Ninakosea wapi? Au biashara ni kipaji?


Kuna mzee pale kkoo sokoni
Yeye mauzo alikuwa anachanganya anachukua mzigo juu ya mzigo

Hili janga la juzi la moto sijui limemuacha katika hali gani!!
 
Kuna mzee pale kkoo sokoni
Yeye mauzo alikuwa anachanganya anachukua mzigo juu ya mzigo

Hili janga la juzi la moto sijui limemuacha katika hali gani!!
Aisee hiyo ni hatar Sana, Nampa pole Sana
 
Kama Manara anakula 700k hawa wa viwandani si wanakula 10k
 
Kama ukitoa kila kitu kuanzia mshahara/matumizi yote unabakiwa na faida ya 80,000 to 100,000

sikushauri uache hiyo biashara hata kidogo,wewe kilio chako ni faida ndogo ila si kwamba hupati kbsa

wenza
Dah! Safi sana broo nimependa unavyompa moyo wa kupambana mdau! "Superb" ni wachache sana wa aina yako wengi wetu tumekuwa watu wa kukatishana tamaa. Nimejifunza jambo kubwa sana katika huu ujasiriamali.
 
Hii shule nimeichukua
 
Ukianzisha biashara kuna ulazima wa wewe mwenye biashara kuwa msimamizi mkuu kabla hujamwajiri mtu! Hii itakusaidia kupata picha kamili ya matumizi na mauzo kwa siku mpaka mwezi mzima!! Itakusaidia kujua range ya mauzo ikoje,, ila ukifungua biashara na kumwajiri mtu direct inakuwa ni rahisi yeye kukuibia maan hujui kabisa range ya mauzo!!
 
Mtaacha huyu mtu achanganyikiwe,
Ushauri anaopokea ni wa maamuzi magumu hata zaidi ya hicho anachopitia sasa...

Yaani kirahisi tuu unamwambia mtu Aache kazi??? Unajua waajiriwa wewee???

Suala la kuoa nalo, ni Suala la msingi lakini sio , eti oa leo kesho upate cheap labor....
Haya yote ni kweli na yana msaada ila ni mambo makubwa yanayohitaji maamuzi chini ya utulivu ila sio kwa shinikizo....

Kinyume na hapo mnataka miezi ijayo aje na mrejesho wa huzuni tena...

Mambo mengi sitofautiani na wadau humu....

Hio elf 80 sio mbaya, asiache hio biashara,

Vitu vya kuzingatia
Awe anaenda kukaa ofisini mwenyewe pale anapopata nafasi kwa ajili ya hesabu, tathmini na kupata Uhalisia wa mauzo,
Aongeze bidhaa mpya zinazoendana na bishara husika, mfano Card za harusi, Flash, mahitaji yote ya shule n.k

Anapoingiza mzigo mpya Awe na kumbukumbu ya kila kilichoingia na idadi, siku anaambiwa kitu flani kimeisha aanze kupiga hesabu ya kimoja baada ya kingine na kuangalia je kilichobaki na kilichoenda vinaendana je vinaleta usawa wa mahesabu ya jumla?

Kila pesa anayotumia/pewa au inayoingia kwenye matumizi yoyote afanye record...

Ashushe matumizi ya mfanyakazi (hapa sasa yawezekana ikawa tatizo, hivyo ikimlazimu abadili mfanyakazi maana aliyezoea 200k ukimshusha mpk 150k ndio anaweza akuibie)

Ukikaa mwenyewe ukaona kuna mauzo mazuri zaidi ya anayokuletea, Mpe mashart ya kiwango cha chini cha mauzo kwa WEEK, akishindwa Mpe notisi...

Kipindi ukikaa kazini wewe fanya tathmini ya matumizi ya umeme kwa WEEK fananisha na matumizi yake yeye kwa mda huo huo...
 
Mkuu hapo badili mfanyakazi na umlipe mshahara huo wa 50k, hiyo wa sàsa motoe tu.

Kamwe usiweke ndugu hapo mkuu... maana umesema uweke ndugu abanane na huyo mfanyakazi wa sàsa bampa to bampa, sasa huyo ndugu ndo atamshauri mfanyakazi wakuibie zaidi alafu kushokutwa utarudi hapa kuiuza stationary yako kwa sababu utayoiita (mapato hayaendani na ulivhowekeza).

Badili hiyo taka fasta hapo na usiweke ndugu tafadhali.
 
Broh usigombanishe watu una uhakika gani anaibiwa
Umeongea kitaalam xnaa mkuu kuna wengine wanakimbilia kusema mfanya kazi ndio anaiba..binafsi kazi izo masuala ya location pia ni yanahusika..kama hauko karib na vyuo au taasis zinazitumia xna makaratasi bhc vumilia
 
Duh mkuu we ndo mjasiriamali... Ila kama sheli ndo mishahara yao hiyo .. si watakuwa wanagongwa sana?
 
Uko sahihi.
Lakini kitu kingine ambacho nimegundua hapo matumizi ya uendeshaji ni makubwa mno ukilinganisha na faida itakayopatikana na itakuwa ni kutwanga maji kwenu labda kama hiyo stationery iko mjini kama Kkoo au Ilala au ndani ya chuo hapo sawa inaendana na hayo matumizi ila kama ni nje ya mji hiyo biashara hailipi.
Unaweza kumtafuta mchawi kumbe kuna mahesabu umeyakosea,watu wenye roho ya ujasiriamali anapoanza biashara kuna mawili either amuweke mke wake au akae yeye mwenyewe kuepuka matumizi.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
amsome jamaa gani sijakuelewa maana wengi ni wahanga wa biashara
 
nilivyoelewa mm ni kua mauzo ni laki 4 hdi 4.5 kwa mwezi na matumizi kila kitu kwa mwezi ni laki 3 na kumi hapo vitu vinapungua sababu si vinauzwa kama wino karatasi pen daftari n.k sasa sijui kwa nn wanampigia hesab za faida ya elf 80 huyu jamaa anapata hasara sio faida na kuna wizi sana stationary wale watu ni wajanja sana pia wanaweza hata pata tenda za kadi za harusi na wasikwambie huyu kama anapata faida haizidi elf 30 kwa mwez
 
hapa ni mtaji wa milion 3 mauzo hayafoki elf 20.kwa siku hata muuza.nyanya mtaji wa laki 2 anauza zaidi ya elf 20.huyu hajajiongeza kwanza anatoa mshahara mkubwa pili posho acancel tatu kama ataweza afunge camera ofisini
 
80000 sio faida kumbuka kauza na vitu vimepungua dukani kama wino pen daftar rim n.k hapa faida huenda ni elf 30 tu
 
hii ni kweli mr wangu anahuruma mnooooo na hakuna anachofanikiwaga hadi sasa nimeacha kupartner nae ktk biashara sabab tunaelewana vizuri wafanyakaz wote wanaripot kwangu unakuta wakianza fanya madudu wananikimbia wanaripot kwake na anawasikiliza at tgw end hakuna ni hasara juu ya hasara nakumbuka kuna kipindi kawekeza sehemu zaidi ya mil 10 hajawahi kula hata elf 50 anakuwaga anawapa darasa ila waaapi msimamizi ndo kwanza akaoa na kuzaa kwa pesa zake haki ndo siku nilijivua kufanya nae biashara niliona nikizubaa nimekwisha mm na wanangu now ninachomshaur awekeze ktk nyumba za kupangisha tu biashara hawezi hana roho ya kijasusi kusimamia biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…