Ningejiajiri kwenye kilimo ningekua mbali sana

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
11,277
15,522
Wanabodi,

Ni mwaka wangu wa nane sasa kwenye ajira, nikijiangalia sina mafanikio ninayoota kuwa nayo na nahisi itachukua muda kuyafikia. Katika tafakari zangu nikagundua kama ningejiajiri kwenye kilimo biashara hata just 3 years back ningekua mbali sana.

Hivi sasa nimeanza mchakato wa kuingia kwenye kilimo biashara na dalili zinaonekana kuwa nzuri. Kila nikiingia humu na kukuta watu tunapambana kutafuta ajira nasikitika sana kwa kuwa miaka kumi ya ajira ni sawa na miwili au mitatu ya kilimo biashara. Kama hamniamini fanyeni utafiti mdogo tu hakika mtabadili mawazo.
 
acha kazi uone kumbe wewe mawazo uchwara kitaa tunalia ajira ww unalalamika nini huna swaga acha kazi ule nyasi
 
Wanabodi,

Ni mwaka wangu wa nane sasa kwenye ajira, nikijiangalia sina mafanikio ninayoota kuwa nayo na nahisi itachukua muda kuyafikia. Katika tafakari zangu nikagundua kama ningejiajiri kwenye kilimo biashara hata just 3 years back ningekua mbali sana. Hivi sasa nimeanza mchakato wa kuingia kwenye kilimo biashara na dalili zinaonekana kuwa nzuri. Kila nikiingia humu nakukuta watu tunapambana kutafuta ajira nasikitika sana kwakuwa miaka kumi ya ajira ni sawa na miwili au mitatu ya kilimobiashara. Kama hamniamini fanyeni utafiti mdogo tu hakika mtabadili mawazo.
Hizi ndoto ni nzuri, pigana kuzifikia, nakuunga mkono ndugu, kama capital inakuruhusu karibu kwenye kujiajiri, tafuta elimu ya unachohitaji kukifanya ili mwisho wa siku ukifanye kwa ufanisi, penye niya pana njia.
 
Wanabodi,

Ni mwaka wangu wa nane sasa kwenye ajira, nikijiangalia sina mafanikio ninayoota kuwa nayo na nahisi itachukua muda kuyafikia. Katika tafakari zangu nikagundua kama ningejiajiri kwenye kilimo biashara hata just 3 years back ningekua mbali sana. Hivi sasa nimeanza mchakato wa kuingia kwenye kilimo biashara na dalili zinaonekana kuwa nzuri. Kila nikiingia humu nakukuta watu tunapambana kutafuta ajira nasikitika sana kwakuwa miaka kumi ya ajira ni sawa na miwili au mitatu ya kilimobiashara. Kama hamniamini fanyeni utafiti mdogo tu hakika mtabadili mawazo.
Yaani ndio kwanza umeanza mchakato tayari umeshaanza kuhubiri mafanikio. Nini kinakufanya uamini kwamba wazo lako ni jipya?

Mimi nakushauri uweke akiba ya maneno. Tanzania hii ina fursa half way. Ukisikia mtu anahubiri kuhusu kilimo, basi mtafute na anayehubiri kuhusu masoko ndio uunganishe mahubiri yao yawe ndoto kamili. Kulima peke yake sio tija kwani mazao hayalimwi ili uyaangalie kwa macho shambani. Kimbiji yoooote ile imejaa matikitiki, Bagamoyo imejaa mananasi...lakini vyooote ni matunda yanayoliwa na wananchi kwa msimu.

Wazo lako zuri, ushauri wangu ni kwamba USIPOTEZE MUDA KUHUBIRI MAFANIKIO YA NDOTO ZAKO, JIKITE KWENYE UKAMILIFU WA WAZO LAKO vinginevyo utajuta. Unaowaona wameajiriwa si kwamba hawana akili, hata huko kulima kunahitaji mtaji.
 
Hicho kilimo ungekifanya kwa mtaji kutoka wapi? Na sasa hivi unalima kwa pesa kutoka wapi?
Kwa wewe kwa tafakuri yako, unadhani pesa ndizo zinazolima? Tena simaanishi kuwa kulima ni kushika jembe na kukwatua aridhi. Pia simaanishi kulima kwa kutumia nyenzo kama, matrekta, na jembe la ngombe. Kilimo ni zaidi ya hayo yote.
 
Wanabodi,

Ni mwaka wangu wa nane sasa kwenye ajira, nikijiangalia sina mafanikio ninayoota kuwa nayo na nahisi itachukua muda kuyafikia. Katika tafakari zangu nikagundua kama ningejiajiri kwenye kilimo biashara hata just 3 years back ningekua mbali sana. Hivi sasa nimeanza mchakato wa kuingia kwenye kilimo biashara na dalili zinaonekana kuwa nzuri. Kila nikiingia humu nakukuta watu tunapambana kutafuta ajira nasikitika sana kwakuwa miaka kumi ya ajira ni sawa na miwili au mitatu ya kilimobiashara. Kama hamniamini fanyeni utafiti mdogo tu hakika mtabadili mawazo.
haina guarantee kama ungeanza miaka mitatu iliyopita basi ungefanikiwa tu.Fursa inapokutana na mtu sahihi katika wakati sahihi huzalisha mafanikio.Kimojawapo kisipokuwepo basi mafanikio unakuwa msamiati.All the best.Usisahau kutupa mrejesho.
 
Yaani ndio kwanza umeanza mchakato tayari umeshaanza kuhubiri mafanikio. Nini kinakufanya uamini kwamba wazo lako ni jipya?

Mimi nakushauri uweke akiba ya maneno. Tanzania hii ina fursa half way. Ukisikia mtu anahubiri kuhusu kilimo, basi mtafute na anayehubiri kuhusu masoko ndio uunganishe mahubiri yao yawe ndoto kamili. Kulima peke yake sio tija kwani mazao hayalimwi ili uyaangalie kwa macho shambani. Kimbiji yoooote ile imejaa matikitiki, Bagamoyo imejaa mananasi...lakini vyooote ni matunda yanayoliwa na wananchi kwa msimu.

Wazo lako zuri, ushauri wangu ni kwamba USIPOTEZE MUDA KUHUBIRI MAFANIKIO YA NDOTO ZAKO, JIKITE KWENYE UKAMILIFU WA WAZO LAKO vinginevyo utajuta. Unaowaona wameajiriwa si kwamba hawana akili, hata huko kulima kunahitaji mtaji.
Mkuu nimegundua wewe pia ni miongoni mwa watu ambao wanaweza kushindwa hata kabla ya kuanza...kwa sababu wengi wanoshindwa ni kwa sababu hawafanyi utafiti wala projections ya mafanikio ya mbeleni ambayo hata nusu yake tu ukiyafikia wewe umefanikiwa... nilichohubiri mimi sio mafanikio ya uwekezaji bali ya ku-connect dots forward not backward. Na hili huhitaji akili ya ziada kuifanya..sikurupuki...miezi 6 ijayo ntakukaribisha uje ujionee kwa macho mkuu.. lengo ni kufunguana
 
Kwa wewe kwa tafakuri yako, unadhani pesa ndizo zinazolima? Tena simaanishi kuwa kulima ni kushika jembe na kukwatua aridhi. Pia simaanishi kulima kwa kutumia nyenzo kama, matrekta, na jembe la ngombe. Kilimo ni zaidi ya hayo yote.
Ni kilimo gani hicho ambacho hakihitaji pesa, trekta wala jembe?
 
haina guarantee kama ungeanza miaka mitatu iliyopita basi ungefanikiwa tu.Fursa inapokutana na mtu sahihi katika wakati sahihi huzalisha mafanikio.Kimojawapo kisipokuwepo basi mafanikio unakuwa msamiati.All the best.Usisahau kutupa mrejesho.
Mkuu...nimefanya utafiti ndio maana nimesema miaka mitatu au miwili...tena hata hivyo ni mingi... kiufupi tayari ninashamba la ekari 20 ambalo nimeshajemga mabanda 15 kwa ufugaji wa nguruwe, mabanda ya kuku, mbuzi. Kilimo cha mbogamboga na matunda ambapo nimetuma sample ya udongo kituo cha utafiti ili nijue virutubisho vinavyopungua ambapo mwishoni mwa mwaka huu nitaweka greenhouse. Nimemnunulia fundi vifaa vya mizinga ya nyuki ambapo mpaka sasa tumetengeneza mizinga 23 bado kuipaka rangi na kuipanga kwenye bee house lengo ni kuweka mizinga mia mbili ila awamu hii ya kwanza ni mizinga 100
 
Ni kilimo gani hicho ambacho hakihitaji pesa, trekta wala jembe?
Mkuu tuelewane...kuna watu wameanza na mbuzi au kuku wawili na wako mbali mno leo hii..ninaushuhuda huo. elfu hamsini au Laki moja shambani ni hela nyingi sana tofauti na mtu anavyoweza kufikiri..kwa tarifa yako wote wanaotafuta ajira hiyo laki moja hawezi kuikosa kama akiamua
 
Sasa hata hao mbuzi na kuku utawapata bure?
 
Mkuu hongera sana kwa jitihada zako..... ila nakuomba ulijibu swali lake la msingi huyo bwana
Mkuu tuelewane...kuna watu wameanza na mbuzi au kuku wawili na wako mbali mno leo hii..ninaushuhuda huo. elfu hamsini au Laki moja shambani ni hela nyingi sana tofauti na mtu anavyoweza kufikiri..kwa tarifa yako wote wanaotafuta ajira hiyo laki moja hawezi kuikosa kama akiamua
 
Mkuu tuelewane...kuna watu wameanza na mbuzi au kuku wawili na wako mbali mno leo hii..ninaushuhuda huo. elfu hamsini au Laki moja shambani ni hela nyingi sana tofauti na mtu anavyoweza kufikiri..kwa tarifa yako wote wanaotafuta ajira hiyo laki moja hawezi kuikosa kama akiamua

Mkuu...nimefanya utafiti ndio maana nimesema miaka mitatu au miwili...tena hata hivyo ni mingi... kiufupi tayari ninashamba la ekari 20 ambalo nimeshajemga mabanda 15 kwa ufugaji wa nguruwe, mabanda ya kuku, mbuzi. Kilimo cha mbogamboga na matunda ambapo nimetuma sample ya udongo kituo cha utafiti ili nijue virutubisho vinavyopungua ambapo mwishoni mwa mwaka huu nitaweka greenhouse. Nimemnunulia fundi vifaa vya mizinga ya nyuki ambapo mpaka sasa tumetengeneza mizinga 23 bado kuipaka rangi na kuipanga kwenye bee house lengo ni kuweka mizinga mia mbili ila awamu hii ya kwanza ni mizinga 100

Mkuu nimegundua wewe pia ni miongoni mwa watu ambao wanaweza kushindwa hata kabla ya kuanza...kwa sababu wengi wanoshindwa ni kwa sababu hawafanyi utafiti wala projections ya mafanikio ya mbeleni ambayo hata nusu yake tu ukiyafikia wewe umefanikiwa... nilichohubiri mimi sio mafanikio ya uwekezaji bali ya ku-connect dots forward not backward. Na hili huhitaji akili ya ziada kuifanya..sikurupuki...miezi 6 ijayo ntakukaribisha uje ujionee kwa macho mkuu.. lengo ni kufunguana

Kwa kuwa lengo lako ni kufunguana macho, usinialike kuangalia mafanikio...nialike sasa nione njia ya kuyafikia mafanikio. Ninatamani sana kuona set up yako ya mabanda ya nguruwe nipate inspiration.
 
Back
Top Bottom