Ninatafuta mpenzi/mume nipo serious

Ninatafuta mpenzi/mume nipo serious

Watu wengine huwa wanakosa wapenz wazuri sio kwa bahati mbaya ila ni kwasababu ya misimamo miingi kama hii yako ambayo kwa kiasi kikubwa umetawaliwa na umimi (ubinafsi). Hivi ni mtu gani anayejitambua utamwambia nataka ufate hiki, kile mara usiniingilie kwenye hiki na kile halafu naye akubali tu na kunywea kama vile sio binadamu mwenye hisia na mapendeleo?
Nakushauri tu, mahusiano yoyote (hata yasiyo ya kimapenzi) it's about compromise of what you believe kwa kiasi flani. Usipolikubali hilo utaendelea kuwa mpweke milele au kupata kampani za watu wenye malengo ya muda mfupi kama hao uliotangulia kuwa nao.
Hilo hata mimi nimeliangalia kwa jicho la tatu. Huyu mama sharti lake lililonishangaza zaidi ni hili na kutaka candidate awe amefiwa na mwenza!!! Nimefuatilia kuona labda naye ni mjane lakini naona si mjane bali mtalaka!!

Ukitumia busara kidogo utajiuliza sana.... Yeye katalikiwa lakini hataki mtaliki bali mfiwa...... Unaona hapa kama kuna walakini kidogo.

Masharti yote hayo, mwanamke kutalikiwa ni rahisi sana. Nachelea kusema labda talaka ilitokea sababu ya masharti yake.

Hakuna mahusiano ya masharti yaliyopata kudumu.
 
Mimi ni kijana umri miaka 25 sina kazi yoyote mision town! Yaani kula kulala siwazi saaana maisha ya hapo baaadae nawaza leo tu nitakula nini na nitalala wapi..... (same text missing)
Umesahau kumalizia kuwa wewe ni Jambazi sugu..... ujambazi nao ni kazi dogo.
 
Loeli a.k.a Bundimkubwa salamu.

Mojawapo ya kigezo ambacho naamini kinakwaza wengi ni hiki cha mlengwa shurti awe amefiwa na mwenza.....

Unaweza niambia ni kitu gani hasa kimekufanya umfikirie mfiwa zaidi na si mwinginewe??
Asante sana kigezo cha mfiwa au mgani nimekiweka kwa kuwa kwa umri wa miaka 47-50 mwanaume atakuwa na familia muda tu I.e ana mke. Hivyo kama hana mke atakuwa alifariki, walitengana, walitalikiana. Wa kutengana simtaki kwa kuwa ndoa bado ipo. Pengine hapa nilusahau kutalikiana.
 
Kama una mtoto wa kike ombea azae mtoto wa kiume uwe unamuita mume wako, miaka 47 ni ya kusubir wajukuu
 
Ahsante kwa ufafanuzi....

Swali dogo la nyongeza..... Huamini kuwa unaweza pata mwenza bila masharti???

Kwenye kigezo cha umri... kwanini awe na miaka 47-50?? Akiwa na miaka 52 au 45 kuna tatizo gani??
 
Sijaona kama amesema huyo mwenza anayemtafuta ni kwa ajili ya kuzaa watoto. Kwa umri huo mtu huhitaji company zaidi ya ngono na uzazi. Ukikua utakuja kujua.
 
Hilo hata mimi nimeliangalia kwa jicho la tatu. Huyu mama sharti lake lililonishangaza zaidi ni hili na kutaka candidate awe amefiwa na mwenza!!! Nimefuatilia kuona labda naye ni mjane lakini naona si mjane bali mtalaka!!

Ukitumia busara kidogo utajiuliza sana.... Yeye katalikiwa lakini hataki mtaliki bali mfiwa...... Unaona hapa kama kuna walakini kidogo.

Masharti yote hayo, mwanamke kutalikiwa ni rahisi sana. Nachelea kusema labda talaka ilitokea sababu ya masharti yake.

Hakuna mahusiano ya masharti yaliyopata kudumu.
Asante. Mimi nimeweka hayo kwa kuwa kwa kipindi nimeshajitahidi kimaisha na yeye pia. Akitokea tutaelewana. Ukiona vigezo vigumu acha.
 
Hapo red... kwa taarifa yako tu, sio kwamba nilikuwa nina mpango wa kujaribu. Mimi ni mme wa mke mmoja wa ndoa takatifu.

Lengo langu ni kujaribu kukusaidia kuweka mambo sawa ili wanaume wenye nia wakuelewe na wasikwazike.

Ila maadam umeona kama nataka kukuwekea mchanga kwenye kitumbua chako, basi nakutaka radhi, na nakuombea kheri katika safari yako ya matumaini.
 
Ahsante kwa ufafanuzi....

Swali dogo la nyongeza..... Huamini kuwa unaweza pata mwenza bila masharti???

Kwenye kigezo cha umri... kwanini awe na miaka 47-50?? Akiwa na miaka 52 au 45 kuna tatizo gani??
Asante. Mwenza ninaweza kumpata ila hayo si mashatti ni vigezo. Hata wewe ukitaka au ulupotaka kuoa au kuolewa ulikuwa na vigezo. Na kwa umri niliyokuwa nao vigezo vitakuwa tofauti na kama ningekuwa binti. Leo hii nina Watoto which are my top priority pia nimejijenga kiasi and for God's sake belongs to my children. Ninamtafuta MTU ambaye kwa miaka yetu tutakuwa na common life including properties. Za sasa alizo nazo ni zake na Watoto wake. Asante again.
 
Hapo red... kwa taarifa yako tu, sio kwamba nilikuwa nina mpango wa kujaribu. Mimi ni mme wa mke mmoja wa ndoa takatifu.

Lengo langu ni kujaribu kukusaidia kuweka mambo sawa ili wanaume wenye nia wakuelewe na wasikwazike.

Ila maadam umeona kama nataka kukuwekea mchanga kwenye kitumbua chako, basi nakutaka radhi, na nakuombea kheri katika safari yako ya matumaini.
Amina. Ubarikiwe na ndoa yako. Mpende sana mkeo. Umetoa ushauri mzuri tu wala hujaharibu. Mungu akupe upendeleo kila iitwayo leo.
 
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 47. Nina watoto watatu. Tulitengana katika ndoa baada ya kutendwa na kutelekezwa na mume. Nilikwazika na kukata tamaa sana ya mahusiano. Nilikaa muda mrefu sana bila mahusiano. Nikajaribu kuruhusu ya aliyejiita mlokole kumbe ilikuwa gear ya kuficha maovu.

Nikaangukia pua kwa mara ya pili na kuamua kuishi tena muda mrefu bila mahusiano. Kwa sasa basi ninahitaji kumpata mwanamume ambaye ana mapenzi ya dhati hasa uaminifu. Sihitaji kuolewa au niseme kuishi na mwanamume tena ila ninataka company tu. Na kupitia kampany nitaweza kujifunza kwa undani kama kweli mwanaume yuko siriazi au la. Ninachohitaji kwa sasa ni upendo wa dhati, nimerudia hapo.

Sitaki wababaishaji wa mahusiano na hapa atakayejitokeza awe mtu wa uhakika ambaye:

- Ni mgani i.e aliyefiwa na mkewe kwa misingi hii kama una baba yako hapa alifiwa na mama niunganishe tu. Au kaka yako ambaye amefiwa na mke niunganishe tu.

- Akubali kupima HIV

- Asiwe mume wa mtu au mwanaume ambaye hajao ila ana wanawake ambao ana connect nao. Hii imenigusa sana baada ya kukutana na mwanaume ambaye alizaa na several women kumbe ni mtu ambaye hana future kabisa kimaisha ya familia. Nilimpenda sana ila changamoto za wanaume kama hawa ni kubwa sana. Ni kujitakia presha.

- Anipe uhuru wa kufanya mambo yangu ya kiuchumi kwa kuwa nina watoto na ninahitaji wasiishi maisha ya tabu . Sitaki kuwa tegemezi hapa. Nimejifunza sana.

- Awe ananithamini mimi kama mpenzi wake na asinilazimishe ndoa mpaka pale nitapona kuwa kweli ni mtu wa kuzeeka naye.

- Awe ni mtu anayejituma katika kuzalisha mali, either ameajiriwa/kujiajiri au anafanya biashara zake.

- Awe ni mtu anayependa familia kwa kuanzia na watoto wake mwenyewe iwe ni priority kwake kabla hajawapenda wanangu mimi.

- Awe tayari kuandikiana pre-nuptial agreement kama itafikia mahali tuamue kuishi pamoja. Ninasema hivi kwa kuwa atakuwa na mali zake na wanawe ambao atataka kuwapa urithi na mimi nina wanangu na chochote kidogo nilichoweza kuhangaikia kwa miaka yangu hivyo sitaki ugomvi wa mali hata kidogo.

-Asiwe Mlevi au Mvuta sigara.

- Awe mkristu. Sibagui ila mimi ni mkristu na wangu pia hivyo itakuwa shida kidogo hapa. Nimekuwa mkweli msinielewe vibaya.

- Awe na miaka kati aya 47-50.

Ninasema sasa kwa mwanaume ambaye anaona anaweza kujaribu kuanzisha mahusiano na mimi karibu PM. Ukiona utatoa lugha mbovu isiyo na staha ninaomba upite taratibu.

Angalizo.
Nipo serious, ninaomba sitaki lugha za matusi ua mitaani mimi ni mtu mzima. Wanaume serious tu na wenye umri niliotaja wani Meseji (PM].

duh kila la kheri utapata kama kweli upo serious ila kuwa makini na makanjanja, ila kwenye umri hapo punguza masharti maana age kwa dunia ya sasa is nothing but numbers. Ungeweka kuanzia 35 hadi 55. Hata dini usibane sana maana unawea kumpata anaekufaa wa dini ingine na akawa tayar kubadilisha na au mkafunga ndoa ya kimila au ya serikalini nadhani flexibility itakusaidia kpanua wigo wa kupata ataekupa faraja uzeeni maana ujana ushatumia tayari kwa sasa unatafuta wa kukupa faraja uzeeni
 
Amina. Ubarikiwe na ndoa yako. Mpende sana mkeo. Umetoa ushauri mzuri tu wala hujaharibu. Mungu akupe upendeleo kila iitwayo leo.
Ahsante na kila la kheri...

Nlipenda kukushauri umwombe Mungu akuangazie heri katika hitaji lako lakini nachelea....... au labda ungenifafanulia kwenye hii sentensi hapa chini, isije ikawa nimeielewa vibaya...

- Awe ananithamini mimi kama mpenzi wake na asinilazimishe ndoa mpaka pale nitapona kuwa kweli ni mtu wa kuzeeka naye.
 
duh kila la kheri utapata kama kweli upo serious ila kuwa makini na makanjanja, ila kwenye umri hapo punguza masharti maana age kwa dunia ya sasa is nothing but numbers. Ungeweka kuanzia 35 hadi 55. Hata dini usibane sana maana unawea kumpata anaekufaa wa dini ingine na akawa tayar kubadilisha na au mkafunga ndoa ya kimila au ya serikalini nadhani flexibility itakusaidia kpanua wigo wa kupata ataekupa faraja uzeeni maana ujana ushatumia tayari kwa sasa unatafuta wa kukupa faraja uzeeni
Asante sana. Umri ni lazima kuanzia 47 -50. Asprin ameshauri hata 52 it is fine. Chini ya 47 hapana. Dini kitabaki kuwa kigezo.
 
Ahsante na kila la kheri...

Nlipenda kukushauri umwombe Mungu akuangazie heri katika hitaji lako lakini nachelea....... au labda ungenifafanulia kwenye hii sentensi hapa chini, isije ikawa nimeielewa vibaya...

- Awe ananithamini mimi kama mpenzi wake na asinilazimishe ndoa mpaka pale nitapona kuwa kweli ni mtu wa kuzeeka naye.
Asante. Sutakimbilia kuwekana pingu kabisa. Ninahitaji company turidhie wote baadaye kuishi kwa moyo safi. Swala lako umri 45-52 kwa 52 sawa ila 45 hapana. Anyway. Let's leave it to our Mighty God.
 
Wakati mkisubiri kupimana kabla hamjafungana pingu za maisha.... itaruhusiwa kuisigina katiba kwenye kifungu cha sita cha amri za Mungu??
 
Watu wengine huwa wanakosa wapenz wazuri sio kwa bahati mbaya ila ni kwasababu ya misimamo miingi kama hii yako ambayo kwa kiasi kikubwa umetawaliwa na umimi (ubinafsi). Hivi ni mtu gani anayejitambua utamwambia nataka ufate hiki, kile mara usiniingilie kwenye hiki na kile halafu naye akubali tu na kunywea kama vile sio binadamu mwenye hisia na mapendeleo?
Nakushauri tu, mahusiano yoyote (hata yasiyo ya kimapenzi) it's about compromise of what you believe kwa kiasi flani. Usipolikubali hilo utaendelea kuwa mpweke milele au kupata kampani za watu wenye malengo ya muda mfupi kama hao uliotangulia kuwa nao.
Asante. Kwa umri huu musimamo au vigezo vitakuwa tofauti na mwenye miaka 20-30, 335-40, 45-50. Pia mwisho wa siku huwezi kupata 100% ila kuna btn 70-100%.
 
Wakati mkisubiri kupimana kabla hamjafungana pingu za maisha.... itaruhusiwa kuisigina katiba kwenye kifungu cha sita cha amri za Mungu??
Hahaha Asprin acha utani wako. Nimpate kwanza tutaamua.
 
Hapo red... kwa taarifa yako tu, sio kwamba nilikuwa nina mpango wa kujaribu. Mimi ni mme wa mke mmoja wa ndoa takatifu.

Lengo langu ni kujaribu kukusaidia kuweka mambo sawa ili wanaume wenye nia wakuelewe na wasikwazike.

Ila maadam umeona kama nataka kukuwekea mchanga kwenye kitumbua chako, basi nakutaka radhi, na nakuombea kheri katika safari yako ya matumaini.
Wewe hujamgundua huyu mama?ni wale wamebutuliwa kwenye mapenzi tena kwa kutafuta ugomvi wao wenyewe then huachwa na kuishia hasira na gadhabu ndo wanapotea kabisaaaa! Mi nilishakua na mtu wa hvyo na nilijuta mpaka leo,hua wanakuja kama wema na anza kua nae uone moto wake,wanakua wameharibu toka enzi za usichana ila hua hawakubali kua waliharibu,ukiwauliza hua wanashutumu na kusema yani wanaume hawa!!! Sitakuja kumuamini mwanaume tena maishani,hujakutana na wa hvyo???ndo hawa sasa
 
Doh!.... Aisee...!😱
 
Back
Top Bottom