Ninaacha Ualimu tangu leo

Daah na inatia hasira ukisikia ESICUROUW imepigwa ka 170billion afu watu wanasema za mboga lazima hasira zikuzidie
 
Nimaamuzi mazito hila yanaitaji weredi Wa kutosha kulingana na ulivo na mishe unazoweza kuanza nazo
 
Ama kweli Uoga ni akiba ya Umaskini !!
 
Dah nilivyosoma nimeumia sana, yaani una deni LA miaka mitatu hujalipwa halafu uandike deni jipya tena! Hii inauma sana, maisha ambayo wanaishi walimu wetu yanatia huruma sana lakini bado kuna watu hawana huruma na walimu, hii ndio kada ya watoto wa maskini. MTU mshahara mdogo nauli humo humo, kodi ya nyumba, chakula kazini(achana na cha family), umeme, maji halafu kuna MTU analipwa mshahara wa ml.5+ na vitu vyote hivyo analipiwa na serikali.

Usiache ndugu yangu komaa hivyo hivyo Magufuli na Majaliwa niamini watafanyia kazi matatizo ya walimu.
 
Vipi ticha number zinasomeka?
Utajuta kwa nini uliuza haki za watu kwa kusaidia mfumo onevu.
Pongezi kwa kula kile ulichopanda.
Sasa panda mbegu sahihi, usirudie makosa.

Unaamini kuwa walimu ndo huwa wanaofanya CCM ishinde?
 
Acha kumfundisha mwenzako uoga wa Maisha,kuajiriwa sio kipimo cha mafanikio kimaisha.

Maana yangu ni kwamba atumie kuajiriwa kama opportunity ya kukopea halafu aanzishe mradi utakaomsukuma mbele. Nina hakika post #12 na #14 umezipitia na kuona advice waliyotoa, iko perfect
 
dada yangu ni mwalimu lakini jamani mbona waalimu wanadharauliwa sana
 

Tupeane maarifa mkuu na mim nafkria hivyo
 
Mimi nimeshaacha kujitambulisha mwalimu, unaonekana bure mbele za watu
 

hapa kuna kundi la waoga litakukatisha sana tamaa ila usirudi nyuma...kwani huku mtaani wanakodai kugumu watu wanaishi vipi?

Mimi pia nilikuwa nafundisha chuo cha private na nikaacha kazi mwaka 2013 baada ya kuona siwezi kutoka kwa namna yeyote ile, wengi walinibeza kwamba nitarudi. tu huko...ila mpaka sasa wanashangaa sina muda na hizo ajira zao na maisha yanaenda!!

Nina miradi ambayo inaniingizia zadi ya 2m kwa mwezi..wapi ningepata mshahara wa aina hiyo?
 
huo ualimu wenzio wanaenda mpaka kuroga walau waupate then we unaukataa.angalia usije lujutia uamuzi wako kijana
 
Wapo wa kuacha kazi lakini si wewe,,
 
Mimi nimeshaacha kujitambulisha mwalimu, unaonekana bure mbele za watu

mwalimu mwenye shahadi anakamata basic ya 730k,bank teller wa nmb mwenye shahada anakamata basic 500k,afu bado mnaona mnaonewa!
 
Ualimu una kero na manyanyaso mengi sana na hasa inapofikia kwenye haki yako. Mimi pia ni miongoni mwa watu ambao naelekea kuacha hiyo kazi. Afisa elimu ananizuia kwenda kusoma na wakat nimepata mkopo kisa sipo kwenye mpango wakati hata ukiwekwa kwenye mpango wanakuambia ujisomeshe. So ukitaka kufanikiwa kwenye ualimu lazima ukubali kutake risk
 
naona ni muda sasa wa mheshimiwa jpm na majaliwa kassim kuliangalia hili la walimu!! haiwezekan nasema haiwezekan kabisaaaaa
 
Pole sana mkuu Elli bt now unadeal na nni mkuu?

Mkuu naendelea na ujasiliamali tu, ni ngumu lakini ni nzuri kwakua kufanikiwa au kutokufanikiwa kunabaki mikononi mwako
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…