Ninapenda uandishi lakini sijui nianzie wapi

Kalamu Nzito

JF-Expert Member
Aug 13, 2015
318
662
Habari wana JF
Mimi ni jobless wa muda mrefu kidogo. Lakini ninapenda sana kuandika tangu utotoni. Wakati nipo shule nilikua nikiandika simulizi za kutunga na wanafunzi wenzangu walikua wakizipenda.

Mwaka 2020 nilishiriki shindano la uandishi “WAKINI KURIA AWARDS” na niliibuka mshindi wa kwanza Afrika katika kipengele cha Literature for Children ambapo nilishinda dollar 100.

Toka hapo nimeshindwa kujua ni namna gani nijiendeleze katika fani hii. Nimewaza kuandika vitabu lakini watanzania sio wasomaji sana. Na mimi kiu yangu ni kwamba katika fani hii, pia niweze kujikwamua kiuchumi.

Nifanye nini niweze kujikwamua katika hili?
 
Tuna tatizo kubwa sana la kutokujiona na tukijiona hatuamini tulichoona, ulochoandika kinaonesha ulichokosa ni nia thabiti ya kuifuta ndoto yako na siyo kwamba hujui namna ya kufanya na ukifanyeje. Eneo hili ndipo tunapopotelea wengi...we find what was already found.
Follow your heart Mkuu. You have already allerted.
 
Tuna tatizo kubwa sana la kutokujiona na tukijiona hatuamini tulichoona, ulochoandika linaloonesha ulichokosa ni nia thabiti ya kuifuta ndoto yako na siyo kwamba hujui namna ya kufanya na ukifanyeje.
Follow your heart Mkuu. You have already allerted.

Amen mkuu
 
Uanzie wapi ? Kaanzie chuoni
Mahali sahihi pa kuanzia ni msukumo uliopo ndani yake " ni yeye mwenyewe na tayari ameshaanza" chuo siyo sehemu ya kuanzia ila ni sehemu sahihi yakuboresha kilichoanza..to sharpen, enhance knowledge.

We start from our inner being Mkuu,
 
Back
Top Bottom