Ninadaiwa Tala, Branch na M-pawa. Nisipowalipa watanifanya nini?

Wasalaam ndugu zangu... Kuna hii mikopo inayotolewa kwa njia ya mitandao nadhani wengi wao tumekopa huko... Sababu wana ushawishi mkubwa mnoo wa matangazo yao

M-pawa nilianza kukopa tangu nipo chuo nasoma nilikua nakopa boom likitoka nawalipa alafu nakopa tena nikafikisha hadi 79,000 deni lao, baada ya kumaliza chuo nilishindwa kuwalipa pesa yote hivyo nikalipa kidogo hadi deni likabaki 48,000

Mwaka jana mwishoni nikakopa branch kwakua walikua wana nishawishi kwa matangazo yao ila tatizo mkopo wao ulikua haupandi unaishia 23800 pamoja na riba nimelipa mara tatu.. nikaona niachane nao hivyo deni nnalo la 23800

Nikahamia tala... Hakika tala kwenye kupandisha pesa kila unapo lipa deni wako vizuri na wanapanda kwa 20,000 kila unapo rejesha mkopo wako... Nilikua nalipa deni lao kila baada ya siku tatu nikajikuta pesa imefika hadi 193,000 kwa week mbili na nusu...

Tatizo kwa sasa sina pesa ya kuwarejeshea hao jamaa... Pesa ninayo ipata inaishia kwenye matumizi yangu ya kila siku na pango la nyumba...

Je! Hao jamaa watanifanya nini maana wameanza kunitumia meseji za vitisho.. sijui nitaorodheshwa kama mdaiwa sugu hao m-pawa na deni lao lina miaka zaidi ya mitatu..... Hawa wengine wanasema nitajiharibia CV ya mikopo..

Sina mpango wa kuwalipa Sasa kulingana na hali yangu ya uchumi ila nikipata pesa nzuri nawalipa wote kwa pamoja.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Branch watakusumbua sana..mimeseji kila siku na kupigiwa simu hadi kero

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! Nilijua ni mimi mwenyewe ni mdaiwa sugu kumbe wapo wengine poa? Hii hali itatufikisha pabaya kwa kweli.

Ninachodaiwa binafsi ni;
1. Tigo nivushe 413,120/=
2. Mpawa 74,300/=
3. Branch 23,800/=
4. Tala 20,000/=
5. Nipige tafu vodacom 6,900/=

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mbona mm mpesa haipandi inabaki 10,000/= kila mara

Japo nachelewa kuwalipa saan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! Nilijua ni mimi mwenyewe ni mdaiwa sugu kumbe wapo wengine poa? Hii hali itatufikisha pabaya kwa kweli.

Ninachodaiwa binafsi ni;
1. Tigo nivushe 413,120/=
2. Mpawa 74,300/=
3. Branch 23,800/=
4. Tala 20,000/=
5. Nipige tafu vodacom 6,900/=

Sent using Jamii Forums mobile app
Anza tu kuwalipa branch maana ile mimeseji yao inakera halafu wanakwambia tutaweka majina kwenye mtandao ya wadaiwa sugu hahaahahahahahah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujanielewa... Nimekosa pesa ya kuwalipa kwa sasa ila nikipata watapata pesa yao

Sent using Jamii Forums mobile app

Sina mpango wa kuwalipa Sasa kulingana na hali yangu ya uchumi ila nikipata pesa nzuri nawalipa wote kwa pamoja.....

Hapo uliposema hauna mpango wa kuwalipa kwa sasa na vilevile hadi utakapo pata pesa nzuri, hauwezi kumlipa mdeni wako kwa pesa ya ziada, kwanza haipo, ni sawa na mtu anapojibana kukukopesha pesa wakati ana mambo yake ila ameamua tu akusaidie kisha unaanza kutaka upate pesa ambayo inabaki baada ya mambo yako ndio umlipe, haiendi hivyo MKUU.

Ushauri wangu, jitahidi walipe kidogo kidogo katika hali ngumu hiyo hiyo unayopitia. Siku ingine utakosa mtu wa kukusaidia.
Lakini sikulaumu sana, kulipa madeni ni kipaji.
 
Back
Top Bottom