Ninalaani vikali kukamatwa kwa Lema! CHADEMA msipochora mstari...

Lema ni mhuni tu. Maneno yake siku zote yamejaa uchochezi. Hivi yeye Lema yupo vp tofauti na viongozi/wabunge wenzake wa cdm? Kwa mfano:
1. Wakati wa uchangishaji m4c Dar alishawahi kusema eti km makampuni ya simu hawataacha kuzuia watu kutuma fedha basi chips zao watazitupa chooni. Hakujua kuwa kulikuwa na watu wengi wakituma hivyo kuwa na congestion. Km isingelikuwa busara ya mbowe mambo sijui yangekuwaje
2. Juzi bungeni alipoambiwa na Lukuvi afute maneno yake ya kumsema vibaya rais wa nchi alimgeukia Lukuvi na kumnyooshea kidole as if anaongea na mtoto wake n.k

Kwa kweli Lema hana kauli za kistaarabu. Siku zote akiongea anakuwa km anaongea na watoto. Si ajabu hata mkuu wa mkoa AR alifanya hiyo dharau yake ya kipuuzi. Uvumilivu una mwisho.
 
Sijui nitumie lugha gani kuelezea hisia zangu juu ya kile kinachoendelea nchini na hasa matumizi ya Jeshi la Polisi dhidi ya raia. Lakini siyo tu matumizi lakini hasa jinsi jeshi hili limekuwa likitumia nguvu kubwa sana kwa ajili ya vitu vidogo na hata visivyo na msingi. Kukamatwa kwa Lema na hasa namna alivyokamatwa ni dalili ya matumizi mabaya ya madaraka ya polisi (abuse of power). Kwamba, kwa vile polisi wana uwezo wa kupekua na kukamata basi wanaweza kufanya hivyo popote, kwa yeyote na kwa lolote wakijua kabisa kuwa hakuna wa kuwakemea. Jeshi la Polisi kama lilikuwa linamtaka Lema vibaya namna hiyo lingeweza kabisa kutumia njia za kawaida za kisheria ikiwemo kumpa wito wa kufika makao makuu ya Polisi wakimueleza anahitajika kwa nini na kama angekataa basi kupata kibali cha mahakama kumuendea na kumkamata na kama kutoa warranti ya kipolisi basi jambo hilo lingefanyika bila kuonesha hisia kuwa Lema analengwa bila ya sababu (targetted for no apparent reason) isipokuwa tu kwa vile ni Lema na ameonesha msimamo wake wa kutokuwapigia magoti watawala. Ni Uhuru huu wa Lema unawatisha watawala zaidi kuliko kitu kingine chochote. Mwendelezo wa vitendo vya aina hii dhidi ya wabunge wa CDM ni jambo la kukataliwa, kulaaniwa na kupingwa na kila mpenda demokrasia na anayeamini katika haki za raia (civil rights). Kwa miaka sasa tangu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 tumeona vyombo vya dola vikitumika kiunyanyasaji dhidi ya viongozi na wanachama wa CDM; kuanzia Arusha hadi Mbeya, Mwanza hadi Ruvuma, Dar hadi Kigoma. Ni vitendo vyenye lengo la kuwatisha na kuwakatisha tamaa viongozi na wanachama wa CDM lakini zaidi ni vitendo vyenye lengo la kufifisha na kudunisha mageuzi yanayokuja. Uongozi wa CDM unapaswa kuchora mstari - ambao naamini watashangaa kuwa umeshavukwa - wa kuhakikisha vitendo hivi vinakoma. Kuendelea kulalamika na kudai serikali na dola inawaonea hakutoshi tena (rejea "Karipio Kali). Nimewahi kuandika huko nyuma kuwa kama CDM hawatatuma ujumbe kuwa the balance of political power in the country has shifted - in CHADEMA'S favor - basi wajue wataendelea kunyanyaswa, kudhalilishwa, kuonewa na kubambikiziwa kesi na tuhuma za kila aina. Wanahitaji kuamua kama wataendelea kufanyiwa hivi au watume ujumbe kuwa "enough is enough". Wasipofanya hivi - na nimewahi kulisema hili pia - watajiandaa kulia na kusikitika na wasipoangalia kujikuta wanazika viongozi na wanachama wao kwani watawala hawaogopi maneno makali ya majukwaani, au vitisho vya matamko. CDM wafikirie namna moja itakayotuma ujumbe dhahiri, wa makusudi na usio na shaka wala utata kuwa mabadiliko ya nchi yanakuja na hakuna lolote ambalo CCM au serikali yake wanaweza kufanya kuzuia. NI mafuriko ya mabadiliko ambayo mkondo wake unatiririka kwa nguvu zote na CCM ama wapishe vinginevyo watasombwa. Jaribio la kuchimba mifereji na kuweka udongo njiani litafeli kwani mafuriko haya hayatakoma. Ni kwa sababu hiyo ninalaani vikali, na kupinga kitendo cha jeshi la POlisi kutumia nguvu ya chombo hicho kumkamata Lema - Mbunge wa ARusha na raia wa Jamhuri ya Muungano ambaye amekataa kufanya kile ambacho watu wengine ni rahisi kukifanya - kupiga magoti mbele ya madhabahu ya CCM na kutoa sadaka za sifa za uongo. MMM (BGM)
bora useme wewe mkuu pengine watakusikia!lakini mi nadhani ni suala la muda tu yote haya yatakwisha.hakuna marefu yasiyo na ncha.
 
