Nyalotsi
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 6,989
- 5,069
Habari zenu wakubwa!! Wakubwa zangu heshima yenu nawapatia. Nimeanza uhusiano na dada mmoja kama miezi mitatu imepita sasa. Nampenda na yeye anasema ananipenda. Nimeanza naye uhusiano baada ya miezi kadhaa tangu mtu niliyemtambulisha nyumbani kwamba ndiye mke mtarajiwa kuvunja uhusiano bila sababu iliyo wazi. Kinachonisumbua sasa hivi huyu dada kila tunapokutana anaulizia sana mambo ya kuoana kiasi ambacho inanitia wasi wasi. Hatujafahamia vizuri, inakuwaje tuanze kuzungumzia kuona mapema namna hiyo? Yaani hajui hata vile vya juu juu kuhusu mimi na nnajua vichache kuhusu yeye. Napatwa na wakati mgumu kumjibu maswali yanayohusu jambo hilo, naogopa kuahidiana na mtu aafu mkijuana vizuri mkajikuta hamuendani. Nifanyeje ndugu zangu? Sikwepi majukumu ila naogopa kwa nini haraka namna hiyo?