Nina wazo la biashara ila sina mtaji

Wadau mambo vipi mko poa? Nina wazo ila sina mtaji wa kuanzia nikipata wa kunishika mkono nitashukuru.

Plan yangu ipo hivi wazo langu ni kuwa nikiwa na kama sh 50,000 hizo zinatosha kabisa naenda kwenye duka la jumla linalouza nguo, za kiume/ kike za jumla mi plan yangu ni kuchukua zile nguo za ndani za kiume (boxer) dozen zipo tatu ndani ambayo kwa moja wao wanauza 3000 na kwa bei ya jumla unachukua kwa 9000,

Nitachukua nitakazoona zinazonifaa harafu narudi mtaani kuwauzia wana kwa bei ya 5000 kila boxer moja mtaji ukikuwa naongeza na za kike kidogo nitakazoona wadada wanapenda.

Kwa mwenye mawazo anaweza akaongezea hapo.

Pia soma: Njia za kupata mtaji wa biashara
Jinsia yako tafadhali?
 
Kijana huoni aibu kuomba mtaji wa 50,000/- ?

Ungeuza hiyo simu yako unayotumia naamini ungeweza kutatua tatizo lako.
 
Kiufupi tafuta hata kikazi hata cha ukibarua wa ujenzi sehem wanapojenga majengo makubwa. Ukiipata Naamin ndan ya wiki mtaji utaupata
 
Maisha haya.. Yan nimetoka kulipa bill ya bia karibia kiasi hicho kumbe ni mtaji wa mtu kabisa.
Daaaa phinah ulaaniwe na misavanna uliobugia kama maji
 
Wadau mambo vipi mko poa? Nina wazo ila sina mtaji wa kuanzia nikipata wa kunishika mkono nitashukuru.

Plan yangu ipo hivi wazo langu ni kuwa nikiwa na kama sh 50,000 hizo zinatosha kabisa naenda kwenye duka la jumla linalouza nguo, za kiume/ kike za jumla mi plan yangu ni kuchukua zile nguo za ndani za kiume (boxer) dozen zipo tatu ndani ambayo kwa moja wao wanauza 3000 na kwa bei ya jumla unachukua kwa 9000,

Nitachukua nitakazoona zinazonifaa harafu narudi mtaani kuwauzia wana kwa bei ya 5000 kila boxer moja mtaji ukikuwa naongeza na za kike kidogo nitakazoona wadada wanapenda.

Kwa mwenye mawazo anaweza akaongezea hapo.

Pia soma: Njia za kupata mtaji wa biashara
Hapa Dar sijaona sehemu gani utamuuzia mtu boksa moja kwa elfu tano. Nisijue kijijini na sijui uko wapi kwanza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom