Ningejiajiri kwenye kilimo ningekua mbali sana

Kwa kuwa lengo lako ni kufunguana macho, usinialike kuangalia mafanikio...nialike sasa nione njia ya kuyafikia mafanikio. Ninatamani sana kuona set up yako ya mabanda ya nguruwe nipate inspiration.
Nitakualika mkuu... Litakua shamba darasa
 
Mkuu hongera sana kwa jitihada zako..... ila nakuomba ulijibu swali lake la msingi huyo bwana
Kwani mnatumia hela ngapi kutafuta kazi? Kuanzia nauli za kwenda kwenye interview mpaka kuhonga sometimes? Kuku na mbuzi ni sh ngapi?
 
Kuajiriwa kunapoteza muda sana labda kwa wachache wanapiga mshahara wa m40+ na wale wanaopewa boom la 10,000/- kwa siku huku wakipewa hela na marupurupu mengine hadi hela ya kunyolea, kukata kucha na kupeleka nguo kwa dobi lakini wengine kujiari hususani kwenye kilimo ndo sehem ya kutokea.
Tatizo watu wanachukulia kilimo kuwa ni ukosefu wa elimu na ni kazi ya masikini bila kujua kipato kinachopatikana shambani ukilima kitaalam au ukajali mimea yako ipasavyo.
 
Hicho kilimo ungekifanya kwa mtaji kutoka wapi? Na sasa hivi unalima kwa pesa kutoka wapi?
Hizi fikra za kwamba unahitaji mamilioni kuanza project ndio zinawarudisha nyuma...nimeeleza vizuri kwamba si lazima uanze kama mi ninavyoanza..hela kidogo zinazotumika kutafuta kazi kwenye agribusiness si hella ndogo..nauli zinazotumika kwenda kwenye mainterview na hata kuhonga sometimes ni kitu.. Sikulazimishi uamini ninachoamini lakini take your time kujifunza utaelewa
 
Thiis is high level of understanding mkuu big up...kilimobiashara mtu anazalisha mwaka mzima tena mazao ambayo sokoni hayaharibiki haraka so unaweza hata kuexport.. Kuna miradi ya nyuki ynavuna hata zaidi ya mara tatu kwa mwaka. Tatizo watu wakiskia kilimo wanajua ni kile cha kusubiri mvua za masika
 
Haya ndo mambo mkuu. Na hapa ndo umuhim wa kujenga kijijini unapoonekana maadam kuna njia za kulink na main road. Huku unafanya kitu utakacho kilimo, ufugaji kama huo kwa kadri utakavyo. Umeme sola zinapiga kazi, maji unachimba kisima chako; network siku hizi hadi vijijini halotel wameokoa jahazi tunastream tu video huku tukifanya matembezi madogo kwenye mashamba.
Kilimo kina raha yake ndo maana JK hajawaacha ng'ombe wake.
 
Mkuu umedumu sana kwenye ajira .. pole sana.

Ebu fikiria kuhusu hii .. ni ndogo lakini ina faida kubwa kupita kiasi ...
Jaribu kilimo cha Nyanya chungu .. kwanza changamoto zake ni ndogo sana ..
Ukianza kuvuna ,, kwenye matuta 3 unaweza kupata ndoo 3 za nyanya chungu kila siku. Ndoo moja inauzwa Tshs. 12,000/= x 3 x 30 = 1,080,000.00 Kwa mwezi.
Zao hili unavuna kwa mwaka mzima na ni bila kuweka kwenye green house.
 
Mtaji wa kwanza na muhimu ni akili na utayari wa kuamua. Mtaji wa pili ni nguvu yaani afya njema. Hivi vikiunganishwa unapata mtaji wa fedha.
Kilimo kinalipa sana ukitumia hayo mambo mawili.
 
Ni kweli kabisa mkuu. Kwenye nyuki nimeiona hiyo nilikuwa Shinyanga kwa wazungu fukani hivi wa shirika nimekuta wamefuga nyuki wa kutosha sehem ambayo sikutarajia nikawa nafikiria sana juu ya ufugaji wake na ninadhani nitaifanyia kazi ili niweke mizinga katika himaya yangu na nipate asali safi na pia niuze niachane na kununua asali kwa bei ghali kila nipitapoa Dodoma-Singida.
Kilimo ni kila kitu, ukachanganya na biashara ya mazao unaishi kama mfalme hakuna shida, hakuna njaa kwako. Matunda, maziwa yanakuwepo tena mtu anachukua toka shambani anakula.
 
Kwani mnatumia hela ngapi kutafuta kazi? Kuanzia nauli za kwenda kwenye interview mpaka kuhonga sometimes? Kuku na mbuzi ni sh ngapi?
Hujajibu Mkuu...hebu jibu badala ya kushusha tuhuma
 
Yap Mkuu wewe ni kama vile tayari umejua nilichopanga... nitajenga ghala kubwa la mazao badae kwa hiyo mazao kama mahindi na mpunga nanunua tu kwa wakulima yanakaa humo. Na hili nililiandika kwenye diary yangu mwanzoni mwa mwaka huu kama moja ya malengo ya baadae. Mi ntakua nalima mazao mengine tu kipindi chote cha mwaka mzima
 
Asante mkuu kwa wazo zuri kama hili sikua nalo kuhusu nyanya chungu...ngoja nifanye utafiti wa mbegu bora
 
Inna-allahu-maswaabrina!

Je subira yangu haitatimu?
 
Haya mambo ya kuajiriwa na kujiajiri ni changamoto sana wakuu. Nionavyo mimi wengi tunakosea sana kudhani kwamba ukiingia kwenye kilimo au biashara ndo ghafla bin vuu utafanikiwa. Kiuhalisia ni mchakato unaohitaji subira ili kufikia malengo. Kwamfano mtu anaeanza biashara leo from the scratch itabidi ajipe mwaka mzima au na zaidi ili kwanza kuweza kuaminika na jamii hasa bankers na wadau wengine wa biashara yake. Na katika huo muda ndo muda wa kupigika na kuonyesha uaminifu wa hali ya juu. Sasa kosa ni pale kijana anatoka na ndoto zake za chuo au huko kwenye alipokuwa ameajiriwa anataka ghafla atoboe. Jamani uvumilivu na uaminifu ndo mtaji wa kwanza.
 
Mkuu, unaposema kupanga mizinga kny bee house ina maana kunakuwa na nyumba ya kupanga hiyo mizinga? Nilidhani inatundikwa tu juu ya miti msituni..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…