Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Mkuu napo sijajua unaenda kufanyia nini lakin sikushauri uwaachie pesa yote hiyo, ukiweza punguza muda tuone inakuaje pia interest CRDB kwa mfanya biashara huwa ni 14% na wana reduce kila mwezi
 
Mimi sio Kapuku mkuu na sijawahi kuchukua mkopo na niko vizuri kimaisha
Naombwa kila leo nichukue mkopo ila nimekataa na ninaendelea na maisha mazuri kuliko hao makapuku waliochukua mkopo bila akili na mwisho kwa aibu gari linapita na maspika kutangaza uuzwaji wa nyumba zao na kurudi umasikini au kuwa jambazi kabisa na kwenda kutafuta SMG
Ila hao matajiri kila mmoja ana nafsi yake
Hahaaaaa
Kwamba jamaa baada ya benki kuuza nyumba yake kawa jambaka
 
Habari za asubuhi wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
Asilimia 16% ya milion 50 au asilimia 16% ya kila unachotakiwa kurejesha kwa utaratibu utakaopewa !?
 
Kwa mwaka riba ni 4M nalipa sawa na 400k per month

Mkuu, kwa nilivyokuelewa hiyo 400K ni rejesho ya riba, Je rejesho lote (riba + deni) kwa mwezi itakuwa kiasi gani?

Umesema unataka kuweka UTT, kwa uelewa wangu ukiweka UTT hiyo 50M mfuko wa bond, kwa mwezi utapata ~430K.

Je hiyo faidia ya mwezi kutoka UTT itaweza kulipa rejesho lote la mwezi kwenye benki? Utabakia na kitu chochote?

Kwa kifupi,
Mimi niliwahi kupiga mahesabu ya kuchukua mkopo benki na kupeleka UTT, na ile faida ya UTT ndo iwe rejesho, lakini mahesabu yalikataa. Faida unayoipata UTT ni ndogo / haiwezi rudisha rejesho lote kwa mwezi labda uongezee kutoka mfukoni mwako.

Au, uongee na hao watu wa mkopo wa benki waweze kupunguza rejesho lako la kila mwezi, lakini hii itafanya muda wa kurudisha mkopo uwe mrefu zaidi.
 
Shida siyo mkopo. Shida ni unaenda kufanyia nini? Usijekuta unaenda kujenga fremu za maduka Kantalamba.
Zile hesabu za makaratasi eti fremu moja napangisha Laki na nusu kwa mwezi, kwa hiyo frem 10 ni milioni moja na nusu kwa mwaka milioni 15, kwa miaka 9 ni 15M x 9
🀣🀣🀣
 
Niko in between kuchukua nataka na kuacha pia nataka
Nakushauri uachane na huo mkopo. Unaweza kufikiri 50m, ni pesa nyingi, lakini kwa hali ya uchumi ilivyo sasa, ni pesa kidogo sana.

Badala yake save benki hiyo pesa ambayo ungelipia huo mkopo. Iweke kwenye fixed deposit account kwa miaka mitano. Tanzania commercial bank

Baada ya miaka mitano utakuwa umesave 50m, ukijumlisha na riba inaweza kufika 70m
 
Wewe ni mtumishi, riba sioni kama ni shida kinachokusumbua hapo ni wivu kuona bank wanaenda tajirika kupitia wewe unasahau hata usipo kopa wengine watakopa , tuje kwenye ushauri je uwekezaji unaotaka kufanya utakuwepo zaidi ya hiyo miaka tisa, je una experience na hicho kitu kuwa kina faida, je gharama za uendeshaji zitakuwaje iwapo mkopo utaisha
 
Je unauhakika hiyo miaka tisa utakuwa hai?
Je una uhakika hiyo miaka tisa utakuwa bado kwenye ajira?
Je unauhakika usipochukua hiyo mil 50 baada ya miaka tisa utakuwa umeipata?

