Huwa inatokea. Nilikuwa na ka site kangu Morogoro. Majirani wote walionizunguka walishajenga. Jirani yangu wa ubavuni akapanda MIGOMBA ubavuni kwake.
MIGOMBA ile ikatambaa mpaka ktk site yng. Mimi sina habari, nipo chuo. Mara moja kwenda kutembelea kale ka site, nikakuta migomba imeingia hadi kwangu. Nikapanick. Kumuuliza, akantuliza kwa kusema yupo tayari kuifyeka migomba wakati wowote mi ntakapoona inafaa.
Kwa aibu, mbele ya mkewe na wanae, nikamuambia basi aiache tu, baadhi ilikuwa inakaribia kukomaa.
Ya Mungu mengi. Yule Mzee akafariki mimi nikiwa Chuo. Kwa ujirani mwema, nikatuma na ubani.
Baada ya msiba kupoa, nikaenda kuwaelewesha kwa upole kuhusu ile habari ya MIGOMBA. Sikuamini macho, maskio na akili yangu. Mke wa marehemu aliniruka. Akasema hajui na kwamba lile eneo Lao.