Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,060
Nchi yetu ina bahati mbaya sana kwa kuwakosa viongozi ambao wana uelewa mpana, wanaoyajua mamlaka yao, wanaoelewa vizuri wajibu wao, wanaoelewa vizuri mamlaka yao yanapoishia, na hasa kwa ujumla, viongozi wanaozielewa vizuri sheria zetu na katiba yetu.
Mkataba wa hovyo wa bandari umetufanya tuwafahamu vizuri viongozi wetu ni watu wa namna gani, na zaidi kufahamu dhamira zao, na uduni wa uelewa wao katika masuala mazito ya kitaifa.
Rais hajatamka lolote mpaka sasa, tunamlaumu kwa kusaini mkataba wa hovyo kabisa usiolinda mamlaka ya nchi, uhuru wetu na wa Taifa letu, na kushindwa kufuata taratibu za mikataba. Mikataba ya uwekezaji huwa haisainiwi na Rais wa nchi, lakini kwenye hili la DP, ambayo ni kampuni, amesaini Rais wetu. Kwenye mkataba wa biashara, pande mbili zinazosaini mkataba huwa zenye nafasi sawa. Kwa hiyo Rais wa nchi yetu amejishusha na kuwa sawa na wawakilishi wa kampuni ya DP. Mkataba kwa upande wetu una sahihi ya Rais Samia, kwa upande wa pili hakuna sahihi ya Rais/kiongozi mkuu wa UAE. Rais amidhalilisha nchi.
Makamu wa Rais Dr. Mpango, kwenye hili kaamua kukaa kimya, na kwenye process nzima amejikalia kimya. Lakini kukaa kimya ni automatic submission. Kwa hiyo hapa, inamaanisha Makamu wa Rais amebariki.
Waziri Mkuu, Majaliwa Majaliwa, ambaye ana historia ya kutokuwa mkweli (wakati watu walipokuwa wanahoji kuwa Hayati Magufuli kwa nini hajaonekana kwa muda mrefu, huku kukiwa na tetesi kuwa anaumwa sana, na wengine wakisema amekwishafariki, Majaliwa alijibu kwa kufoka kuwa Rais Magufuli haonekani, wanaouliza walitaka wamwone wapi? Wamwone Kariaokoo sokoni? Akaeleza kuwa Rais Magufuli ni mzima kabisa, yupo ikulu anachapa kazi, wakati tayari Hayati Magufuli alikuwa amekwishafariki), yeye amejitokeza hadharani kuutetea mkataba huo wa hovyo. Ukiutazama mkataba wenyewe, na maneno anayoyatamka Majaliwa, ambayo hayamo kwenye mkataba, unaona wazi kuwa anaendelea na ile historia yake, kama alivyofanya kwenye taarifa kuhusiana na kifo cha Rais Magufuli. Majaliwa, mwishoni anasema kuwa eti wao viongozi wamesikia hofu za wananchi, lakini wananchi wawaamini vjongozi wao. Yaani wananchi wawaamini viongozi ambao wana historia ya kusema uwongo. Yaani wanaanchi waamini porojo za viongozi wakati wakati mkataba wenyewe upo wazi, na wananchi wana uwezo wa kuusoma, na kuuchambua, na tena baadhi ya wananchi hawa wana uelewa mkubwa maradufu ya viongozi wanaotaka waaminiwe wakati hawaaminiki.
Maswali muhimu kuhusiana na mambo ya hovyo yaliyopo kwenye mkataba ule wa hovyo, Majaliwa hajajibu hata moja, halafu anataka watu wamwini! Sisi wananchi hatujawa wajinga wa kiwango hicho.
Majaliwa anatakiwa ajibu kwa hoja, huku akifanya rejea kwenye mkataba wenyewe:
1) Kwa nini mkataba huu wa hovyo kwa upande wetu umesainiwa na Rais na kwa kwa upande wa pili haujasainiwa na mkuu wa nchi, bali kampuni?
2) IGA huwa kati ya nchi na nchi, je DP ni nchi?
3) Kama DP siyo nchi, na kama ni kampuni, zabuni ya kumtafuta mwendeshaji ilifuata taratibu na sheria za nchi, au haikufuatwa? Kwa nini?
4) IGA iliyosainiwa ndiyo Master agreement, yaani mkataba mama na mkataba kiongozi, na una nguvu ya kisheria, na hairuhusiwi kuuvunja mpaka DP waridhie, analifahamu hilo?
5) Aeleze, kwa kadiri ya IGA, kuna HGA itakayokuwa na uwezo wa kuikiuka IGA? Na hilo limeandikwa wapi kwenye mkataba uliosainiwa na Rais?
6) Nchi kutoruhusiwa kuingia makubaliano na mwekezaji mwingine yeyote ama kujenga, kuendeleza au kuendesha bandari zingine, haoni kuwa ni kuua sovereignty ya nchi?
7) Sheria zetu za fidia ya ardhi zinatamka wazi kuwa anayehitaji kuitumia ardhi, na ardhi hiyo ikawa inamilikiwa na watu au taasisi nyingine, anayeihitaji ndiye anatakiwa kulipa fidia, lakini IGA inatamka kuwa ardhi yoyote ambayo DP ataihitaji, Serikali ya Tanzania ndiyo itakayowajibika kuwaondoa wamiliki wa ardhi na kuwalipa fidia. Kwa nini sheria zetu zikanyagwe kwa sababu ya DP? Kama sheria ni mbaya, kwa nini haijabadilishwa ili kila mwekezaji akitaka kuwekeza, kazi ya kutafuta ardhi kwaajili ya mwekezaji liwe ni jukumu la Serikali?
8) Nchi yetu imewekeza matrilioni ya pesa katika kuijenga, kuiboresha na kuiendeleza bandari ya Dar es Salaam, Majaliwa aoneshe kwenye mkataba, uwekezaji wetu utatupatia hisa ngapi katika uendeshaji baada ya DP kuwekeza kiasi gani? Lakini akumbuke kuwa mktaba na DP unasema DP atakuwa na umiliki wa 100% katika uendeshaji! Yaani sisi uwekezaji wetu umefanywa kuwa ni 0%. Kama tulichowekeza sisi ni 0%, kwa nini DP asipewe eneo akajenge bandari from scratch?
9) Tatizo kubwa la kukosekana ufanisi katika miradi na mashirika yote yanayosimamiwa na Serikali, iwe ni bandari, TANESCO, mamlaka za maji, ATCL, mahospitali, TBS, n.k. ni uwezo mdogo wa viongozi wa Serikali ambao wameyageuza mashirika haya kuwa sehemu za kuwapachika watu kwa misingi ya itikadi za kisiasa, kufahamiana na undugu, na kisha kiyaingilia katika uendeshaji waje. Je, ina maana kila mahali tutawaweka wawekezaji wa nje? Kwaajili ya ufanisi, kwa nini tusiangalie kwanza msingi na chanzo cha matatizo yote ambayo ni uduni, upeo mdogo, ukosefu wa uadilifu na udhaifu wa uongozi wa nchi yetu kwa muda mrefu? Haoni tunapoteza muda kushughulika na matawi wakati shina na miziz ya mti wenye sumu umebakia kama ulivyo?
10) Ni lini JMT ilitangaza kuwa suala la bandari siyo miongoni mwa mambo ya Muungano? Maana bandari za Zanzibar hazijaingizwa kwenye mkataba huu wa hovyo.
11) Kwa nini Mbarawa, ambaye ni Mzanzibari, amekuwa waziri kwenye wizara isiyo ya Muungano? Kwa nini Aisha ambaye ni Mzanzibari, amekuwa katibu mkuu wa Wizara isiyo ya Muungano?
12) Kwa nini uporaji huu wa rasilimali za Tanganyika umefanyika kipindi ambacho wafanya maamuzi wote ni Wazanzibari, tena wengine, kwa kadiri ya artickes of union, hawakustahili kuwa kwenye nafasi ambazo zimewezesha kuporwa kwa bandari ziluzopo Tanganyika?
NB: MAJALIWA AFAHAMU KUWA WANANCHI SIYO TU WANASTAHILI KUSIKILIZWA LAKINI NDIO WENYE MAAMUZI YA MWISHO KUHUSU RASILIMALI ZAO.
WANANCHI HAWATAKIWI KUFUATA MAAMUZI YA VIONGOZI BALI VIONGOZI WANATAKIWA KUTII MAAMUZI YA WANANCHI.