sweet poison
Senior Member
- Aug 16, 2013
- 104
- 15
Mara nyingi Watanzania hususani Waislam tumekuwa katika mkanganyiko mkubwa kwamba BAKWATA ni ya Waislam, wengine wakisema ya serikali, na wengine wakiwa na majibu yao mengine!
Nimekuwa nikimsikiliza mtu mmoja hapa katika mikutano yake nanukuu "BAKWATA ni tawi la Kanisa," baada ya kusoma rejea mbalimbali kufahamu historia ya BAKWATA nikagundua kuwa mwaka 1968 ndio ulikuwa mwanzo wa BAKWATA.
BAKWATA iliundwa na mwalimu Nyerere baada ya kuivunja EAMWS ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa ni taasisi iliyokuwa imepiga hatua kubwa katika uchumi, siasa na elimu Afrika Mashariki.
Kwanini Nyerere aliivunja EAMWS? Ni swali tuulizane mimi na wewe. Je, alikuwa kama nani katika taasisi za dini? Nalo tuulizane.
Kiufupi, BAKWATA imekuwa ikipingana sana na Waislamu waliowengi hapa nchini katika mambo mengi yahusuyo dini, kibaya zaidi inapingana hata na taasisi zingine za Kiislam!
Nawaulizeni wadau, BAKWATA ni ya nani?