Ningejiajiri kwenye kilimo ningekua mbali sana

Mkuu...nimefanya utafiti ndio maana nimesema miaka mitatu au miwili...tena hata hivyo ni mingi... kiufupi tayari ninashamba la ekari 20 ambalo nimeshajemga mabanda 15 kwa ufugaji wa nguruwe, mabanda ya kuku, mbuzi. Kilimo cha mbogamboga na matunda ambapo nimetuma sample ya udongo kituo cha utafiti ili nijue virutubisho vinavyopungua ambapo mwishoni mwa mwaka huu nitaweka greenhouse. Nimemnunulia fundi vifaa vya mizinga ya nyuki ambapo mpaka sasa tumetengeneza mizinga 23 bado kuipaka rangi na kuipanga kwenye bee house lengo ni kuweka mizinga mia mbili ila awamu hii ya kwanza ni mizinga 100
"Dont tell people your dreams,show them"
 
Wanabodi,

Ni mwaka wangu wa nane sasa kwenye ajira, nikijiangalia sina mafanikio ninayoota kuwa nayo na nahisi itachukua muda kuyafikia. Katika tafakari zangu nikagundua kama ningejiajiri kwenye kilimo biashara hata just 3 years back ningekua mbali sana.

Hivi sasa nimeanza mchakato wa kuingia kwenye kilimo biashara na dalili zinaonekana kuwa nzuri. Kila nikiingia humu na kukuta watu tunapambana kutafuta ajira nasikitika sana kwa kuwa miaka kumi ya ajira ni sawa na miwili au mitatu ya kilimo biashara. Kama hamniamini fanyeni utafiti mdogo tu hakika mtabadili mawazo.
Usije ukadhani mafanikio yanakujaKwa Muda Mfupi... Katika sekta zote Hata ya Kilimo

Tanzania ina miaka 50 na Kilimo ndo uti wa mgongo ila Angalia Sasa Hivi Tupo wapi
 
Back
Top Bottom