Tatizo lako unatumia taarifa za JF kuhukumu mambo usiyoyajua kwa undani...

funga domo kama huna cha kuandika,wanaume wenye uwelewa na wazarendo wa nchi hii watoa hisia zao na zenye mashiko na sio upuuz wenu wa kucheza dance hosptal ni wendawazimu.
 
MMM uko sahihi sana. Ni lazima kuchora mstari sasa na vyombo vya dola vielewe kuwa mamlaka ya mwisho yako kwa wananchi. Viwaheshimu na kuwatendea haki wenye Nchi.

Wasi wasi wangu ni nani wa kuuchora huo mstari? Kwa lugha nyingine mstari unaotakikana una namna yake ya kuuchora, ni nani wa kuongoza uchoraji huo? Umma uko tayari, wongozaji je?

Kumbuka MMM, jipu limeiva, linahitaji mkamuaji tu, lakini hakuna aliye tayari kulikamua jipu, labda wenye Nchi wenyewe waamue kufanya hivyo.

Nachelea kusema kwamba uzoefu wa kusimama kidete katika haki mpaka mwisho na kutoa fundisho kwa Serikali na vyombo vyake ili viwe vinasimamia haki siku zote na sio kuwaonea wananchi unakosekana hapa Tanzania.

Siasa zetu ni za kistaarabu mno, hakuna aliye tayari ku-risk! Kuwaondoa kina Mulugo siku 14 hazijaisha?

Zipo post hapa kuwa watu wamechoshwa na matamko, wanataka vitendo! Wakati mwingine ili watu waweze kuheshimiana ni lazima kukwaruzana kidogo. Vyama vya siasa vinatakiwa vilielewe hili kwa mapana zaidi.
 
Tusiumize vichwa kuhusu kukamatwa kwa Lema. Bora hili limetokea maana litarahisisha CCM kuondolewa madarakani.

Mkoa wa Manyara sasa unategemea sana siasa za Arusha hasa za CDM. Kuna mabadiliko makubwa ya kisiasa yanakuja katika Mkoa wa Manyara na kilimanjaro. Lema amekuwa role model kwa vijana wa mikoa hiyo. Tusubiri.
 
Unashangaa vipi polisi kukamata mtuhumiwa ?...ulitaka wakae pembeni na kushangilia alichofanya ? Isitoshe taarifa zilizokuwepo ni kuwa aliihitajika polisi ili ahojiwe sasa kwa nini alikuwa anakwepa kwenda polisi kuhojiwa kama hana kosa ? Wewe badala ya kumshangaa Lema unawashangaa polisi...Juzi juzi kule Boston polisi walikuwa wanasaka watuhumiwa wa kutega mabomu, na alipohojiwa mzazi wa mmoja wa aliyekuwa anatafutwa alionekana kushangazwa na mwanae kuhusishwa na tuhuma zile..Sasa swali hapa ni kwa nini alikuwa anakimbia kama hakuwa na kosa ? na mbaya zaidi yeye na mwenzake walikuwa wanatumia silaha kujilinda..unajilinda vipi dhidi ya jeshi linalokutafuta kama si kutarajia mazingaumbwe ? kama walikuwa hawahusiki wangejisalimisha mapema..sasa kukimbia tayari ilikuwa ni ushahidi tosha kuwa ni wahusika..Na wewe mtoa mada huku ni sawa na yule baba mzazi wa mtuhumiwa aliyeapa kuwa mwanae hawezi kuhusika na tuhuma hizo asilani...Tuache dola ifanye kazi yake
 
unashangaa vipi polisi kukamata mtuhumiwa ?...ulitaka wakae pembeni na kushangilia alichofanya ? Isitoshe taarifa zilizokuwepo ni kuwa aliihitajika polisi ili ahojiwe sasa kwa nini alikuwa anakwepa kwenda polisi kuhojiwa kama hana kosa ? Wewe badala ya kumshangaa lema unawashangaa polisi...juzi juzi kule boston polisi walikuwa wanasaka watuhumiwa wa kutega mabomu, na alipohojiwa mzazi wa mmoja wa aliyekuwa anatafutwa alionekana kushangazwa na mwanae kuhusishwa na tuhuma zile..sasa swali hapa ni kwa nini alikuwa anakimbia kama hakuwa na kosa ? Na mbaya zaidi yeye na mwenzake walikuwa wanatumia silaha kujilinda..unajilinda vipi dhidi ya jeshi linalokutafuta kama si kutarajia mazingaumbwe ? Kama walikuwa hawahusiki wangejisalimisha mapema..sasa kukimbia tayari ilikuwa ni ushahidi tosha kuwa ni wahusika..na wewe mtoa mada huku ni sawa na yule baba mzazi wa mtuhumiwa aliyeapa kuwa mwanae hawezi kuhusika na tuhuma hizo asilani...tuache dola ifanye kazi yake
mkl158k imethibitishwa umepokea tsh 7000 kutoka kwa nape nnauye
 
Lema ni mhuni tu. Maneno yake siku zote yamejaa uchochezi. Hivi yeye Lema yupo vp tofauti na viongozi/wabunge wenzake wa cdm? Kwa mfano:
1. Wakati wa uchangishaji m4c Dar alishawahi kusema eti km makampuni ya simu hawataacha kuzuia watu kutuma fedha basi chips zao watazitupa chooni. Hakujua kuwa kulikuwa na watu wengi wakituma hivyo kuwa na congestion. Km isingelikuwa busara ya mbowe mambo sijui yangekuwaje
2. Juzi bungeni alipoambiwa na Lukuvi afute maneno yake ya kumsema vibaya rais wa nchi alimgeukia Lukuvi na kumnyooshea kidole as if anaongea na mtoto wake n.k

Kwa kweli Lema hana kauli za kistaarabu. Siku zote akiongea anakuwa km anaongea na watoto. Si ajabu hata mkuu wa mkoa AR alifanya hiyo dharau yake ya kipuuzi. Uvumilivu una mwisho.

Viongozi wa CCM wanachefua hawa sio wa kuwafanyia ustaarabu hata kidogo...Toka lini mtu nayepanga kukuuwa,kukulaza njaa,kukunyima maji,kukunyima elimu, unamfanyia ustaarabu? toka lini mwizi unamfanyia ustaarabu? Watu wanahasira usiwaeleze huo ujinga wa ustaarabu kwa watu wabaya kama haya MACCM.
 
Naweza kuhisi unachokilenga. Endelea zaidi ya hapo, lakini nakuakikishia propaganda zote hizo haziwezi kushinda atakacho Mungu juu ya nchi hii. Hamwezi kufanya lolote mnalotaka simply because ninyi ni watawala bila kufuata sheria.

Kwa vyovyote vile hakutakuwa na kesi dhidi ya Lema maana tulishajua in advance nini kilitokea mbali na kesi mtakazoziunda ninyi.
Wewe wasema!
 
Mzee Mwanakijiji,Kimsingi mimi nakuunga mkono kabisa kwa bandiko lako,hasa kuhusu kutafuta suluhu endelevu na si kuendelea kuwaambia wananchi juu ya uonevu wa serikali,afterall hata wao wanajua wazi kuwa Maccm na Serikali yao imebaki kutumia vyombo vya dola kufifisha mabadiliko yajayo,hasa ukizingatia yameanza kushika kasi.
Kimsingi hatua iliyobaki kwa CHADEMA ni kuwaongoza watanzania wapinga udhalimu,wapinga uonevu,na wapenda mabadiliko kwenye suluhu endelevu ambayo kwangu mimi naona ni kuiambia serikali ya CCM kuwa hapa sasa mwisho.lakini haiwezekani kufikia huko kwa maneno bila vitendo,hatuwezi kufikisha ujumbe kwa watawala.Na ili ujumbe ufike ni lazima dhamira yetu ya moyoni isiwe ni ya kutanguliwa na tamaa ya madaraka,bali itanguliwe na moyo safi wa kizalendo,wa kulipenda taifa,moyo wenye upendo kwa wanadamu wenzio na hivyo kuwa jasiri hata kufikisha ujumbe kwa ku-sucrifice maisha,kukubali kufungwa na hata kupata ulemavu ukipigania haki.CCM kamwe hawatatoka madarakani kwa kuwapigia tarumbeta,na kadri kasi ya mabadiliko inavyoogezeka ndio na wao wanapanga mkakati wa kudhoofisha kasi hiyo.
Ni jukumu la viongozi wa CDM kuwaongoza watu kwenye kupeleka ujumbe wa kukataa unyama unaoendelea kwa kutumia kile kilichotangazwa kuwa mwaka huu kwa CDM ni mwaka wa nguvu ya umma.tuuongoze umma kukataa mbinu dhalimu za kufifisha kasi ya mabadiliko.

Hakuna mageuzi ya aina yoyote yanayoweza kuongozwa na wenye shibe kwani hao wanacho cha kupoteza; uongozi wote wa sasa wa cdm hauwezi kufanya anachokisema MMM kwa kuwa watapoteza shibe zao na ccm wanalijua hilo kwamba hawatathubutu mpaka pale tutakapokuwa na viongozi wenzetu wenye njaa kama sisi ndio hilo laweza kutimia na si leo wala kesho; kwa maneno mengine kimbunga anachoongelea MMM hakijakusanya nguvu ya kotosha na hatujafikia huko.
 
Hakuna mageuzi ya aina yoyote yanayoweza kuongozwa na wenye shibe kwani hao wanacho cha kupoteza; uongozi wote wa sasa wa cdm hauwezi kufanya anachokisema MMM kwa kuwa watapoteza shibe zao na ccm wanalijua hilo kwamba hawatathubutu mpaka pale tutakapokuwa na viongozi wenzetu wenye njaa kama sisi ndio hilo laweza kutimia na si leo wala kesho; kwa maneno mengine kimbunga anachoongelea MMM hakijakusanya nguvu ya kotosha na hatujafikia huko.
Time will Tell.
 
hii ni zaidi ya hatari kwa usalama wa Raia na mali zao,who to trust sasa? kama mkuu wa mkoa nae anatuma msg za kutishia watu? halafu kwa nini katika serikali hii mbunge wa upinzani hana haki kama wa chama tawala?
 
Back
Top Bottom