Je vipi familia yako leo na miaka tisa ijayo je itaitaitaji chumba kimoja na sebule, itaitaji Bill ya maziwa tu au itaitaji na ada ya shule nk

Jiulize hayo maswali majibu yakiwa
A. Sina uhakika kama takuwa bado hai miaka tisa ijayo
B. Sina uhakika na ajira mda wowote naweza fukuoka au kupata maradhi nikawa nje ya kazi
C.sina uhakika wakuwa na milion 50 baada ya miaka tisa ijayo
D. Baada ya miaka tisa sitaitaji chumba na sebule. Sitaitaji kulipa bill ya maziwa pekee taitaji kulipa ada nk

Kama majibu ni A mpaka D kachukue pesa hiyo fanya mambo yako usiogope miaka tisa kwani kabla ya hiyo milion 50 ulikiwa hauishi

MY TAKE
Kama huna nyumba katika hiyo milion 50 chukua milioni 20 jenga sehemu ya kujihifadhi hiyo miliom 30 ndio ichezee ni aibu sana salary slip inaso,a deni milion 90 unaishi nyumba ya kupanga aibu na utapata stress maana ukweli usemwe hiyo pesa itaisha tu hilo ujue kwaiyo ikiisha utabakije ndio hapo sasa
 
ushauri wa bure ndugu yangu,kukopa harusi kulipa ni matanga miaka 9 ni mingi mnoo kama unauwezo dunduliza pesa yako,nnamkopo wa miaka 4 naliona joto lake nilikopa nikaekeza ktk biashara,plani ikaenda mrama nalipa uku nnaumia
 
Mkuu, kwa nilivyokuelewa hiyo 400K ni rejesho ya riba, Je rejesho lote (riba + deni) kwa mwezi itakuwa kiasi gani?

Umesema unataka kuweka UTT, kwa uelewa wangu ukiweka UTT hiyo 50M mfuko wa bond, kwa mwezi utapata ~430K.

Je hiyo faidia ya mwezi kutoka UTT itaweza kulipa rejesho lote la mwezi kwenye benki? Utabakia na kitu chochote?

Kwa kifupi,
Mimi niliwahi kupiga mahesabu ya kuchukua mkopo benki na kupeleka UTT, na ile faida ya UTT ndo iwe rejesho, lakini mahesabu yalikataa. Faida unayoipata UTT ni ndogo / haiwezi rudisha rejesho lote kwa mwezi labda uongezee kutoka mfukoni mwako.

Au, uongee na hao watu wa mkopo wa benki waweze kupunguza rejesho lako la kila mwezi, lakini hii itafanya muda wa kurudisha mkopo uwe mref
 
Mkuu, kwa nilivyokuelewa hiyo 400K ni rejesho ya riba, Je rejesho lote (riba + deni) kwa mwezi itakuwa kiasi gani?

Umesema unataka kuweka UTT, kwa uelewa wangu ukiweka UTT hiyo 50M mfuko wa bond, kwa mwezi utapata ~430K.

Je hiyo faidia ya mwezi kutoka UTT itaweza kulipa rejesho lote la mwezi kwenye benki? Utabakia na kitu chochote?

Kwa kifupi,
Mimi niliwahi kupiga mahesabu ya kuchukua mkopo benki na kupeleka UTT, na ile faida ya UTT ndo iwe rejesho, lakini mahesabu yalikataa. Faida unayoipata UTT ni ndogo / haiwezi rudisha rejesho lote kwa mwezi labda uongezee kutoka mfukoni mwako.

Au, uongee na hao watu wa mkopo wa benki waweze kupunguza rejesho lako la kila mwezi, lakini hii itafanya muda wa kurudisha mkopo uwe mrefu z
 
Mkuu, kwa nilivyokuelewa hiyo 400K ni rejesho ya riba, Je rejesho lote (riba + deni) kwa mwezi itakuwa kiasi gani?

Umesema unataka kuweka UTT, kwa uelewa wangu ukiweka UTT hiyo 50M mfuko wa bond, kwa mwezi utapata ~430K.

Je hiyo faidia ya mwezi kutoka UTT itaweza kulipa rejesho lote la mwezi kwenye benki? Utabakia na kitu chochote?

Kwa kifupi,
Mimi niliwahi kupiga mahesabu ya kuchukua mkopo benki na kupeleka UTT, na ile faida ya UTT ndo iwe rejesho, lakini mahesabu yalikataa. Faida unayoipata UTT ni ndogo / haiwezi rudisha rejesho lote kwa mwezi labda uongezee kutoka mfukoni mwako.

Au, uongee na hao watu wa mkopo wa benki waweze kupunguza rejesho lako la kila mwezi, lakini hii itafanya muda wa kurudisha mkopo uwe mrefu zaidi.
Sitaweka bond fund Mkuu nitaweka liquid fund na jikimu....narely kwenye compounding effect nitakaa pesa zikae zijizalishe Kwa miaka 30
 
Back
Top Bottom