Ninatafuta mpenzi/mume nipo serious

Ninatafuta mpenzi/mume nipo serious

Aisee kumbe jf humu tuna mama zetu na bibi zetu...........kila kheri mama

Sent from my HUAWEI Y330-U01 using JamiiForums mobile app
JF ni open kwa watu wote na kwa taarifa kuwa wazee mpaka maprofesa wamo humu ndani kwa ID fake kama ya kwangu.
 
JF ni open kwa watu wote na kwa taarifa kuwa wazee mpaka maprofesa wamo humu ndani kwa ID fake kama ya kwangu.
Sawa sawa ......ndugu

Sent from my HUAWEI Y330-U01 using JamiiForums mobile app
 
Haya nyie watu wazima njooni huku kuna msosi.
Niliomba comments za staha hapa. Heshimu andiko kama huwezi unaacha tu. Msosi mkeo au mama yako anaweza kukupikia ila siyo mimi tafadhali. Asante.
 
Mh 47-50 cjui km utampata,bora usinge garantee umri
Umri ni muhimu kwa kuwa mimi nina 47 siwezi kuwa na mwanaume umri wa chini ya hapo. Angalao awe hata 47-55 naweza kuingia meza ya makubaliano. Kwa hapa inawezekana si rahisi kumpata ila nimeomba hata kama mtu baba yake au ndugu amefiwa na mkewe basi aniunganishe kwa kuwa sitaki mwanaume wa mtu. Nimesema ninataka mgani tu hapa basi si mwingine. Na wagani ninajuwa wapo ila kwa umri huo kweli inawezekana kuwa JF hawapo. Ila mimi nina 47 niko hapa. Sema tu sijapata hiyo match.
 
True love is what all we need,
Hard to find it,
Hard to keep it.
 
tutafutie baba maana tunechoka kukuona mpweke mama etu 😉🙂
 
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 47. Nina watoto watatu. Tulitengana katika ndoa baada ya kutendwa na kutelekezwa na mume. Nilikwazika na kukata tamaa sana ya mahusiano. Nilikaa muda mrefu sana bila mahusiano. Nikajaribu kuruhusu ya aliyejiita mlokole kumbe ilikuwa gear ya kuficha maovu.

Nikaangukia pua kwa mara ya pili na kuamua kuishi tena muda mrefu bila mahusiano. Kwa sasa basi ninahitaji kumpata mwanamume ambaye ana mapenzi ya dhati hasa uaminifu. Sihitaji kuolewa au niseme kuishi na mwanamume tena ila ninataka company tu. Na kupitia kampany nitaweza kujifunza kwa undani kama kweli mwanaume yuko siriazi au la. Ninachohitaji kwa sasa ni upendo wa dhati, nimerudia hapo.

Sitaki wababaishaji wa mahusiano na hapa atakayejitokeza awe mtu wa uhakika ambaye:

- Ni mgani i.e aliyefiwa na mkewe kwa misingi hii kama una baba yako hapa alifiwa na mama niunganishe tu. Au kaka yako ambaye amefiwa na mke niunganishe tu.

- Akubali kupima HIV

- Asiwe mume wa mtu au mwanaume ambaye hajao ila ana wanawake ambao ana connect nao. Hii imenigusa sana baada ya kukutana na mwanaume ambaye alizaa na several women kumbe ni mtu ambaye hana future kabisa kimaisha ya familia. Nilimpenda sana ila changamoto za wanaume kama hawa ni kubwa sana. Ni kujitakia presha.

- Anipe uhuru wa kufanya mambo yangu ya kiuchumi kwa kuwa nina watoto na ninahitaji wasiishi maisha ya tabu . Sitaki kuwa tegemezi hapa. Nimejifunza sana.

- Awe ananithamini mimi kama mpenzi wake na asinilazimishe ndoa mpaka pale nitapona kuwa kweli ni mtu wa kuzeeka naye.

- Awe ni mtu anayejituma katika kuzalisha mali, either ameajiriwa/kujiajiri au anafanya biashara zake.

- Awe ni mtu anayependa familia kwa kuanzia na watoto wake mwenyewe iwe ni priority kwake kabla hajawapenda wanangu mimi.

- Awe tayari kuandikiana pre-nuptial agreement kama itafikia mahali tuamue kuishi pamoja. Ninasema hivi kwa kuwa atakuwa na mali zake na wanawe ambao atataka kuwapa urithi na mimi nina wanangu na chochote kidogo nilichoweza kuhangaikia kwa miaka yangu hivyo sitaki ugomvi wa mali hata kidogo.

-Asiwe Mlevi au Mvuta sigara.

- Awe mkristu. Sibagui ila mimi ni mkristu na wangu pia hivyo itakuwa shida kidogo hapa. Nimekuwa mkweli msinielewe vibaya.

- Awe na miaka kati aya 47-50.

Ninasema sasa kwa mwanaume ambaye anaona anaweza kujaribu kuanzisha mahusiano na mimi karibu PM. Ukiona utatoa lugha mbovu isiyo na staha ninaomba upite taratibu.

Angalizo.
Nipo serious, ninaomba sitaki lugha za matusi ua mitaani mimi ni mtu mzima. Wanaume serious tu na wenye umri niliotaja wani Meseji (PM].


and
 
Mpaka sasa hivi naona wachangiaji karibu wote wamechangia kwa heshima na taadhima, hii ni ishara kubwa ya wewe kufanikiwa Dada yangu. Binafsi nakutakia kila la kheri
 
Dada kama unatafuta mwenza usiandike au kutoa shutuma juu ya past relationship yako. kwani hutoa red flag kwa mpenzi utakaempata atakuona ni mtu wa shutuma tu.
 
Back
Top Bottom