Ninakwenda mafunzo ya JKT...

Ninakwenda mafunzo ya JKT...

Status
Not open for further replies.
Imagine jama anaenda kwa wiki tatu kama sio utani na dharau ni nini? Three weeks atapewa "uchele" huyu?
Hata UKURUTA atakuwa hajamaliza! Kwa nini sheria za NCHI zinachezewa hivi? Tena eti wameandikiwa barua kwenda JKT badala ya kwenda kwa mujibu wa sheria!
 
wiki tatu tu? Kwa hiyo ile kwata tuliyopiga Jitegemee itakua zaidi ya hiyo yenu
 
Uzalendo sio kuvaa bendera ya taifa mwigulu labda ukienda hayo mafunzo unaweza kuongeza upeo wako wa kufikiri na utaacha kutumikia wezi na mafisadi wa nchi hii.kwa sasa bado huna uzalendo kwani unajua nchii ipo wapi akina nani wakulaumiwa na bado unajifanya hujui.kila la kheri.

Naamini atajifunza nidhamu japo kidogo iwapo makamanda huko JKT watamtreat inavyostahili kama watanzania wengine.Vinginevyo kuhusu uzalendo ni ndoto Mwigulu kurudi akiwa mzalendo maana uzalendo unajengwa na haufundishwi kama hesabu!!Asante Jonaleemson kwa kumwambia uzalendo sio kuvaa bendera kama hirizi!!!
 
Wake za watu sasa huko uendako

umeandaa faini za kutosha kama igunga?

kaka mtenga tunapoongea mambo ya msingi tujaribu kuweka kando mambo ya siasa uchwara ma mambo yakusikia. Mwigulu amekanusha mara kibao kiss hajawahi kukutwa na mke WA mtu ma hakuna aliyejitokeza kuwa ndiye aliyemkuta na mke wake. Hata hivyo hata ingekuwa hivyo kama basi unataka huduma yake mtafute sio kufanya deal la kisiasa kila siku. Wewe unakiheshimu kiasi gani. Tunajua mwigulu no mwiba WA cdm hili halitoshi kuwa ndio swala kubwa kwa hisia wakati babu yenu amepoka mke WA mahimbo na kuzaa naye
 
Natumai utarudi ukiwa 'mzalendo' wa kweli kwa nchi yako, maana unafiki wako wa kuvaa skafu ya bendera ya Taifa wakati unalihujumu unanichefua kweli! Kila la heri...
Rows hujuma gani hiyo tuache kujumuisha wary kwa chuki binafsi
 
hayo sio mafunzo ya kijeshi nadhani wanakwenda warsha au semina. mafunzo gani ya kijeshi ya wiki tatu?
 
Wana JF, salam!

Nategemea kushiriki mafunzo ya JKT yatakayoshirikisha wabunge vijana. Nafanya hivyo kwa ajili ya NCHI YANGU, VIJANA WENZANGU NA CHAMA CHANGU.

Nawatakia ujenzi mwema wa taifa kwa kutumia ubao huu/tuition hii ya bure itoayo elimu ya maisha ie JF.

Hongera Shemeji

Ila safari hii ukifunzwa uzalendo uelewe na ku-practice

Usifanye kama ulivyofanya kwenye hizo taaluma nyingine.....
 
Waheshimiwa wanakwenda kufanya nini? mafunzo gani ya Jeshi kwa wiki tatu? Ujinga mtupu
 
kahamasishe vijana wa ccm jinsi ya kujiandaa kuiba kura tutachinjana 2015(ujumbe ndio huo)longolongo huna lolote tumewashawastukia ccm na jkt
 
Hivi Mwigulu watakuruhusu kuvaa kile kitambaa chako cha kisharobaro huku ukiwa ndani ya gwanda?
Utupe update please.
 
Wadau, nina swali kidogo.
Hivi wabunge walioishia FORM SIX nao wanaenda JKT au batch hii ni ya wale wenye degree tu?
 
Hapo ndio umeonesha UZALENDO na utajifunza mengi na kuachana na hao wasioheshimu Bunge na Viongozi
 
Hongera bw Lameck, ushauri wangu kwako japo cku za nyuma niliwahi kukwambia cpendezwi na aina ya saisa uzifanyazo, naamini ulijaribu kutafakari na kuona mapungufu fulani ktk siasa zako sasa nakushauri kupitia hiyo fulsa hadhimu jaribu kubadilika na kuwa mzalendo wa kweli wa nchi na c wachama pambana kuitetea nchi chukia ufisadi ambao chama chako ndio kimekuwa mama wa ufisadi epuka kupinga hoja za zamsingi na za kweli eti kwakuwa zimetolewa na upinzani hasa chadema na NCCR.tanguliza maslahi ya nchi na wananchi na c ya chama ambacho kwa hakika unatambua mapungufu madhambi na madhahifu yake.mwisho kama kweli umed dhamiria mafunzo ya JKT yatakufanya uwe c mwigulu yule wa siasa za chuki ghiriba matusi na dharau bali mwigulu mwenye siasa za kuheshimaiana kujenga hoja kuvumilia na kutetea nchi kwa maslai ya wote,asante na nakutakia mafunzo mema Mungu awakulinde na kuwatunza wewe na wote mtakaohudhuria mafunzo hayo.

bora umepata kumhabarisha huyo jamaa na siasa zake za maji taka.
Ni vema umkumbushe ambebe na. chizi mwenzie Lusinde kutoka mtela waende wakafundwe namna ya kuishi na wanajamii bila ya kutembea na wake za watu pamoja na kutukana matusi mbele ya umati wa watu wenye kukuzidi elimu,umri,fikra,hekima pia mali na akili.
Inaonekana kalelewa ktk mazingira ya uchokora huyo jamaa.
watoto mwenye malezi ya baba na mama hawako hivo.
Nenda kitchen part pamoja na majuha wenzako wote mkafundwe upya kwani mnakera ktk jamii kwa matusi yenu.
pweeeeeeee! kama kinyesi.
 
Barua imeonesha muda wa kuanza tu ila najua sio mwaka mmoja ni kipindi kisichopungua wiki tatu wala si zaidi ya miezi mitatu

Ina maana hawa watu hawajajipanga bado? Watasemaje 'kipindi kisichopungua wiki tatu wala kuzidi miezi mitatu?

Mtu anatakiwa awe na uhakika jeshini ni muda gani ili aweke mipango sawa baada ya jeshi. Mfano, wengi ni wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita, na kwa vyovyote watakuwa ama wanajiandaa kwenda chuo kikuu, au sehemu nyingine kujiendeleza au hata kuanza kazi. Sasa kama hajui ni lini atakuwa amemaliza mafunzo jeshini, atasema nini huko anakotafuta nafasi ya masomo au ajira?

Au kwa kwa mfano, wewe mbunge, utajipangaje jimboni kwako kama hujui jeshini unatoka nini? kuna vikao vya kawaida na wanajimbo, kuna vikao vya madiwani ambavyo vyote mbunge anatakiwa awepo, sasa kama huna ratiba kamili ya jeshini watajipangaje hawa watu hata kama wangekubali kusogeza vikao?
 
Ni vyema na hongera kwa hilo ila wasiwasi wangu kwenu nyinyi waheshimiwa msiende kulpeleka nyazifa zenu kwenye mafunzo hayo mkifanya hivyo hamtakuwa na cha kujifunza. Nawaomba pia makamanda wa JKT muwatreet hawa jama kama raia wa kawaida na si waheshimiwa kwani lengo la kuwapeleka huko ni ili watakapo rudi wawe na moyo wa uzalendo kwa taifa lao sasa kama uheshimiwa ukipewa kipaumbele huko mafunzoni mafunzo yao hayatakuwa na maana itakuwa ni sawa na kupoteza fedha za umma naomba sana makamanda wa JKT mtakaowafua hawa jamaa mzingatie hilo.
 
Mwigulu,
Mimi sikushauri uende sababu nilipata taarifa kuwa huwa unatembea na wake za watu,
Sasa hebu ona wakati unaenda Igunga na kutembea na wake za watu si ungeweza kwenda
na wife wako au girlfriend wako?sasa huoni wewe utatumia hela za ufisadi kutembea na wake za watu?
Angalia wanajeshi wanaweza kukumaliza,jaribu kuwa binadamu yasijekukuta mabaya
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom