Ninatafuta mpenzi/mume nipo serious

Loeli

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
997
763
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 47. Nina watoto watatu. Ninaishi Dar es Salaam.

Ninahitaji kumpata mwanamume ambaye ana mapenzi ya dhati hasa uaminifu. Sihitaji kuolewa au niseme kuishi na mwanamume kwa haraka ila ninataka company tu. Na kupitia kampani nitaweza kujifunza kwa undani kama kweli mwanaume yuko siriazi au la. Ninachohitaji kwa sasa ni upendo wa dhati, Nimerudia hapo.

Sitaki wabahishaji wa mahusiano na hapa atakayejitokeza awe mtu wa uhakika ambaye:

- Ni mgani i.e aliyefiwa na mkewe kwa misingi hii kama una baba yako hapa alifiwa na mama niunganishe tu. Au kaka yako ambaye amefiwa na mke niunganishe tu. Au awe Mtalaka na si kutengana.

- Akubali kupima HIV

- Asiwe mume wa mtu au mwanaume ambaye hajaoa ila ana wanawake ambao ana connect nao. Hii imenigusa sana baada ya kukutana na mwanaume ambaye alizaa na several women kumbe ni mtu ambaye hana future kabisa kimaisha ya familia. Nilimpenda sana ila changamoto za wanaume kama hawa ni kubwa sana. Ni kujitakia presha.

- Anipe uhuru wa kufanya mambo yangu ya kiuchumi kwa kuwa nina watoto na ninahitaji wasiishi maisha ya tabu . Sitaki kuwa tegemezi hapa. Nimejifunza sana.

- Awe ananithamini mimi kama mpenzi wake na asinilazimishe ndoa mpaka pale nitapona kuwa kweli ni mtu wa kuzeeka naye.

- Awe ni mtu anayejituma katika kuzalisha mali, either ameajiriwa/kujiajiri au anafanya biashara zake.

- Awe ni mtu anayependa familia kwa kuanzia na watoto wake mwenyewe iwe ni priority kwake kabla hajawapenda wanangu mimi.

- Awe tayari kuandikiana pre-nuptial agreement kama itafikia mahali tuamue kuishi pamoja. Ninasema hivi kwa kuwa atakuwa na mali zake na wanawe ambao atataka kuwapa urithi na mimi nina wanangu na chochote kidogo nilichoweza kuhangaikia kwa miaka yangu hivyo sitaki ugomvi wa mali hata kidogo.

- Asiwe Mlevi au Mvuta sigara.

- Awe mkristu. Sibagui ila mimi ni mkristu na wanangu pia hivyo itakuwa shida kidogo hapa. Nimekuwa mkweli msinielewe vibaya.

- Awe na miaka kati aya 47-52.

- Akiwa DSM ni vizuri. Nje ya DSM tutakubaliana workable situations.

- Vigezo visikutishe kama una vingi kati ya hivyo hasa umri na kutokuwa na mke tuwasiliane PM na ninaamini tutafikia muafaka wa pamoja.

Ninasema sasa kwa mwanaume ambaye anaona anaweza kujaribu kuanzisha mahusiano na mimi karibu PM. Ukiona utatoa lugha mbovu isiyo na staha ninaomba upite taratibu.

Angalizo.
Nipo serious, ninaomba sitaki lugha za matusi au mitaani mimi ni mtu mzima. Wanaume serious tu na wenye umri niliotaja wani Meseji (PM].
 
dah kwenye umri sipo.kwenye kufunga ndoa sipo.imekula kwangu.utampata tu mkuu.all the best
Asante sana sema katika umri niliokuwa nao na ninaohitaji itachukua muda pia. Nitavumilia ninaamini kama sitampatia hapa basi watu wataniunganisha na potential candidates.
 
Naogopa hata kucoment maana Mama mkubwa anaonekana hataki masikhara na kuzamilia kumpata Baba mkubwa wetu.

Kila la kheri Mama mkubwa, Mungu akupe hitaji la moyo wako.
Asante sana Humble African niko katika uhitaji wa ukweli na nimeusema moyo wangu ili mtu ajue kuwa sitanii hapa.
 
Kuna brother yangu sema ni mlevi sana vipi atakufaa?
Asante sana. Kwa mlevi hapana kabisa ndugu yangu. Tena ni kigezo sema nilisahau kukiweka pale juu labda ni edit kuna mambo mawili ninataka niongeze.
 
47- 50 yrs kwa sisi wanaume wa ki Tz tunakuwa tumeshatumika sana"

Hata pulling inakuwa ya kuvizia hasa kama umekulia mjini.

Hizo condition ulizozi-attach+ jina, zina tisha kidogo' na zinaweza kukufanya ukakosa potential bidder,

Kila la kheri ktk safari yako/usiku mwema.
 
47- 50 yrs kwa sisi wanaume wa ki Tz tunakuwa tumeshatumika sana"

Hata pulling inakuwa ya kuvizia hasa kama umekulia mjini.

Hizo condition ulizozi-attach+ jina, zina tisha kidogo' na zinaweza kukufanya ukakosa potential bidder,

Kila la kheri ktk safari yako/usiku mwema.
Hapa ninatafuta life partner kwa upande mwingine si mtu wa sarakasi kitandani. Binafsi nina miaka 47 na niseme niko busy na maisha na kazi zangu zaidi kuliko masuala ya sarakasi.

Kwa misingi hii pia kimaadili mimi kuwa na underage haitawezekana. Ingekuwa nina 30s then ningesema wa late 30 au 40s. Ndiyo maana hata hapa age range ni ndogo sana ya 3 yrs. Sijaweka conditions bali ni vigezo, hata wewe ulipokuwa unamtafuta mke/mume kuna vigezo uliweka na si lazima by 100% viwe sawa ila angalao vingi vipatikane.

Kuhusu jina kweli limetisha na linafanyiwa kazi. Mpaka kesho ninadhani Mh. Invisible atanisikia na avatar nitabadilisha pia. Uwe na amani sana.
 
Asante sana Mh. Invisible kwa kubadili ID yangu. Mungu akupe maisha tele.

Sasa ninatafuta pia avatar na nitabadili by kesho au leo baadaye. Wale mliokuwa mnatishika kwa jina msiogope tena.

Kwa sasa ninaitwa Loeli na lina maana kubwa sana kwangu.

Karibuni.
 
Si useme tu unatafuta mstaaafu mwenzako mle pension....
Hivyo hivyo hujakosea kabisa maana atakuwa ameshatafuta na mimi nimeshatafuta then tunaunganisha nguvu. Tunakula bata tu sasa si kutesana tena. Asante kwa kuliona hilo.
 
Asante. Mpaka sasa kama hujafahamu maana ya kupenda kwa dhati itakuwa ngumu sana kwangu kujieleza.
Mkuu hapo ndipo pamebeba mzimu wa kufeli unapokuwa kwenye mahusiano.
Ubebwe mgongoni ndio kipimo chako cha upendo wa dhati!!??
Usingwe Bafuni!!?
Upikiwe chakula???

Usibebe theory za kukufelisha ukaishia kuwachukia wanaume.
 
Mkuu hapo ndipo pamebeba mzimu wa kufeli unapokuwa kwenye mahusiano.
Ubebwe mgongoni ndio kipimo chako cha upendo wa dhati!!??
Usingwe Bafuni!!?
Upikiwe chakula???

Usibebe theory za kukufelisha ukaishia kuwachukia wanaume.
Asante.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom