 2018
- 437
- 1,532
Mabinti wengi huwa tunajisahau kuweka mambo sawa mapema pale tunapojukuta tupo mikononi mwa hawa wazee Matajiri maana wengi mda wowote kukuacha mjane ni kitu cha kawaida.
Ningekuwa Jaqy mapema sana ningemshauri mzee aniwekezee biashara zangu peke yangu au aniwekezee kiasi cha fedha kwa siri katika account yoyote ya benki bila ndugu yoyote kujua.
Pia, ningeachana kabisa na kufikiria biashara za mzee za zamani ambazo alianza kutafuta yeye na familia yake ningekaa nazo mbali kabisa maana mbele zingeleta mgogoro mkubwa, nisingemshauri mzee aandike wosia wowote ambao ungeleta ugomvi bali ningemshauri aniwekezee biashara zangu mapema na kiasi cha fedha benki hata asipokuwepo niendelee kusurvive na watoto.
Mzee angeondoka hapo ningekuwa na biashara zangu mwenyewe na fedha za kutosha benki, alafu sasa mali na biashara za mzee kama vituo vya habari na uwekezaji mwingine alioanza na familia yake kuutafuta ningekaa nazo mbali labda wenyewe wakubali kunipa kwa ajili ya watoto maana aibu ingewajia.
Lakini kinachomcost jaqy ni tamaa ya mali ambazo nyingine hakuzitafuta yeye Amezikuta tu na alichokosea zaidi ni kumshinikiza mzee aandae ule wosia ambao umekaa kikatili kitu ambacho kimezidi kuwakera ndugu wa marehemu hadi kufikia kwenda mahakamani, jaqy amedumu na mzee kwa miaka mitano tu lakini anataka arithi hadi vile mzee alivyoanza kutafuta na mkewe pamoja na wanawe miaka 50 iliyopita kitu ambacho hata wewe unayesoma hapa usingekubali.
Jaqy alitakiwa asome alama za nyakati mapema kwa kumshauri mzee amuwekezee biashara zake mapema, Angemshauri mzee amuwekee Fedha za watoto Benki za kutosha kimya kimya, hizi mali nyingine angewaachia ndugu tu waamue wenyewe, fikiria mzee angemuwekezea Billioni kadhaa Benki na biashara ambazo tayari alishamfungulia asingeteseka kamwe kama sasa anavyopambana na Ndugu.
Na usikute biashara alimuwekezea na fedha alimuwekezea lakini jaqy bado akawa na tamaa tu ya kutaka vyote, Tamaa ni mbaya sana jamani,Mabinti msikimbilie Utajiri wa haraka wa mali ambazo mmekuta zishatafutwa, mkipata wenza Wazee waambieni wawawekezee nyie kama nyie muaze na moja hizo mali nyingine ziacheni kwa familia waamue wenyewe wawape au wasiwape tayari mlishawekeza vya kwenu.
Hapo mtaishi kwa amani...
Sent using Jamii Forums mobile app