GE2025 Ninaishauri CCM irudie upya kura za maoni nchi nzima

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
1,289
Reaction score
2,190
Kuna malalmiko mengi nchi nzima kuhusiana na kura za maoni zilizopigwa hivi karibuni. Wengi wamelalamika kuwa rushwa ilitawala sana na hasa wale walioshika namba moja hawakushika namba moja kwa haki.

Ninaishauri CCM irudie zoezi hili kwa mara ya pili ili haki ipatikane. CCM inapiga vita rushwa sasa ni kwa nini ikubali rushwa itawale kwenye zoezi hili?.
 
Waripoti Taarifa za rushwa katika mamlaka husika.
 
Mkuu kubali matokeo kuwa umepoteza. Tafuta milioni 600 ujipange awamu ijayo.
 
Kuna malalmiko mengi nchi nzima kuhusiana na kura za maoni zilizopigwa hivi karibuni. Wengi wamelalamika kuwa rushwa ilitawala sana na hasa wale walioshika namba moja hawakushika namba moja kwa haki.

Ninaishauri CCM irudie zoezi hili kwa mara ya pili ili haki ipatikane. CCM inapiga vita rushwa sasa ni kwa nini ikubali rushwa itawale kwenye zoezi hili?.
Rushwa ni halali ndani ya CCM ya sasa ,ndio maana mwenyekiti kahonga pikipiki,kahonga baskeli kahonga takataka chungu nzima na wanachama mbumbumbu wanaruka ruka tu maamuma hawa.
 
Tafuta hela uwape wajumbe.
Wajumbe wanauza kura zao kama huna pesa imekula kwako acha kulalamika.
 
Kuna aliyepelea kupewa hiyo rushwa Hadi warudie? Au hao watoaji wa rushwa watakuwa wameishiwa? Au hao wapokeaji watakuwa wametosheka?
 
Kuna malalmiko mengi nchi nzima kuhusiana na kura za maoni zilizopigwa hivi karibuni. Wengi wamelalamika kuwa rushwa ilitawala sana na hasa wale walioshika namba moja hawakushika namba moja kwa haki.

Ninaishauri CCM irudie zoezi hili kwa mara ya pili ili haki ipatikane. CCM inapiga vita rushwa sasa ni kwa nini ikubali rushwa itawale kwenye zoezi hili?.

Mwenyekiti mwenyewe ndiye mtoaji rushwa namba 1, sasa wa chini yake wakifuata mfano aliouonesha mwenyekiti wao, kuna ubaya gani? Kwani wewe hujafikiwa na baiskel, pikipiki au mtungi wa gas wa mama? Rushwa ndiyo sera kuu ya CCM kwa sasa, hakuna wa kulizuia hilo kwa sababu ndiyo mwongozo alioutoa mwenyekiti kwa wagombea.

kama kuna mgombea hakutoa rushwa, umshtaki kwa mwenyekiti kuomba afutwe uanachama wa CCM, kwa kosa la kwenda kinyume na mwongozo wa mwenyekiti.
 
Kamshitaki mgombea urais wa ccm kwanza, ndipo ulalamikie wagombea udiwani na ubunge.
 
Back
Top Bottom