Ningejua nisingeoa maishani mwangu

Ningejua nisingeoa maishani mwangu

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
8,260
Reaction score
9,743
Habari za asubuhi wadau wa jukwaa hili.

Mwezi uliopita nilipata nafasi ya kukutana baba yangu ambaye mara ya mwisho tulikuwa tumeonana mwaka 2012.

Tukiwa mimi, yeye na dada yangu mkubwa tukipata lunch baba yangu alitoa kauli moja ambayo nami imenibadili mtazamo wangu.

Alisema eti laiti angejua asingeoa, angeishi kama bachelor maisha yake yote.

Nahisi kauli yake ilitokana na kupishana mara kwa mara baina yake na mzazi mwenzake ambaye ni mama yangu.

Wazazi wangu wameenda age kidogo baba yangu yuko kwenye early seventy's wakati mamangu ni mid sixty's.
Wamekuwa katika ndoa for more than fourty years lakini uwa hawaishi kutofautiana mpaka sisi tumeshazoea hiyo hali.

Hiyo kauli yake imenifanya na mimi niwaze kuwa bachelor maisha yangu yote.

Nitasaka mtoto but no kuishi na mwanamke wala ndoa.
 
Kila anachosema baba kipo sawa?...wot if yeye ndio analeta mifarakano kwny ndoa?

Things are complicated, sio kila anachosema kiko sawa ni mengi tu uwa nina ya ignore
Halafu mkuu hakuwa ananipa ushauri ni kauli tu aliyosema katika mazungumzo lakini naona imeniaffect
 
elmagnifico

mkuu hayo aliyosema baba yako anaweza akawa sahihi kabisa kwasababu kuna wanawake yaan unajiuliza huyu alifundwa na binadam kweli?! Wanawake wanaweza kukufanya ukawa na roho ya kinyama sana au unaweza kuwa na mtizamo tofauti kabisa juu ya hawa viumbe.
Mzee wako yupo sahihi kabisa kwa kauli aliyokwambia.
 
Kweli mkuu ikitokea mtu akapata wrong person tena kwa ndoa zetu za kanisani nadhani ni majuto for the rest of her/his life
 
Things are complicated, sio kila anachosema kiko sawa ni mengi tu uwa nina ya ignore
Halafu mkuu hakuwa ananipa ushauri ni kauli tu aliyosema katika mazungumzo lakini naona imeniaffect
yapo yaliyokuaffect waache wazazi wako na yanayowasibu!
Burden ya kutofanikiwa kwenye ndoa yao yanawatosha
Usiwabebeshe lingine la kufanya watoto wao wasifanikiwe kwenye ndoa/mahusiano yao
 
Jamani sasa ili kuiboresha mmu na kuirudisha zama zake tujaribu kuweka filter kwenye ubongo, si kila kitu cha kuleta hapa, mambo mengine ukitumia sehemu ya akili ndogo tu aliyokupa Mungu unapata majibu wala huna haja ya kuleta hapa thread isiyo na kichwa wala miguu.
 
labda amekupa angalizo uwe makini unapotafuta mke.......ndoa si kitu cha kufanya ujutie labda tu ikitokea haujapata mtu sahihi ndiyo unaweza kujuta....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom