Ninatafuta mpenzi/mume nipo serious

Ninatafuta mpenzi/mume nipo serious

Khira la heri mama, ila uwe makini na watu sie wanaume huwa hatueleweki, they can use your weakness to u again. Nc journey 4 fighting,
NB:Wife/ husband comes from God
 
nnm
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 47. Nina watoto watatu. Tulitengana katika ndoa baada ya kutendwa na kutelekezwa na mume. Nilikwazika na kukata tamaa sana ya mahusiano. Nilikaa muda mrefu sana bila mahusiano. Nikajaribu kuruhusu ya aliyejiita mlokole kumbe ilikuwa gear ya kuficha maovu.

Nikaangukia pua kwa mara ya pili na kuamua kuishi tena muda mrefu bila mahusiano. Kwa sasa basi ninahitaji kumpata mwanamume ambaye ana mapenzi ya dhati hasa uaminifu. Sihitaji kuolewa au niseme kuishi na mwanamume tena ila ninataka company tu. Na kupitia kampany nitaweza kujifunza kwa undani kama kweli mwanaume yuko siriazi au la. Ninachohitaji kwa sasa ni upendo wa dhati, nimerudia hapo.

Sitaki wababaishaji wa mahusiano na hapa atakayejitokeza awe mtu wa uhakika ambaye:

- Ni mgani i.e aliyefiwa na mkewe kwa misingi hii kama una baba yako hapa alifiwa na mama niunganishe tu. Au kaka yako ambaye amefiwa na mke niunganishe tu.

- Akubali kupima HIV

- Asiwe mume wa mtu au mwanaume ambaye hajao ila ana wanawake ambao ana connect nao. Hii imenigusa sana baada ya kukutana na mwanaume ambaye alizaa na several women kumbe ni mtu ambaye hana future kabisa kimaisha ya familia. Nilimpenda sana ila changamoto za wanaume kama hawa ni kubwa sana. Ni kujitakia presha.

- Anipe uhuru wa kufanya mambo yangu ya kiuchumi kwa kuwa nina watoto na ninahitaji wasiishi maisha ya tabu . Sitaki kuwa tegemezi hapa. Nimejifunza sana.

- Awe ananithamini mimi kama mpenzi wake na asinilazimishe ndoa mpaka pale nitapona kuwa kweli ni mtu wa kuzeeka naye.

- Awe ni mtu anayejituma katika kuzalisha mali, either ameajiriwa/kujiajiri au anafanya biashara zake.

- Awe ni mtu anayependa familia kwa kuanzia na watoto wake mwenyewe iwe ni priority kwake kabla hajawapenda wanangu mimi.

- Awe tayari kuandikiana pre-nuptial agreement kama itafikia mahali tuamue kuishi pamoja. Ninasema hivi kwa kuwa atakuwa na mali zake na wanawe ambao atataka kuwapa urithi na mimi nina wanangu na chochote kidogo nilichoweza kuhangaikia kwa miaka yangu hivyo sitaki ugomvi wa mali hata kidogo.

-Asiwe Mlevi au Mvuta sigara.

- Awe mkristu. Sibagui ila mimi ni mkristu na wangu pia hivyo itakuwa shida kidogo hapa. Nimekuwa mkweli msinielewe vibaya.

- Awe na miaka kati aya 47-50.

Ninasema sasa kwa mwanaume ambaye anaona anaweza kujaribu kuanzisha mahusiano na mimi karibu PM. Ukiona utatoa lugha mbovu isiyo na staha ninaomba upite taratibu.

Angalizo.
Nipo serious, ninaomba sitaki lugha za matusi ua mitaani mimi ni mtu mzima. Wanaume serious tu na wenye umri niliotaja wani Meseji (PM].
 
Khira la heri mama, ila uwe makini na watu sie wanaume huwa hatueleweki, they can use your weakness to u again. Nc journey 4 fighting,
NB:Wife/ husband comes from God
Asante nitakuwa makini sana. Mdogo maana nimesema tukikubaliana tunaandikiana pre-nuptial agreement ya Mali na mambo mengine. Niko smart.
 
Mpaka sasa hivi naona wachangiaji karibu wote wamechangia kwa heshima na taadhima, hii ni ishara kubwa ya wewe kufanikiwa Dada yangu. Binafsi nakutakia kila la kheri
Amina. Mola awabariki kwa nidhamu kubwa sana. Name ninaheshimu sana. Hata wachache walioteleza nimewajibu vuzuri na kule PM pia.
 
Halafu kuna wadada wengine huja na kejeli za uzi zao hapa hawataki waume. kumbe umri ukiwaenda hutafuta wanaume kama majangili
Asante sana ila Mimi Siyo jangili. Ukumbuke pia kuwa niliolewa pia hata mpaka sasa wapo wanaume wananitaka kwa kasi ila si type ninayotaka. Ningekuwa ninataka mume wa mtu wala nisingekuja hapa JF, hata 100 ningechukua.
 
Asante sana ila Mimi Siyo jangili. Ukumbuke pia kuwa niliolewa pia hata mpaka sasa wapo wanaume wananitaka kwa kasi ila si type ninayotaka. Ningekuwa ninataka mume wa mtu wala nisingekuja hapa JF, hata 100 ningechukua.
Nilikusudia kuna baadhi ya wadada huja na uzi humu na kejeri juu ya wanaume. sijakukusudia wewe dada samahani kama nimekukwaza
 
Asante sana ila Mimi Siyo jangili. Ukumbuke pia kuwa niliolewa pia hata mpaka sasa wapo wanaume wananitaka kwa kasi ila si type ninayotaka. Ningekuwa ninataka mume wa mtu wala nisingekuja hapa JF, hata 100 ningechukua.
Bado hujapata,njoo kwangu
 
Toka alhamisi hadi leo jumamosi nadhani mstahiki keshajitokeza kuwania nafasi

Kuomba unachokihiitaji ni jambo moja na kupata unachokitaka ni jambo la pili...Mungu akusimamie
 
Back
Top Bottom