Ninaomba nijibiwe, Waziri Mbarawa anao uhalali wa kushiriki maamuzi yanayoihusu bandari? (Kisheria)

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
8,098
9,994
Nimefuatilia mjadala ulioandaliwa na serikali leo.

Msemaji mmoja mwenye mlengo wa kiserikali alisema na naomba nimnukuu

"Kasomeni katiba masuala ya viwanda na uwekezaji sio miongoni mwa mambo ya muungano" mwisho wa kumnukuu.

Kauli hii inaonyesha dhahili ilivyo ngumu kwa mmatumbi kutoka Tanzania bara kushiriki iwe kwa mawazo au kwa vitendo katika masuala ya uwekezaji huko visiwani zanzibar (haiwezekaniki)

Hii ni kwakuwa wazanzibari wameweka usimamizi mzuri kwenye mambo yasiyo ya muungano.

Je, inakuweje kwa upande wetu

Mzanzibari akawa kinara kwenye maamuzi ya mambo yasiyo ya muungano?

Je, hili ni jambo lisilo na ulakini mbele ya sheria?
 
Yes, ni halali kabisa na anao uwezo wote!.
Kwenye issues za uraia kuna ujinga mwingi na wajinga wengi ambao ni kwa ujinga tuu, hawajui kuwa Tanzania ni nchi moja ya JMT, yenye uraia mmoja tuu, uraia wa JMT. Kwenye uraia, hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari, kuna Mtanzania tuu, na kila Mtanzania ana haki zote za Utanzania.

Namna pekee ya kuondoa ujinga huu ni elimu ya uraia.
p
 
Kwani Profesa Mbarawa ni waziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Mambo ya muungano au si ya muungano hayana uhusiano na uasili wa nani aliyepewa majukumu ya kikatiba katika kuyasimamia. Leo tuna raisi wa JMT amabye asili yake ni mzanzibari na tuna raisi wa Zanzibar ambaye asili yake ni Tanzania bara (Tanganyika).
 
Naona walipokuwa wanatunga sheria wengine walikuwa wamelala na wengine walikuwa hawajui lolote na wengine walikuwa wamezubaa tu hawajui waanzie wapi

Akili za binadamu zinatofautiana na wanyama ila kuna wengine bora paka
 
Kwani Profesa Mbarawa ni waziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Mambo ya muungano au si ya muungano hayana uhusiano na uasili wa nani aliyepewa majukumu ya kikatiba katika kuyasimamia. Leo tuna raisi wa JMT amabye asili yake ni mzanzibari na tuna raisi wa Zanzibar ambaye asili yake ni Tanzania bara (Tanganyika).
Hujanielewa. Jambo ambalo sio la kimuungano mfano ardhi unamuweka waziri mzanzibari kweli? Hilo linawezekana wakati scope of operations itakuwa ni Tanzania bara?
 
Tatizo ni mfumo wenyewe wa Muungano hauna tafsiri ya kueleweka kuhusu lipi ni la Muungano na lipi silo hata Nyerere alishawahi kumuweka Salim Ahmed kuwa Waziri mkuu wakati waziri Mkuu mamlaka yake mwisho ni Chumbe
 
Nimefuatilia mjadala ulioandaliwa na serikali leo.

Msemaji mmoja mwenye mlengo wa kiserikali alisema na naomba nimnukuu

"Kasomeni katiba masuala ya viwanda na uwekezaji sio miongoni mwa mambo ya muungano" mwisho wa kumnukuu.

Kauli hii inaonyesha dhahili ilivyo ngumu kwa mmatumbi kutoka Tanzania bara kushiriki iwe kwa mawazo au kwa vitendo katika masuala ya uwekezaji huko visiwani zanzibar (haiwezekaniki)

Hii ni kwakuwa wazanzibari wameweka usimamizi mzuri kwenye mambo yasiyo ya muungano.

Je, inakuweje kwa upande wetu

Mzanzibari akawa kinara kwenye maamuzi ya mambo yasiyo ya muungano?

Je, hili ni jambo lisilo na ulakini mbele ya sheria?
Sikiliza Press Leo.
 
Yes, ni halali kabisa na anao uwezo wote!.
Kwenye issues za uraia kuna ujinga mwingi na wajinga wengi ambao ni kwa ujinga tuu, hawajui kuwa Tanzania ni nchi moja ya JMT, yenye uraia mmoja tuu, uraia wa JMT. Kwenye uraia, hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari, kuna Mtanzania tuu, na kila Mtanzania ana haki zote za Utanzania.

Namna pekee ya kuondoa ujinga huu ni elimu ya uraia.
p
Kwa hiyo wanzanzibar Wana uraia pacha au nini maana wao wanaweza kupiga kura zanzibar na Tanganyika. Lakini mtanganyika hawezi huko Zenj, je hii inaitaje?
 
Nimefuatilia mjadala ulioandaliwa na serikali leo.

Msemaji mmoja mwenye mlengo wa kiserikali alisema na naomba nimnukuu

"Kasomeni katiba masuala ya viwanda na uwekezaji sio miongoni mwa mambo ya muungano" mwisho wa kumnukuu.

Kauli hii inaonyesha dhahili ilivyo ngumu kwa mmatumbi kutoka Tanzania bara kushiriki iwe kwa mawazo au kwa vitendo katika masuala ya uwekezaji huko visiwani zanzibar (haiwezekaniki)

Hii ni kwakuwa wazanzibari wameweka usimamizi mzuri kwenye mambo yasiyo ya muungano.

Je, inakuweje kwa upande wetu

Mzanzibari akawa kinara kwenye maamuzi ya mambo yasiyo ya muungano?

Je, hili ni jambo lisilo na ulakini mbele ya sheria?
Anayo mia kwa mia.
 
Hata Samia urais wake unapaswa ukatafutiwe uhalali mahakamani. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampasa awe anatokea upande wa bara, kwani Zanzibar tayari wanaye Rais. Isipofanyika hivyo, kuna hatari kubwa ya maslahi ya Tanganyika kuhujumiwa.

Kwa mfano aje atokee Rais dikteta mwenye asili ya visiwani.. akiamua kuugawa mkoa wa Dar es Salaam kuwa sehemu ya Zanzibar ni nani atamzuia?

Tunaposoma katiba tujaribu kuangalia na yale mambo ambayo hayakuandikwa lakini yanaonekana kwa uwazi by implication.
 
Suruhisho ni kua na serikali tatu ili Kila mmoja awe na maamuzi kwenye Mali zake, sio kama hivi ambavyo anaweza akatoka mtu kule akaja huku akafanya upuuzi wake kwa kigezo cha muungano, kama haiwezekani basi huo muungano uvunjike tuu, kwa sababu ulikua ni muungano wa Nyerere na karume
 
Jibu ni ndiyo

As long as such investment inafanyika ndani ya wizara yake

Mfano labda ingekuwa ajabu angeshiriki waziri wa maji......coz sio eneo lake
 
Yes, ni halali kabisa na anao uwezo wote!.
Kwenye issues za uraia kuna ujinga mwingi na wajinga wengi ambao ni kwa ujinga tuu, hawajui kuwa Tanzania ni nchi moja ya JMT, yenye uraia mmoja tuu, uraia wa JMT. Kwenye uraia, hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari, kuna Mtanzania tuu, na kila Mtanzania ana haki zote za Utanzania.

Namna pekee ya kuondoa ujinga huu ni elimu ya uraia.
p

Acha kudanganya
Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania upande wa Tanganyika haruhusiwi kupiga kura ya Rais wa Zanzibar.
Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania upande wa Tanganyika haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar
Sio kweli kwamba Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana haki sawa pande zote.
Hivi unajua Kwa nini kwenye articles of association ya Muungano kulikuwa na mambo ya specifically ya Muungano tu ?
Si sawa Kwa Mzanzibar kushiriki kwenye suala ambalo sio la Muungano hata kule bungeni wabunge wangekuwa wanachangia kwenye mambo yao makhususi tu kama ni suala la Muungano wajadili wote na kama suala sio la Muungano kila upande ujadili kivyake wasiohusika watolewe
 
Ni Upumbavu kabisa kuamini mzanaki ni Mtanzania zaidi kuliko mpemba..-Julius Nyerere
Ujinga ni kutokujua, ignorance na mjinga ni asiyejua, yaani ni ignorant. Mjinga akifundishwa na kufundishika, ujinga unamtoka, anakuwa sio mjinga tena unakuwa mwerevu, unaerevuka.

Mjinga hata baada ya kufundishwa, na bado akawa ni mjinga, huyo ni mpumbavu!, foolish!. Mpumbavu ni mjinga asiyefundishika!.

Tuko wana jf kibao humu tumeamua kuwa waalimu wa kujitolea kufundisha wengine ili kuwatoa ujinga, ili wajinga hao, waerevuke. Wako wanaofundishika hivyo ujinga unawatoka, na wapo wasiofundishika hata uwafundishe vipi, ujinga wao hauwatoki, hao ni Wapumbavu!, fools!.

It's very unfortunately Watanzania wengi zaidi ni ignorants and fools kuliko walioerevuka!, na hii ni moja ya sababu ya kwanini CCM utaendelea kutawala Tanzania kwa miaka mingi. Mimi niliweka projections za mpaka 2030 Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika! lakini kama sasa tunaelkea 2025 na ujinga bado ni wa kiwango hiki, then hata hiyo 2030, I doubt!.
P
 
Acha kudanganya
Ujinga ni kutokujua!, na mjinga ni asiyejua!.
Dawa ya ujinga ni elimu, kufundishwa, kujua na kuerevuka!. Mjinga akifundishwa ujinga unamtoka, anaerevuka. Mjinga akifundishwa asipofundishika huyo ni mpumbavu!.
Mwalimu wa kujitolea wa somo la uraia, anapojitolea kufundisha kuhusu uraia wa Tanzania, ni uraia mmoja tuu. Hakuna uraia wa Tanzania Bara wala uraia wa Zanzibar, bali Zanzibar kuna ukaazi na sio uraia. Zanzibar hakuna uraia kwasababu Zanzibar sio nchi, Zanzibar ni sehemu ya JMT.
Kama mtu alikuwa hajui hili, amefundishwa anaona anadanganywa... , tumuiteje?.
P
 
Back
Top Bottom