Ninadhani wanasheria wa CHADEMA wameishauri vibaya Kamati Kuu

Ninadhani wanasheria wa CHADEMA wameishauri vibaya Kamati Kuu

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
678
Jana kwenye vyombo mbalimbali vya habari Mh Mbowe(mb) na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa amenukuliwa akisema chama chake kimejitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 ya mwezi huu. Mh Mbowe amesistiza kuwa hayo ni maadhimio ya Kamati kuu na makubaliano ya kikao cha Wabunge kilichoketi jijijni Dodoma jana tarehe 7. Mkakati wa CHADEMA kwa mjibu wa Mh Mbowe Mbunge si tu wamesusia uchaguzi, bali watasusia shughuli zote zitakazokuwa zikiratibiwa na viongozi watakaochaguliwa kuanzia tarehe 24.

Baada ya matamshi hayo ya CHADEMA niliona twetter moja ambayo ilikuwa inahusishwa na nukuu ya Mh Jafo Waziri wa TAMISEMI akisema kuwa CDM kususia uchaguzi ni kuwanyima haki wananchi. Alisema CHADEMA wanapaswa kukata rufaa na siyo kususia uchaguzi. Alisema hata hivyo yapo maeneo rufani zimeanza kusikilizwa na aliwataka wasikiliza rufa wote wasiwe binded na maamzi ya mwanzo.

Baada ya hoja hizo mbili, yaani nukuu kutoka CDM na nukuu kutoka TAMISEMI ndipo ninaposhawishika kusema CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO wamefanya makosa. Tena wamefanya kosa la kiufundi. Ninatambua watanielewa wachache kwa sababu wengine tumejazwa na mihemko, lakini ifahamike hivyo kuwa wamefanya kosa ambalo sikutegemea kwa Chama kama CDM wenye wataalamu wengi wangefanya kosa kama hili. Ibara ya 107 katiba yetu inaeleza namna mtu anavyoweza kutafuta haki anayohisi imeporwa. Katiba inazungumza na sheria mbalimbali za uchaguzi zinaelekeza.

Njia sahihi ambayo CDM wangefanya ilikuwa ni kukata rufaa wakidai mazingira yaliyotumika kuwaengua wagombea wao si za kweli. Wangefanya hivyo kwa kuwa ushahidi wao wa kwanza ni zile copy za fomu ambazo ni valid evidence before the Court. Hii ingesaidia kujua kama wagombea walionewa au wao ndio walifanya makosa kwenye ujazwaji wa fomu? Kama kosa ni Watendaji kufunga ofisi basi mazingira hayo pia rufani zao zingezingatiwa. Ninadhani ulikuwa ni muda sahihi wa CDM kuviamini vyombo vinavyohusika na rufaa kwa kuwa precedents zinaonyesha CDM walishawahi shinda matukio hayo kwenye vyombo hivyo hivyo iweje leo wasusie kwa kusema hawaviamini? Local Government (Elections) Act ninadhani imesomwa vizuri, lakini kwa nini hizo offences hamjazikatia rufaa na mnasusia uchaguzi? Kama mlijua sheria hazifai, kwa nini mliingia kwenye uchaguzi kwenye sheria ambazo hamziamini?

Kutokuviamini vyombo ambavyo ninyi wenyewe mumevipa nguvu kisheria kushughulikia masuala yenu, vyombo ambavyo mara nyingi tumesikia mkivipongeza kuwa vimetenda haki basi mimi ninapata mashaka kuwa huenda wagombea wenu wameenguliwa si kwa kuonewa bali walikuwa wamefanya tekinikaliti errors. Ninamini wangeonewa basi mungeenda hatua za juu kutafuta haki yenu. Lakini kutokwenda kwenye nafasi ya rufani ni kujaribu kuficha yale yanayonyeshwa kuvurundwa kwenye kujaza fomu. Ninadhani kama kuna maeneo mumeonewa tengueni msimamo wenu nendeni mkate rufaa, wakishindwa kuwasikiliza angali mnaona mlikuwa na haki chukueni hatuazingine.

Hata hivyo ninajaribu kufikiria ni kweli watendaji wanaweza kuwaonea CDM kwa kiwango hiki? Kama CDM wataamua kukata rufaa, na rufaa zao zikasikilizwa na wakashinda kwenye rufaa hizo ningependekeza Mh Rais awafukuze watendaji wote nchini na kuwatupa ndani. Kwanza kwa kumhujumu na kumgombanisha na wananchi na pili kwa kutaka kuwanyima wananchi haki ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa inayotolewa Ibara ya 21(1). Haiwezekani Watendaji kuonea watu wakati Mh Rais siku zote amesistiza maendeleo hayana vyama na WATANZANIA WOTE NI SAWA.

Lkini hata hivyo kisheria uchaguzi hauwezi kuahirishwa kwa chama au vyama kujitoa , kwani sheria zipo wazi. Tanzania inavyama zaidi ya 20, chama kimoja kikijitoa bado hakiondoi mfumo wa vyama vingi unasomeka kwenye ibara ya 3 ya katiba yetu(Declaration of multiparty state).

Mwisho udhaifu wa vyama vya siasa ndio unaokipa nguvu CCM kuwa kwa sasa hakiwezi kutoka madarakani labda miaka ya huko mbeleni. Upinzani uliopo Tanzania ni dhaifu na ni upinzani wa watu kutengeneza maisha. Upinzani huu ni dhaifu. Upinzani imara kwa CCM ulipaswa kuwa na vyama vitano tu vyenye nguvu na hoja nzuri. Lakini Tanzania kuonyesha upinzani ni furusa ni huu utitiri wa vyama tena vyenye hoja zilezile tangu 1994. Hawana hoja mpya za kuwashawishi watu kuiondoa CCM, na CCM inatumia udhaifu huo kujichimbia mizizi yak echini zaidi.
Tafakari.
 
Ukitaka kujua kama Tanzania kuna upinzani dhaifu au imara basi:
*Polisi wajitenge na ccm.
*Kuwe na tume huru ya uchaguzi.
*Demokrasia iwe huru nchini.

Hapo sasa ndiyo unaweza kusema upinzani ni dhaifu au sio dhaifu.
 
Nia ilikuwa chama kushinde kwa asilimia mia bila kujali mbinu za ushindi. Sasa kama hawa wamejitoa voluntary basis watu wanywe mfinyo was ushindi
 
Tatizo la CHADEMA wanayo migongano ya wao kwa wako ndani ya chama ila wanaacha kutafuta suluhu baina yao ,wao wanataka kuonyesha watu as if nothing is going on ...na ndiyo mwisho wao huu
 
CUF ndio chama kikuu cha upinzani tunachokitaka na TLP, PPT Maendeleo nacho kipo vizuri
 
Tusishangilie kuona vyama vya upinzani vinaminywa.
Hakika nawaambia, nguvu zao ni muhimu sana kwenye kuliendesha gurudumu la maendeleo.
Vikifa, hakuna wa kupiga kelele mambo yakienda kombo
 
Ukitaka kujua kuwa CHADEMA wamechukua maamzi sahihi ni pale ambapo watu jamii ya Jafo wanapolaumu kujitoa kwa CHADEMA kwenye uchaguzi.

Lakini watendaji walipokuwa wanafunga ofisi kwa kuwazuia wapinzani wasichukue fomu na watendaji walipokuwa wanatoa fomu fake kwa wapinzani, wapinzani wanapokamatwa na kubambikiziwa kesi wanapokwenda kudai fomu za uchaguzi hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza kukemea vitendo hivyo, vyote waliona ni sawa
 
Chadema waliingia uchaguzini dakika za mwisho,hawakuhamasisha wafuasi kujiandikisha
Wametoka uchaguzini dakika za mwisho

Inaweza kuwa mkakati mahsusi ili kususa kutengeneza picha mbaya,au wamenusa tu kushindwa
Wasuse tu,ukimsusia mwwnywkiti wa mtaa barua ya udhamini wa mkopo wa polisi kumtoa ndugu utapata wapi?
 
Mbona unalialia mkuu,CHADEMA wamewaachia ulingo mshinde kwa 100%.

Unafikiri haya maoni yako wanasheria wa CHADEMA hawakuyafikiria? Au unafikiri wewe ndio unaweza kuwaza vyema zaidi kuliko wao?

Haiwezekani hata siku moja mapungufu yawepo kwa wapinzani pekee ila wanaCCM wawe sawa. Zinduka,tapika huo ujinga,pona!
​
 
Back
Top Bottom