Soko la maboga

BARA BARA YA 5

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
1,127
734
Wakuu habari,

Nimepanda maboga ya kisasa F1 kama elfu 2 hivi, nataraji kuvuna maboga zaidi ya elfu 8. Naomba mwenye kujua soko zuri la maboga yenyewe yakiwa mabichi, mbegu zake au unga wa maboga.

Shamba lipo Bagamoyo.

Asanteni
 
Yanalipa tafuta watu wanaofuga nguruwe, ngombe, mbuz ata mabata wanakula mifugo mingi tu n chakula chao kizur
 
Maboga yanaliwa tafuta masoko masokoni, ningekuwa karibu ningenunua, mazuri kuchemsha kutengeneza futari hata kutengeneza supu.
 
Naleta mrejesho......Maboga yanauzika sana ndugu zangu,nimeuza vizuri kwa bei 3 tofauti..2500,1800 na 1000.Changamoto sikutoa huduma nzuri ula sasa naingia tena kazini
 
unalima breed gani ya boga, maboga yapo ya aina nyingi mkuu. mbegu za maboga ni dili kwa nchi za uarabuni.

changamoto ni wakulima hawana uwezo wa kukidhi vigezo vya mnunuzi. ili uweze kuexport kuna vigezo mnunuzi anatoa kuanzia aina ya boga, moisture, ujazo na uweze kusuply kwa muda ambao wao watahitaji

Kuna mzee ana kampuni na alipata tenda ya kusuply huko uarabuni, ishu ikawa anashindwa kupata tani wanazozihitaji kwa muda waliopanga. mfn supplier uwe na uwezo wa kusuply container 4 za futi 40 kwa mwaka mara nne. Huo mzigo unapata wapi? Alijaribu kuwahusisha wakulima wengine ili anunue mzigo kutoka kwao, lakini njaa inawafanya wanauza nje ya makubaliano. Tenda ilimshinda mkataba ukavunjika

mazao mengi yanahitajika nje, changamoto ni kukidhi standards zinazohitajika na wanunuzi.

Kwenye maboga tukiwa na kilimo cha pamoja, kuhusisha watu wengi ili ulkukidhi demand ya mnunuzi inawezekana. Ukisema ni kuingia kivyakovyako ni ngumu aisee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom