Ninadhani wanasheria wa CHADEMA wameishauri vibaya Kamati Kuu

Ninadhani wanasheria wa CHADEMA wameishauri vibaya Kamati Kuu

Mkuu, Unavyoandika ni kama vile kweli una hisi huruma kwa Chadema, mimi namini pasipo na shaka wewe ni wale ambao mnatumwa au umejitolea ili kutaka kujua wananchi wanasemaje kuhusu haya yanayotokea,
Jaribu kutulia ujiulize maswali yafuatayo

1-Hivi ni kweli wagombea wa ccm wote ndio wanauelewa /ujuzi wa kujaza hizo fomu kwa usahihi ?
2-Ni kwanini wagombea wa ccm peke yao ndio walioruhusiwa kurudisha fomu kabla ya siku iliyopangwa kuanza zoezo la urudishwaji fomu ? (huoni kulikuwa na hiden agenda hapo)?
3-Kwanini unataka chadema waanze h\kuhangaika na mahakama sasa ilhali taratibu zingefuatwa na hayo yasingekuwepo
4-Unajua kuna gharama kuendesha makesi hayo ?, Chadema wanapata wapi fedha ya kugharimia hizo kesi .
5-Unaona kuna mahakama hapa nchini eti ya kusikiliza kesi ambapo ccm/serikali ndio walalamikiwa ?
6-Kwanini watendaji (maeneo mengi nchini) wamekuwa wanafunga Ofisi zao na kukimbia ?
6-Haya yote yanayofanyika, Watendaji wanatimiza maagizo kutoka juu,
7-Unajua magufuri aliwaambia nini watendaji wote alipowaita ikulu siku chache zilizopita ?,
8-Unadhani magufuli huyo huyo anaweza kufukuza hao watendaji

Anachoongea Jafo ni unafiki, anajua fika yanayoendelea.
Niishie hapo nina mengi sana ya kuongea na wewe.
 
Tukundane,
Well said. Mie kwanza sijajiandikisha kupiga kura. Nawaza kwa sauti.
 
Ukitaka kujua kama Tanzania kuna upinzani dhaifu au imara basi:
*Polisi wajitenge na ccm.
*Kuwe na tume huru ya uchaguzi.
*Demokrasia iwe huru nchini.

Hapo sasa ndiyo unaweza kusema upinzani ni dhaifu au sio dhaifu.
sasa kama hivyo vitu havipo nyie kama upinzani nmechukua hatua gan?
 
Elius W Ndabila,

Unaweza kutuambia mantiki ya maamuzi ya kesi ya Lissu juu ya uchaguzi mdogo Singida kuwa "kungekuwa na wabunge wawili" kama angeamua vinginevyo? Hata mwanafunzi wa semista ya kwanza wa sheria asingetamka hivyo! Unategemea haki ipatikane toka kwa mahakimu/majaji wa aina hii? Uamuzi wa CDM ni sahihi 100%
 
Elius W Ndabila,
Sikukuona ukitoa ushauri wakati dhuluma hizi zilipoanza kufanyika.
Muda huu ndo unajifanya kuonesha masikitiko yako kwa Chadema kujitoa huo ni unafiki.
Mimi nadhani ni muda wenu wa kushangilia kwa sababu malengo yenu ya kupata ushindi kwa asilimia 100 yametimia sasa
 
Hoja zako ni za hovyo maana tayari rufaa zilizokatwa 100% zimeshatolewa uamuzi kuwa hawakuteuliwa kwa kukosa sifa.
Mimi sihitaji kuelewa mtu kama wewe kwa sababu hata tofauti kati ya uchaguzi na uteuzi hujui. Anayechagua ni mpiga kura; kwa hali hii ni wazi TAMISEMI wameteua au kama walivyoagizwa ama kwa kutokujua kuwa wapiga kura ndio wenye kauli ya mwisho.

Kwa maagizo tunayojua toka kwa mwenye nchi aliagiza atangazwe mtu wa CCM hata kama wapiga kura hawajamchagua .
Ebu jiridhishe kuwa ni kweli kuna uchafuzi badala ya uchaguzi.
 
Ninyi mmetaka mshinde kila mahali mnaita ikulu watendaji wa kata kuwapa maagizo yakukimbia Ofisi kila wanachama wa vyama vingine wanaporudisha fomu....lengo muonekane mnakubalika sasa ilikuwasaidia Chadema wamewapata nafasi zote povu zanini? kujitoa wajitoe wao povu mtoe ninyi
 
Mkuu kuondolewa wagombea wao 85% sio jambo la kawaida. Anzia uchujuaji na urudishaji form ndio utaona kwamba huko mbele giza ni kubwa zaidi.

Pili mchakato wa kujiandikisha wenyewe ulionekana kudorora daliki kwamba wananchi wanamashaka juu ya uchaguzi.

Hatujaona hatua kali zikichukuliwa kwa watendaji wazembe kwenye uchaguzi. Sasa bora huo uchaguzi usifanyike kabisa watu watangazwe washindi.

Haiwezekaniki jimbo zima la uchaguzi watu wapite bila kupingwa. Hiyo tu ingekuwa alarm na kufuta hizo hatua za awali mchakato urudiwe maana watendaji 90 wamewanyima watu zaidi 50,000 haki ya kupiga kura
 
Ukitaka kujua kama Tanzania kuna upinzani dhaifu au imara basi:
*Polisi wajitenge na ccm.
*Kuwe na tume huru ya uchaguzi.
*Demokrasia iwe huru nchini.

Hapo sasa ndiyo unaweza kusema upinzani ni dhaifu au sio dhaifu.
Yaaani ccm na serikali ndo wameamua sana hawakutegemea kbs maana hawana tena guts za kujimwambafy kuwa wanapenda halafu huko cdm kuna maji tu yana akili wamehakikisha wamekata evidence yoteza rafa na kauli za wanaccm.... siasa ni sayansi
 
Unaendaje mahakamani wakati mahakama ipo chini ya CCM
Umenikumbusha zuio la kuapishwa kwa mbunge wa jimbo la Lissu.... kwamba uamuzi wa leo hauathiri uamuzi wa baadaye, hiyo baadaye ilipofika sasa,..........
 
Mkuu umepoteza muda tuu kushusha shudu,inaonekana unaandika ili kuendelea kuwahadaa wajinga wachache ,kipi usichokielewa Sasa hapo ulishawah ona kesi ya ngedere ikatatuliwa Na nyani
Sasa watashitaki wapi? Nendeni ICC basi au waache siasa.
 
Umeandika tu, ukisukumwa na nia yako ya nje.
Hatukuona ukiandika kufuatia hila, undava, ukatili waliofanyiwa hao wagombea wa Chadema.
Kwa mantiki hii naona kabisa, umefanya hivi kwa makusudi makubwa.

Sasa kwa ukweli like neno uchaguzi halipo tena, Sasa mmeanza kumtafuta ng'ombe wa kumvika kengere.
Umenichekesha sana, pole nilikuwa naamini kama una akili bado, lakini umebaki na undumila kuwili.
Maamuzi ya kamati kuu Chadema ni dhabiti na yamekuja wakati muafaka.
 
Kwa kweli viongozi wetu wa chama chetu cha Cdm wametuvunja moyo sisi wanachama wao. Nasari alionewa walienda mahakamani, Lisu kaonewa wamekwa mawakili lukuki kumtetea, leo sisi wanyonge tumeonewa kwa maelfu hawaendi popote kututetea. Sasa najiuliza wametudharau au sisi hatuma umuhimu katika chama?
 
We endelea kukurupuka kama vile huon kinachoendelea. Nyambafu
 
Back
Top Bottom