Ninaionya Serikali katika kuingiza siasa kwenye Mashirika na Wakala zake mbalimbali

winnerian

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
335
530
Kuna trend inaendelea ya kuweka siasa kwenye kila kitu ambacho serikali ina nguvu na mamlaka juu yake bila kujali dira mwelekeo na maono ya taasisi hizi.

Kubadilisha watendaji wakuu kwenye taasisi, mashirika na wakala tendaji za serikali kwa vipindi vifupi vifupi ni kuingiza siasa kwenye uti wa mgongo wa nchi na sote tunajua siasa mwisho wake ni mbaya na hakuna mwamba mbele ya siasa. Tuiziache hizi taasisi zijitegemee mbali na siasa. Unapomuondoa mkuu wa taasisi tendaji kama kumbadilisha mkuu wa mkoa unaua mambo mengi sana ya taasisi maana taasisi za serikali zinajiendesha kwa "Mission" na "Vision" sasa kila mara unabadilisha mwenye mwelekeo na maono halafu mwisho wa siku unataka matokeo chanya kamwe hutoyapata.

Naishauri serikali yafuatayo:-
1. Upatakanaji wa watendaji wakuu wa taasisi, mashirika, na wakala wake uwe wenye lengo la kumpata mtu makini sana ambaye ana nguvu, ari, uwezo wa mkubwa akili na uzalendo na atakaeweza kuhudumu katika nafasi yake kwa kipindi kisichopungua miaka flani ili kuleta matokeo chanya. Ingekuwa raisi anabadilishwa badilishwa kila mara nchi yetu isingekuwa na utulivu.

2. Nafasi hizi zisiwe za teuzi bali ziwe "competitive positions", maanake washindanishwe watu wenye uwezo na mchakato uwe wa wazi kabisa ili kuboresha upatakanaji wa mtu mwenye uwezo mkubwa na weledi. Leo Rais kampenda mbumbu na kumchagua sehemu nyeti yenye kupelekewa pesa nyingi za nchi kisha anaharvurunda tu na kupoteza pesa za umma.

3. Taasisi zote zenye maslahi mapana na zenye kuleta matokeo chanya serikalini zipewe uhuru wa kujitegemea na sio kuwa chini ya viongozi wa kisiasa.
 
Wataonekanaje kwamba wanafanya kazi, tuliamua kuipa siasa kipaumbele toka enzi ya mwalimu hayo ndo matunda yake.
 
Kwa mujibu wa maelekezo ya watendaji ni kwamba CEO Hana madaraka yoyote.katibu mkuu ndio aneyepanga na kupangua.na pia katibu mkuu ndie mwenyekiti wa bodi.sasa huyoCEO aliyeteuliwa kisiasa atafanyaje?nimemsikiliza Dr Slaa ameainisha hivyo.
 
Kuna trend inaendelea ya kuweka siasa kwenye kila kitu ambacho serikali ina nguvu na mamlaka juu yake bila kujali dira mwelekeo na maono ya taasisi hizi.

Kubadilisha watendaji wakuu kwenye taasisi, mashirika na wakala tendaji za serikali kwa vipindi vifupi vifupi ni kuingiza siasa kwenye uti wa mgongo wa nchi na sote tunajua siasa mwisho wake ni mbaya na hakuna mwamba mbele ya siasa. Tuiziache hizi taasisi zijitegemee mbali na siasa. Unapomuondoa mkuu wa taasisi tendaji kama kumbadilisha mkuu wa mkoa unaua mambo mengi sana ya taasisi maana taasisi za serikali zinajiendesha kwa "Mission" na "Vision" sasa kila mara unabadilisha mwenye mwelekeo na maono halafu mwisho wa siku unataka matokeo chanya kamwe hutoyapata.

Naishauri serikali yafuatayo:-
1. Upatakanaji wa watendaji wakuu wa taasisi, mashirika, na wakala wake uwe wenye lengo la kumpata mtu makini sana ambaye ana nguvu, hari, uwezo wa mkubwa akili na uzalendo na atakaeweza kuhudumu katika nafasi yake kwa kipindi kisichopungua miaka flani ili kuleta matokeo chanya. Ingekuwa raisi anabadilishwa badilishwa kila mara nchi yetu isingekuwa na utulivu.
2. Nafasi hizi zisiwe za teuzi bali ziwe ""competitive positions" maanake washindanishwe watu wenye uwezo na mchakato uwe wa wazi kabisa ili kuboresha upatakanaji wa mtu mwenye uwezo mkubwa na weledi. Leo raisi kampenda mbumbu na kumchagua sehemu nyeti yenye kupelekewa pesa nyingi za nchi kisha anaharvurunda tu na kupoteza pesa za uma.
3. Taasisi zote zenye maslahi mapana na zenye kuleta matokeo chanya serikalini zipewe uhuru wa kujitegemea na sio kuwa chini ya viongozi wa kisiasa.

Adui wa taifa hili ni CCM, chama chakavu kilichotufikisha sisi Watanzania hapa tulipo leo. Hata wakikana watakavyo ukweli ni kwamba matatizo yote katika taifa hili yamesababishwa na CCM.

Na sasa hata Rais anatanguliza uCCM katika shughuli zote rasmi za kiserikali. Vyombo vyetu vya dola vimetelekeza wajibu wao wa kuwalinda wananchi na badala yake kuwa vitengo maalum vya kuilinda CCM.

Lakini funga mwaka ni Bunge hivi sasa kugeuzwa uwanja kwa CCM kujipigia kampeni na kumtukuza Rais. Wamepoteza kabisa sifa ya kuwa wawakilishi wa wananchi kwa kuisimamia serikali kwa niaba yetu.
 
Back
Top Bottom