Nina wakati mgumu, ushauri wako unahitajika

Nina wakati mgumu, ushauri wako unahitajika

Lol...haraka zingine sio nzuri, mwambie awe mvumilivu.
 
ameona umemdatisha ili awe karibu nawe lazima akuingilie na gia ya kuoa dah usipende kufurahisha nafsi ya mtu bali furahisha nafsi yako kwa maamuzi yako
 
Habari zenu wakubwa!! Wakubwa zangu heshima yenu nawapatia. Nimeanza uhusiano na dada mmoja kama miezi mitatu imepita sasa. Nampenda na yeye anasema ananipenda. Nimeanza naye uhusiano baada ya miezi kadhaa tangu mtu niliyemtambulisha nyumbani kwamba ndiye mke mtarajiwa kuvunja uhusiano bila sababu iliyo wazi. Kinachonisumbua sasa hivi huyu dada kila tunapokutana anaulizia sana mambo ya kuoana kiasi ambacho inanitia wasi wasi. Hatujafahamia vizuri, inakuwaje tuanze kuzungumzia kuona mapema namna hiyo? Yaani hajui hata vile vya juu juu kuhusu mimi na nnajua vichache kuhusu yeye. Napatwa na wakati mgumu kumjibu maswali yanayohusu jambo hilo, naogopa kuahidiana na mtu aafu mkijuana vizuri mkajikuta hamuendani. Nifanyeje ndugu zangu? Sikwepi majukumu ila naogopa kwa nini haraka namna hiyo?

ngoja kwanza bwana Nyalotsi, hebu tueleze kwanza.. ndani ya hii miezi mitatu, ulishawahi kumgegeda?!!

anzia hapo kwanza, then ntarudi!
 
Last edited by a moderator:
Lol...haraka zingine sio nzuri, mwambie awe mvumilivu.

si nasikiaga eti mvumilivu, hasa akiwa wa mjini anaweza kula na jirani!? au sio mkuu mdida?
 
Last edited by a moderator:
Habari zenu wakubwa!! Wakubwa zangu heshima yenu nawapatia. Nimeanza uhusiano na dada mmoja kama miezi mitatu imepita sasa. Nampenda na yeye anasema ananipenda. Nimeanza naye uhusiano baada ya miezi kadhaa tangu mtu niliyemtambulisha nyumbani kwamba ndiye mke mtarajiwa kuvunja uhusiano bila sababu iliyo wazi. Kinachonisumbua sasa hivi huyu dada kila tunapokutana anaulizia sana mambo ya kuoana kiasi ambacho inanitia wasi wasi. Hatujafahamia vizuri, inakuwaje tuanze kuzungumzia kuona mapema namna hiyo? Yaani hajui hata vile vya juu juu kuhusu mimi na nnajua vichache kuhusu yeye. Napatwa na wakati mgumu kumjibu maswali yanayohusu jambo hilo, naogopa kuahidiana na mtu aafu mkijuana vizuri mkajikuta hamuendani. Nifanyeje ndugu zangu? Sikwepi majukumu ila naogopa kwa nini haraka namna hiyo?

ila we nae kijana wangu unaniangusha kabisa..!! kwa hiyo ukimwambia ndoa ni baada ya miaka mitano, atakufa ?
 
*mwambie mambo mazur hayataki
haraka
*pia ni mda mfupi sana tumejuana
cwez kukwambia chochote kuhusu
kukuoa unless umeni force kufanya
hivyo,
*akupe mda wa wew na yey
kumchunguza na kumwelewa
mwenzie vizuri kabisa,sio tu kwako
wew na yeye,hadi kwenye familia
pia,usijekuta unataka kuoa familia
yenye machizi,
*jaribu kumwelewesha kwa
kumwambia haraka haraka haina
baraka,kama ni mwanamke
mwelewa atakuelewa na pia
onyesha msimamo kwamba hutaki
kuwekewa limit ya kwamba ni
lini,mwambie siku ikifika na
nikifanikisha nnachotaka kwanza
basi nitakwambia laa sivyo kama
anaharaka sana aende kwa ambae
atampa promise za uongo,
natumai tupo pamoja.
 
Mkuu inawezekana kabisa huyo dada ana nia njema pengine niulize uhusiano wenu una miezi mingapi. Kama imezidi 3 labda ndivyo alivyojiwekea yeye. Hii issue isikusumbue kaa na mwenzi wako ongeleeni suala hili na ujaribu kumuelimisha . Huenda pia anaogopa kukaa na mtu kwenye mahusiano kwa miaka 3 au zaidi kwa kisingizio cha kuchunguzana na mwisho wa siku akabaki mdomo wazi. Unaposema hamjajuana vya kutosha sasa huwa mnaongea nini mnapokutana , si toka siku ya kwanza mnashirikishana mambo yenu ikiwa pamoja na familia mnazotoka . Nikuulize swali la kizushi je wewe kwa huu muda mliojuana umeona anafaa kua mke au bado huna uhakika. Kumbuka probation period ni 3 months baada ya hapo ni bora ujue kama wewe ni permanent employee au bado wanaendelea kukuchunguza kabla ya kuenjoy benefits na kujua kama umefika au uendelee kutafuta kazi.
 
aah, bwana nae atulie. Ndio ni vzr kujua mtu ana mpango gani, ss mbona km yy ana haraka sana!!?
Mwambie asubiri,anafikiri ndoa mchezo! ooh!
 
*mwambie mambo mazur hayataki
haraka
*pia ni mda mfupi sana tumejuana
cwez kukwambia chochote kuhusu
kukuoa unless umeni force kufanya
hivyo,
*akupe mda wa wew na yey
kumchunguza na kumwelewa
mwenzie vizuri kabisa,sio tu kwako
wew na yeye,hadi kwenye familia
pia,usijekuta unataka kuoa familia
yenye machizi,
*jaribu kumwelewesha kwa
kumwambia haraka haraka haina
baraka,kama ni mwanamke
mwelewa atakuelewa na pia
onyesha msimamo kwamba hutaki
kuwekewa limit ya kwamba ni
lini,mwambie siku ikifika na
nikifanikisha nnachotaka kwanza
basi nitakwambia laa sivyo kama
anaharaka sana aende kwa ambae
atampa promise za uongo,
natumai tupo pamoja.

Nimekupata mkuu, nashukuru kwa ushauri wako mzuri.
 
Mkuu inawezekana kabisa huyo dada ana nia njema pengine niulize uhusiano wenu una miezi mingapi. Kama imezidi 3 labda ndivyo alivyojiwekea yeye. Hii issue isikusumbue kaa na mwenzi wako ongeleeni suala hili na ujaribu kumuelimisha . Huenda pia anaogopa kukaa na mtu kwenye mahusiano kwa miaka 3 au zaidi kwa kisingizio cha kuchunguzana na mwisho wa siku akabaki mdomo wazi. Unaposema hamjajuana vya kutosha sasa huwa mnaongea nini mnapokutana , si toka siku ya kwanza mnashirikishana mambo yenu ikiwa pamoja na familia mnazotoka . Nikuulize swali la kizushi je wewe kwa huu muda mliojuana umeona anafaa kua mke au bado huna uhakika. Kumbuka probation period ni 3 months baada ya hapo ni bora ujue kama wewe ni permanent employee au bado wanaendelea kukuchunguza kabla ya kuenjoy benefits na kujua kama umefika au uendelee kutafuta kazi.

Unajua tunapoanza mwanzo tulianza kama rafiki, tumeingia kwenye uhusiano bila kila mmoja kumjua mwenzie kiundani zaidi.nashukuru kwa ushauri
 
Asante kwa ushauri mwalimu! Tatizo anataka niseme lini ntakuwa tayari.

Taja muda mrefu kama miaka 2 au 3....nina hakika rangi zake utazijua.
Wengi tumefanya hivyo, waliotupenda walisubiri maana walipenda kweli.
 
aah, bwana nae atulie. Ndio ni vzr kujua mtu ana mpango gani, ss mbona km yy ana haraka sana!!?
Mwambie asubiri,anafikiri ndoa mchezo! ooh!

Yawezekana anahisi ntatumia papuchi yake na kusepa! BTW kuna watu wanajuaga uhusiano wowote lazima uishie kwenye kuoana, ndio maana wanatakaga kuambiwa mambo ya kuoana mapema.
 
Aaaah! Huko tena! Tumeshamalizana.

Safi.sasa kuwa na msimamo kwamba muoaji ni wewe na sio yeye kama alivoshauri gfsonwin

Halafu sio vema mwanamke kuulizia ndoa kama anakumbushia madeni ya saccos
 
Last edited by a moderator:
Nimemwambia kwamba tunahitaji kufahamiana lakini anataka time limit. Yaani maswali ya mpaka lini huwa nakereka nayo kwa kweli.! Yaani hapa nilipo sijamwambia hata structure ya familia yangu, sasa tuanze kuzumzia kuoana si akiona familia iko tofauti na vile alivotegemea atakuwa disapointed?
Definitely..kuna watu hawapendi kuolewa familia zenye/watoto/watu weengiii kama zetu hizi.
Sasa wewe kuwa na msimamo..mwambie NO..
Halafu kama vipi achana naye kaka..tayari ameonesha doa.
 
Last edited by a moderator:
Big Red Flag!!!!!!! 3 months is a very teeny amount of time to know someone...... Endelea kumsaundisha asubiri kwanza ili muweze kufahamiana kama ulivyo sema!!!!!!!! Napata wasiwasi isije ikawa anataka umuoe haraka ili usigundue tabia zake mbovumbovu mapema!!!!!

SHTUKA!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom