Ninataraji kuvuna Maboga. Wapi ninaweza kupata soko?

Penyenia

Member
Aug 5, 2016
40
95
Habari wanajukwaa,

Nahitaji kujuzwa wapi naweza pata soko la maboga, kwani nataraji kuvuna maboga takriban fuso moja au zaid mnamo mwezi wa nane. Nimelima mkoani Tanga wilaya ya Handeni.

Nilipanda maboga kwa lengo la kuhifadhi unyevu kwenye shamba langu la mahindi,lakini kwa jinsi yalivyomea na kuzaa ndio napata wazo la kutafuta soko. Karibuni.
 
kirikou1

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
3,953
2,000
hongera mkuu, kama yangekua tayari kipindi hiki cha Ramadhan hakika mambo yangekua mujarabu
fuatilia masoko makubwa kama ngamiani au masoko ya dar
 
CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
6,893
2,000
Maboga chakula kizuri sana kuna maeneo nilikuwaga haya maboga yabapijwa then yanachanganywa na unga wa mahindi na yanasongwa.Hahaa unakula hata bila mboga
 
CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
6,893
2,000
Ni chakula kizuri ila mtaani ukionekana unakula watasema kaishiwa.

Maboga nayala sana sema muda unakuwa hauopo. Ila peleka Supermarjet sema ndo hizo zingine zinafungwa kama NAKUMAT
 
PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Mar 25, 2016
9,322
2,000
Prof nipe huo utaalamu nitengeneze siku moja maana me ni mdau wa african cuisines
Mkuu upishi wake sio kazi unalichukua boga unalikata vipande unavyoona vitashikikika vizuri mkononi pale utakapo kuwa unakula unavitia kwenye sufuria unatia maji kiasi kulingana na wingi wa maboga yako unatia na chumvi kiasi baada ya hapo unafunika na kutenga yaache yachemke hadi yawe malaini kiasi hapo yanakuwa tayari kwa kuliwa mimi huwa nikipakua natumia kijiko kulia huwa yanakuwa matamu sana hasa ukipata na kikombe cha chai
 
asante sana mkuu, baada ya kuhangaika na dunia nikitulia sehemu inayoeleweka nitafanya Eden on earth mambo kama hizi hazitakosekna. mpaka sasa nimepata aina mbili za mbegu zake hope until those days ntakua nimepata all varieties
 
Penyenia

Member
Aug 5, 2016
40
95
Miss Natafuta! ni wapi huko wanakonunua boga kwa tshs 3000/= hadi 7000/=? kwa sababu ndio natafuta soko hivyo kabla sijayafanya chakula cha ng'ombe.
 
Penyenia

Member
Aug 5, 2016
40
95
Miss Natafuta pita na huku, kwani nahtaji kujua lilipo hilo soko ambalo maboga huuzwa kwa bei hiyo ulioitaja.
 
realpatriot

Member
May 28, 2009
87
125
mkuu maboga ni chakula safi sana kwa watu wanaojali afya zao kama mimi kutokana na kwamba mara nyingi nachelewa kurudi nyumbani napenda kupata chakula laini ili niamkapo asbh niwe mwepesi...SASA khs soko lake kwa kweli lipo na ni kubwa sana kwa maana boga dogo kabisa nanunua kwa 3000 na kubwa mpaka 6000 hii ni kwa masoko ya stereo na tegeta ,kwa maelezo haya naomba fanya utafiti taratibu lazima utauza tu tena kama huna papara yavune weka sehemu kavu na kivulini uuze kidogo kidogo mpaka utakapo maliza...NAWASILISHA
 
Mkuu realpatriot ahsante kwa mchango wako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom