Ninapokumbuka ya Morgan I Tsvangirai nahuzunishwa na ya Upinzani wa kina Lissu na wenzake

Kwa bahati mbaya sikuwepo nchini, ningekuwa mbele kabisa. Sina woga wala hofu ya risasi kupigania demokrasia
Lissu alisema kweli hatujawa tayari mkuu hata hao wazimbabwe kabla hawakuwaza mfumo wa Mugabe kwamba ni mbaya ila njaa ipokaza mixer vikwazo akili zipo sawa so ujasiri unaotaka kwa Lissu utakuja njaa ikitukaba vizuri akili zikawa tayari then atarudi kuwa mbele ya mapambano
 
Lissu hashindani na risasi, anashindana kuikomboa nchi toka kwa watawala wasiojali utu wa Mtanzania, wasiojua kufuata sheria za nchi, hivyo kuendelea kukaa Tanzania asubiri kifo nao ungekuwa ni ujinga, kukimbia sio ujinga ukiwa vitani, nayo ni mbinu ya kivita.

Wapo wanasiasa wengi waliozikimbia nchi zao wakiwa kwenye harakati za mapambano na bado dunia inawatambua kwa uimara wao mpaka leo, hivyo Lissu sio wa kwanza kutafuta hifadhi nje kwa ajili ya usalama wake.

Labda nikuulize ewe mpenda mabadiliko, siku ya maandamano ulijitokeza barabarani au uliogopa virungu vya Mambosasa? Ni upi mchango wako kwenye kuikomboa demokrasia ya nchi yetu? kuna msemo usemao; "changes begins with you"

Nikushauri badala ya kumlaumu Lissu, anza na wewe kuwa chachu ya hayo mabadiliko unayoyataka, sio unalala nyumbani unasubiri uletewe mabadiliko ukiwa kitandani.
Lema hayuko Kenya, labda kama kuna kopi yake.

Wewe in mmoja wa wale ambao hawakunutia Lissu kupigwa risasi ndiyo mliidai kwanini hakufa kama zilikuwa risasi kweli! Na bado unaendelea kuamini Lissu aliigiza!

Hii nchi si yako jaribu kuwa makini na ukisemacho kwani hao unaowashabikia kwa kejeri hawatakulinda asilani.
 
Nawasalimu wanabodi wa JamiiForums

Usiku wa kuamkia leo akili yangu ilinigomea kupata usingizi na hivyo kukaa macho almost the whole night. Nilikuwa nikimkumbuka mtu jasiri na mpambanaji wa kutetea haki za binadamu na ustawi wa demokrasia nchini Zimbabwe.

Alikuwa ni mtu aliyejitolea maisha yake ili hatimaye wengine waje kuishi maisha ya raha na amani hata kama yeye hatokuwepo duniani. Namzungumzia Morgan Tsvangirai wa chama cha Movement for Democratic Change, MDC aliyefariki Afrika Kusini miaka mitatu iliyopita kwa ugonjwa wa saratani ya utumbo.

Morgan alikuwa ni mwiba mkali mbele ya macho ya dikteta Robert Mugabe tangu akiwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi hadi alipoanzisha MDC kuendeleza mapambano dhidi ya utawala wa kifashisti ya ZANU-PF ya Mugabe iliyojaa dhulma, ufisadi, kujuana, utekaji, utesaji kwa waliomkosoa dikteta Mugabe na ushetani mwingine kama ilivyo kwa Serikali ya CCM.

Upambanaji wa Morgan kwa utawala wa ZANU-PF ya dikteta Mugabe umesheheni simulizi za kusisimua sana. Kwamba hata alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu kama hatua ya kumtaka "astaafu" upambanaji bado hakukubali kusaliti wazalendo. Morgan hakuwa mwoga na kamwe hakushikwa na hofu ya kuuawa na Mugabe. Na hiyo ilimfanya asikimbie nchi yake kwenda Uropa. Alikuwa tayari kufa nchini Zimbabwe kuwapigania wananchi waliokuwa wakionewa na Serikali katili ya Mugabe.

Baada ya Mugabe kuvifungia magazeti yaliyokosoa Serikali yake, aliviamuru yaliyosalia kumtangaza Morgan kama kibaraka wa wazungu asiye na nia njema na Zimbabwe lakini bado Tsvangirai hakukata tamaa.

Sina kumbukumbu ni mara ngapi Morgan alilazwa rumande na kupigwa na Wana usalama vibaraka wa Mugabe maana picha za Morgan zikimuonesha akichuruzika damu zimetapakaa katika maktaba mbalimbali duniani.

Mugabe alijaribu hata kumhonga vyeo na pengine ofa ya vyeo na fursa za biashara lakini dunia imeandika historia kuwa alivikataa kuwapambania Wazimbabwe.

Ukweli uliokodoa macho ni kwamba mchango wa Morgan ni mkubwa sana katika kumwondoa Mugabe madarakani. Ndiyo, maana jiulize wale makamanda wa Mugabe walipata wapi ujasiri wa kumwambia "bosi" wao aondoke ofisini? Wale vijana wa "UVCCM" wa Zanu-Pf walipata wapi ujasiri wa kuunga mkono maandamano ya kumng'oa dikteta Mugabe madarakani? Ukweli ni mbegu ya ujasiri alioupanda Morgan kwa wananchi wa Zimbabwe.

Hata Rais Mnangagwa aliingiwa na woga hivyo kukimbilia ughaibuni baada ya kubaini kukamilika kwa mpango wa kumuua uliopangwa na mke wa Mugabe, Grace lakini Morgan alisalia Zimbabwe kupanda mbegu ya ujasiri na akafanikiwa.

Nikikumbuka haya ya Morgan nasononeshwa na hali ya Upinzani Tanzania. Tundu Lissu amenukuliwa akisema, "Watanzania hawajawa tayari kwa mabadiliko kukiondoa CCM madarakani". Najiuliza ni lini Lissu amepanda mbegu ya ujasiri wa kukiondoa CCM ya Magufuli madarakani? Ni lini Lissu amepanda mbegu hiyo kwa vyombo vya usalama vinavyokilinda CCM madarakani? Kwa nini Lissu aliahidi kutupeleka barabarani akaishia kujipeleka ubalozini kwa woga na hofu ya kuuawa na vyombo vya usalama alivyodai?

Unajiuliza hivi Tanzania nani hasa ni kinara na alama ya Upinzani aliyetayari "kufa" kwa ajili ya umma mpana. Kenya wanaye Raila Odinga, Uganda wanaye Kiiza Besigye na Bobi Wine, Afrika Kusini wanaye Julius Malema nakadhalika. Tanzania tunaye nani? Mdee, Sugu, Lema, Heche, Mbowe, Zitto, Membe, Rungwe, au nani?

Kwa mbali alionekana Lissu angechukua nafasi hiyo lakini naye amejawa hofu na woga kana kwamba katika Afrika demokrasia, haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza, Katiba bora nakadhalika ni Mambo ya kuletwa na watawala kama bakuli la dengu mezani.

Wanajisahaulisha kuwa Mambo hayo hupiganiwa katika majukwaa ya siasa bila kujali maslahi binafsi na matumbo. Ni vita inayogharimu damu, jasho na mateso. Morgan hakufikiri wala kusubiri kuwa mageuzi yangeletwa na dikteta Mugabe. Alipambana. Hakuogopa "kushughulikiwa" kama wapinzani wetu.

Wakati Lema akitimkia Kenya na familia yake akidai nayo inaweza kuumizwa, Morgan aliwahi kuchomewa nyumba na kila kitu ndani lakini alipopata nafasi ya kuongea na media akisema, "nimepoteza kila kitu ndani ya nyumba lakini sijapoteza chochote kwa Wazimbabwe maana ukombozi uko mlangoni."

Leo Wazimbabwe wanafurahia maisha yasiyo na vituko vya Mugabe na mkewe Grace lakini jasiri Morgan ametangulia kaburini. Huo ndio Upinzani wa kweli. Kupanda mbegu ya ujasiri si lelemama. Linahitaji kujitoa mhanga si kukimbia. Tumebaki na wapinzani wa mitandaoni. Inasononesha sana!!!

Nawatakia mapumziko mema.
Umeandika vizuri sana mkuu, swali wewe una miaka zaidi ya 18 kwanini wewe usiwe mfano kwa kuanzisha chama chako au kujiunga na CUF, ACT ukawa mfano kwa kutupigania kwa nguvu zako zote ukawa tayari kufa?
 
Kwa asilimia kubwa naweza kusema Mh Lissu yupo sahihi kabisa, sisi waTz hatujawa tayari kabisa.

Mfano mzuri ukiangalia majirani zetu waganda wapo tayari kwa lolote tofauti kabisa na sisi.
Kule wamekufa zaidi ya watu 50 lakini bado wapo imara sisi tunaongea tu huku tumejificha
 
Kwa asilimia kubwa naweza kusema Mh Lissu yupo sahihi kabisa, sisi waTz hatujawa tayari kabisa.

Mfano mzuri ukiangalia majirani zetu waganda wapo tayari kwa lolote tofauti kabisa na sisi.
Muwe teyari vp na wakati hadi sasa bado kuna watu wanakipenda chama tawala,upinzani una nguvu mitandaoni tu Kwa hichi walichokifanya ccm katika uchaguzi wa mwaka huu kama kungekuwa na upinzani kweli wenye nguvu huku uraiani basi kusingekalika ila angalia baada ya matokeo ya uchaguzi watu walikuwa wako busy na shughuli zao utafikiri walikuwa wanasubiri uchaguzi uishe waendelee na kazi zao.
 
Najiuliza ni lini Lissu amepanda mbegu ya ujasiri wa kukiondoa CCM ya Magufuli madarakani?
 
Nawasalimu wanabodi wa JamiiForums

Usiku wa kuamkia leo akili yangu ilinigomea kupata usingizi na hivyo kukaa macho almost the whole night. Nilikuwa nikimkumbuka mtu jasiri na mpambanaji wa kutetea haki za binadamu na ustawi wa demokrasia nchini Zimbabwe.

Alikuwa ni mtu aliyejitolea maisha yake ili hatimaye wengine waje kuishi maisha ya raha na amani hata kama yeye hatokuwepo duniani. Namzungumzia Morgan Tsvangirai wa chama cha Movement for Democratic Change, MDC aliyefariki Afrika Kusini miaka mitatu iliyopita kwa ugonjwa wa saratani ya utumbo.

Morgan alikuwa ni mwiba mkali mbele ya macho ya dikteta Robert Mugabe tangu akiwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi hadi alipoanzisha MDC kuendeleza mapambano dhidi ya utawala wa kifashisti ya ZANU-PF ya Mugabe iliyojaa dhulma, ufisadi, kujuana, utekaji, utesaji kwa waliomkosoa dikteta Mugabe na ushetani mwingine kama ilivyo kwa Serikali ya CCM.

Upambanaji wa Morgan kwa utawala wa ZANU-PF ya dikteta Mugabe umesheheni simulizi za kusisimua sana. Kwamba hata alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu kama hatua ya kumtaka "astaafu" upambanaji bado hakukubali kusaliti wazalendo. Morgan hakuwa mwoga na kamwe hakushikwa na hofu ya kuuawa na Mugabe. Na hiyo ilimfanya asikimbie nchi yake kwenda Uropa. Alikuwa tayari kufa nchini Zimbabwe kuwapigania wananchi waliokuwa wakionewa na Serikali katili ya Mugabe.

Baada ya Mugabe kuvifungia magazeti yaliyokosoa Serikali yake, aliviamuru yaliyosalia kumtangaza Morgan kama kibaraka wa wazungu asiye na nia njema na Zimbabwe lakini bado Tsvangirai hakukata tamaa.

Sina kumbukumbu ni mara ngapi Morgan alilazwa rumande na kupigwa na Wana usalama vibaraka wa Mugabe maana picha za Morgan zikimuonesha akichuruzika damu zimetapakaa katika maktaba mbalimbali duniani.

Mugabe alijaribu hata kumhonga vyeo na pengine ofa ya vyeo na fursa za biashara lakini dunia imeandika historia kuwa alivikataa kuwapambania Wazimbabwe.

Ukweli uliokodoa macho ni kwamba mchango wa Morgan ni mkubwa sana katika kumwondoa Mugabe madarakani. Ndiyo, maana jiulize wale makamanda wa Mugabe walipata wapi ujasiri wa kumwambia "bosi" wao aondoke ofisini? Wale vijana wa "UVCCM" wa Zanu-Pf walipata wapi ujasiri wa kuunga mkono maandamano ya kumng'oa dikteta Mugabe madarakani? Ukweli ni mbegu ya ujasiri alioupanda Morgan kwa wananchi wa Zimbabwe.

Hata Rais Mnangagwa aliingiwa na woga hivyo kukimbilia ughaibuni baada ya kubaini kukamilika kwa mpango wa kumuua uliopangwa na mke wa Mugabe, Grace lakini Morgan alisalia Zimbabwe kupanda mbegu ya ujasiri na akafanikiwa.

Nikikumbuka haya ya Morgan nasononeshwa na hali ya Upinzani Tanzania. Tundu Lissu amenukuliwa akisema, "Watanzania hawajawa tayari kwa mabadiliko kukiondoa CCM madarakani". Najiuliza ni lini Lissu amepanda mbegu ya ujasiri wa kukiondoa CCM ya Magufuli madarakani? Ni lini Lissu amepanda mbegu hiyo kwa vyombo vya usalama vinavyokilinda CCM madarakani? Kwa nini Lissu aliahidi kutupeleka barabarani akaishia kujipeleka ubalozini kwa woga na hofu ya kuuawa na vyombo vya usalama alivyodai?

Unajiuliza hivi Tanzania nani hasa ni kinara na alama ya Upinzani aliyetayari "kufa" kwa ajili ya umma mpana. Kenya wanaye Raila Odinga, Uganda wanaye Kiiza Besigye na Bobi Wine, Afrika Kusini wanaye Julius Malema nakadhalika. Tanzania tunaye nani? Mdee, Sugu, Lema, Heche, Mbowe, Zitto, Membe, Rungwe, au nani?

Kwa mbali alionekana Lissu angechukua nafasi hiyo lakini naye amejawa hofu na woga kana kwamba katika Afrika demokrasia, haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza, Katiba bora nakadhalika ni Mambo ya kuletwa na watawala kama bakuli la dengu mezani.

Wanajisahaulisha kuwa Mambo hayo hupiganiwa katika majukwaa ya siasa bila kujali maslahi binafsi na matumbo. Ni vita inayogharimu damu, jasho na mateso. Morgan hakufikiri wala kusubiri kuwa mageuzi yangeletwa na dikteta Mugabe. Alipambana. Hakuogopa "kushughulikiwa" kama wapinzani wetu.

Wakati Lema akitimkia Kenya na familia yake akidai nayo inaweza kuumizwa, Morgan aliwahi kuchomewa nyumba na kila kitu ndani lakini alipopata nafasi ya kuongea na media akisema, "nimepoteza kila kitu ndani ya nyumba lakini sijapoteza chochote kwa Wazimbabwe maana ukombozi uko mlangoni."

Leo Wazimbabwe wanafurahia maisha yasiyo na vituko vya Mugabe na mkewe Grace lakini jasiri Morgan ametangulia kaburini. Huo ndio Upinzani wa kweli. Kupanda mbegu ya ujasiri si lelemama. Linahitaji kujitoa mhanga si kukimbia. Tumebaki na wapinzani wa mitandaoni. Inasononesha sana!!!

Nawatakia mapumziko mema.
Kwani lazima awe Lissu, uwe wewe kama hao uliowataja.
 
Bongo tunamambo ya Ajabu, kama unamwona Lissu siyo Mpinzani wa kweli, kuwa wewe Mpinzani wa kweli!! Kwani lazima awe Lissu Tu!!
 
Lissu hashindani na risasi, anashindana kuikomboa nchi toka kwa watawala wasiojali utu wa Mtanzania, wasiojua kufuata sheria za nchi, hivyo kuendelea kukaa Tanzania asubiri kifo nao ungekuwa ni ujinga, kukimbia sio ujinga ukiwa vitani, nayo ni mbinu ya kivita.

Wapo wanasiasa wengi waliozikimbia nchi zao wakiwa kwenye harakati za mapambano na bado dunia inawatambua kwa uimara wao mpaka leo, hivyo Lissu sio wa kwanza kutafuta hifadhi nje kwa ajili ya usalama wake.

Labda nikuulize ewe mpenda mabadiliko, siku ya maandamano ulijitokeza barabarani au uliogopa virungu vya Mambosasa? Ni upi mchango wako kwenye kuikomboa demokrasia ya nchi yetu? kuna msemo usemao; "changes begins with you"

Nikushauri badala ya kumlaumu Lissu, anza na wewe kuwa chachu ya hayo mabadiliko unayoyataka, sio unalala nyumbani unasubiri uletewe mabadiliko ukiwa kitandani.
Umewahi kuona morgan anahudumiwa na mzungu kama lisu?

Kuna picha ya Lisu ilizunguka anahudumiwa na beberu limemuwekea mishikaki na mvinyo anajimwambafai huko ugaibuni.

Kwa hiyo Tundu ni mtumbuaji tu na lengo lake ni kupata huduma ya kuwa bwanyeye na sio kutumika kwa ajiri ya watanzania.

Na siku angepata uraisi angebebwa kama wafalme wa zamani.
 
Usimlinganishe Morgan na wapumbavu vibaraka wa kutupwa.

Morgan hakuwahi kuwatisha Wazimbabwe wasidai haki za rasilimali zao kuwa eti watashitakiwa MIGA.

Sent from my Infinix X622 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom