BBT Mkombozi kwenye kilimo au laana?

ndoto2020

JF-Expert Member
Feb 25, 2017
203
315
1. Watanzania wenzangu naomba tushauriane kuhusu hichi kitu kinachoitwa BBT ? 4. Kilimo

JE KILIMO NI UTI WA MGONGO WA NCHI YETU? - Ndio , watu wote milioni 61 tunategemea kilimo kutulisha nafaka, mboga mboga, protein na matunda.
2. Kilimo kinatupa malighafi za viwanda vingi vya msingi.

3. Kilimo kinatupa fedha za kigeni
4. Kilimo kinatoa ajira nyingi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.
5. Kilimo ni usalama wa taifa kwa kulinda afya ya wananchi wake na utegemezi kwa nchi zingine.

KWA NINI KILIMO KILIKWAMA TANZANIA?
1. Technolojia hafifu ( BBT suluhu imetoa kwa kuwezesha mabenki na kampuni binafsi nyingi kuingia knye sector hii)

2. Mvua za kubahatisha - Hili lilikuwa tatizo kubwa sana , kilifanya kilimo kuwa ni biashara isiyokopesheka wala kuaminika kabisa sasa kwa mara ya Kwanza baada ya Uhuru tunaenda kuwa na schemes za umwagiliaji kila kanda.

3. Mbegu bora za uhakika na za bei nafuu ( BBT inaenda kuleta suluhu ya kudumu ya Tanzania kuwa na mbegu zake za uhakika na kwa bei nafuu TARI wamewezeshwa haswa.

4. Gharama za kufungua mashamba na kuandaa mashamba - Hili lilikuwa Tatizo kubwa kuliko jambo lolote lile . watu kibao walishika mapori hawayaendelezi kisa gharama za kuyaendeleza BBT inakufungulia maeneo na kuyaandaa kabisa - MUNGU ATUPE NINI TENA WAJASILIAMALI WA KILIMO TANZANIA?

5. Soko la mazao. Bashe na serikali wamechukua uamuzi wa busara sana kutufungulia mipaka ya kuuza mazao yetu nje ya nchi knye bei nzuri na kuifanya TFRA kununua mazao ya ziada . USHAURI WAPANUE WIGO WA MAZAO YA KUNUNUA YAWE MPKA KNYE LEGUMES , NA MAFAKA ZINGINE

USHAURI NAMNA YA KUBORESHA BBT.
1. Turuhushu watu wa kawaida wanaotaka kuwekeza knye kilimo walipie gharama halisi za mradi - Mfano wauze eneo rasmi la umwagiliaji kwa mkopo kwa bei ya soko.

2. Halmashauri zitumie zile asilimia 10 za walemavu kuwalipia wajane na vijana training ya BBT.

3. Tuingize incentive za viwanda kwenye haya maeneo na storage facilities . Kivipi ? ukiwekeza hapa ardhi iwe bure au free corporate tax

4. Tuanze kuongeza kodi knye mazao yanayoagizwa nje mpka asilimia 200 ili ku discourage uagizaji
 
Mapinduzi ya kilimo yanahitaji mda mrefu , kama akili yetu imezoea kilimo cha mazoea alaf kila sku mnalaumu kilimo hakilipi Kwa vyovyote vile mtamuona Bashe mpigaji na mwanasiasa.

Fedha za kigeni haziwez kuingia Kwa kutegemea kilimo chetu cha kuunga unga , na wananchi wetu hawawezi kilimo cha kisasa sababu ni maskini lazima serikali iingie kutoa support , atakayechangamkia hii bidii ya Bashe atanufaika lakini wale ambao watabeza ( na ndo kundi la wengi ) wataishia kulalamika.

Sisi viwanda hatuwezi sababu hatuna knowledge na pia hatuwezi kufanya competition na wenzetu waliotutangulia eg Chinese industry, tunachoweza ni kilimo ambacho pia ni Tia maji Tia maji , ni heri tukaongeza nguvu kwenye kilimo kule tunakoweza ili tufanye mastering na hvyo tuexport more.

Huku panahtaji kujitoa na mchakato wa mda mrefu kidog matunda yakianza kuonekana serikali itafanya tena jitihada ya kutafta masoko ndo wananchi mnatoboa na hapa unahtaji mtu upstair kama Bashe tatizo hii inch imejaa chuki , ukanda , na unafiki thus why akili ndogo hawamuelew Bashe wanamuona kama fisadi , Yes yawezakuwa anafaidika na anachofanya Ila maono yake Yana tija ....

Hii sio issue ya overnight kama ambavyo wengi wanatarajia , Ila angalau Kwa miaka miwili au mitatu tutaona kitu

Kama ilivyo Kwa mambo mengine kuna kufeli na kupata wacha ajaribu ....

Bashe mi namuelewa na kwangu ndo presidential material sioni mwingine Kwa mle mjengoni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom