Ninamshangaa Dr Mollel anapolalamika watanzania kuchangia harusi kuliko kuchangia matibabu!Falsafa za kiongozi ndizo hutengeneza mwelekeo wa watu wake

Ninamshangaa Dr Mollel anapolalamika watanzania kuchangia harusi kuliko kuchangia matibabu!Falsafa za kiongozi ndizo hutengeneza mwelekeo wa watu wake

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,289
Reaction score
5,741
Binafsi nikiri ni mchangiaji mzuri wa arusi ingawa ni utamaduni wa hovyo sana kukubalika katika jamii wa watu maskini na wanaojitafuta.

Kusema kweli wengi tunaoshirikishwa tunajikuta tunalazimika kutoa ili tusiwakwaze ndugu na marafiki kwa kuwa jambo hili hakuna viongozi wa dini hususan wakristo wanaokemea hill ijapo wakristo ndio ambao hufanya ujinga huu.

Kusema kweli kwa waziri kulalamikia jambo hili naona sio sahihi kwa kuwa ninachoamini ni kwamba watu huishi falsafa za kiongozi wao.
Ninaamini kiongozi kama Rais wa nchi akiwa na falsafa zinazomuongoza,ni rahisi kuuambukiza umma kupitia kwa waajiriwa wa serikali na watu maarufu.

Ningekuwa Rais ningepambana sana kuwajengea wananchi utamaduni wa kuchangia elimu na wagonjwa kuliko kuchangia harusi na pesa zinaishia kununua pombe na maua ya kichina .

Huwezi kuthubutu kuwaambia wakemee jambo hili kwani utasutwa sana kwamba unasumbuliwa na roho ya umaskini
 
Back
Top Bottom