Nina PhD natafuta kazi

Nina PhD natafuta kazi

nenda kafundishe au tafuta kazi kwa kutumia iyo degree yako au masters, usilete sifa kwenye interview oooh nina PHD, tunakukata tuu, so wewe weka iyo degree au masters inategemea na kazi inahitaji nini then huko huko mbele utaonesha iyo PHD yako, otherwise wewe ni academician nenda kafundishe
 
pole sana!!! Jichanganye,,usisubiri kutafutwa.

lakini tukirudi nyuma nyie wenzetu ambao mko elimu za juu, anachokiongea mjomba kinawezekana?? inatukatisha tamaa nasisi ambao tuko chini.
mi nahisi there is something/somewhere wrong.

kama tu form vi leaver anatumia anaweza hata kufundisha hata tuition,,,,yani kweli mkuu umekosa fursa yoyote kabisa!!!! kuna vyingi sana kufundisha hata certificate!!!
Kubali kujishusha anzia chini ajira nzuri utapata tu.
(kama hutu enjoy!)
 
Ndg yangu weka picha tuone hivo vyeti vyako bana, haya mambo tumezoea kuyaskia Nigeria, yameanza lini Tz kuwa na jobless phd? lkn pole sana, mkuu hukubana bana vile vijisenti vya DAAD ukarudi na change kwa ajili ya capital? so sorry!
 
daaah eee bwana kwanza pole sana , watu wamekupa ushauri sana hapo juu chukua ushauri mzuri ufanyie kazi , rudi nyuma jiulize kwa nini ulienda kusoma phd , anzia hapo , hatua ya pili nenda orodhesha vyuo vyote vilivyosajiliwa nchini Tanzania , kuanzia mtwara mpaka nkasi fanya mawasiliano na vyote tuma barua na cv yako kwa vilivyo mbali na vilivyo karibu omba appointments peleka cv kwa wahusika , hata ukimuona lecturer mmoja kwenye hivyo vyuo anaweza kupeleka cv yako , kingine usikae unabweteka nyumbani na tv , phd manake ni research , kwa sasa anza kuandika paper , topic yoyote think tank zote zinapokea research papers zilizosimama kuanzia repoa mpaka esrf hili ni muhimu sana kupublish kitu kwa sababu kutoka kwenye mikiki ya kuandika maneno 90000 ya thesis alafu tu unapoteza fani alafu pia unavyopublish paper Fulani unajitangaza wasomi wengine wanaweza kukutafuta na hapo ndio network zinaongezeka ..prof wa mwanza anaweza soma paper yako akakuita muandike kitu akakupa link ya kazi iringa hayo tu
 
Leo Daily news wametangaza kazi inazoendana kabisa na qualification zako Muccobs apply ndugu na kila la heri
 
Huyu jamaa hana PhD, alafu atasababisha watu waone kusoma hakuna maana bure!!
 
Ingekua ni mimi nakushauri, kwa GPA yako hiyo ya undergraduate 3.4 bora ungeajiriwa kwanza upate experience, kusoma PhD kuna maana ulitaka kuwa intellectual wakati GPA yako ilikua ndogo. Ila hii nchi ni shida sometime hata GPA kubwa unakosa kazi mi mwenyewe na GPA yangu above 4 from the hill, sijaitwa hata kwenye interview ya Akiba Commercial Bank.
 
PHD serious, unafind kazi ??????
You mean ulienda kustdy Phd wthout direction, hivi hata ukipewa kazi utaweza kweli, Naogopa juu ya hilo.
Ok, my advice kwa level yako nenda kafanya volunteer, internship kwenye UN organzations kule watakupokea sema ukubali kujitoa. Sema umetuhaibsha watanzania.
 
huyu jamaa ni muongo, nendeni kaangalieni thread zake kwenye profile yake, kuna moja ameandika akielezea siku alipoacha internship bank moja hapa dar es salaam na anasema hiyo internship aliifanya kwa mwaka mmoja

ulishawah ona wap mtu mwenye phd anafanya internship..???
 
A Jobless PhD holder looking for a job!!!! It seems your studies taught you what to think rather than how to think,

Inaonekana ulikuwa unasomasoma Tu bila malengo kisa unamdhamini.kama vipi tafuta sponsor tena urudi shule.

'the best way to escape from hangover is to keep drinking'
 
Kuna mtu aliwahi kuniambia, nchi hii ukiwa mtu wa kushangaa, utashangaa mengi !Sasa mtu hadi unamaliza PhD unatafuta ajira kama Form Six ? Andaa CV vizuri , jenga confidence peleka CV yako kwenye Academic, Financial na Research Institutions ! Omba consultancies siyo lazima permanent employment.

Mwalimu wangu wa Sekondari wakati akituhamasisha kusoma elimu ya juu aliwahi kutuambia "Kwenda Chuo Kikuu ni rahisi sana, mtu yeyote hata kichaa, you just go to Mwenge or Ubungo, you board a UDA to the varsity" wakati huo chuo ni Mlimani. akaendelea " Tatizo ni kwenda kupata elimu Chuo Kikuu'' .

Mwalimu mwingine akatuuliza " mtu anatafuta degree ili nini? " tukabaki tunaangaliana, akatuambia acheni use.... "Unatafuta degree ili uweze kujenga Confedence ''!

Jamani napita kidogo !
 
Habari zenu ndugu zanguni,

Nimesoma B.A ya economics UD, kwa kuwa mzee wangu alikuwa ana kauwezo mdogo akanishauri nisome masters. Nilipokuwa nasoma Masters niliona tangazo la PhD scholarship ya DAAD-Germany, nikaomba kwa bahati nzuri nikapata hivyo baada ya kumaliza masters nikaenda kusoma Hamburg Ujerumani. Hivi sasa ninapoongea nina PhD ya business administration management na kwa bahati mbaya sana hamna tangazo la kazi wanalotaka mtu mwenye PhD asiye na experience hata kidogo, nimechanganyikiwa mpaka najuta kusoma.

Huu ni mwaka wa pili natafuta ajira, niliomaliza nao degree ya kwanza hivi sasa wana maisha mazuri namimi hali yangu haieleweki. Na wazazi uwezo wao kiuchumi umepungua sana hiyvo hawawezi kunipa hata mtaji nikafanye biashara, maisha haya jamani, sijui ninamfundisha nini mdogo wako anayenifata?

MKINIPA MAWAZO YA KUJENGA NTAWASHUKURU ZAIDI.

kumbe kuna kozi inaitwa business administration management!!? nielimishen jaman..
 
huyu jamaa ni muongo, nendeni kaangalieni thread zake kwenye profile yake, kuna moja ameandika akielezea siku alipoacha internship bank moja hapa dar es salaam na anasema hiyo internship aliifanya kwa mwaka mmoja

ulishawah ona wap mtu mwenye phd anafanya internship..???

jf noma
 
umbombo ngafu Mungu awe nawe fuata ushauri hapo juu jichanganye na wenzako .
 
Mtu ana PHD bado ajui jinsi ya kupata Kazi,eti uajiliwe,andika vitabu wewe
Nategemea utaandika reseach book
 
You can try this while hunting job JamiiForums.com Earn 10$ for every 30 second Task. Internet Job from home
 
Aisee pole sana mkuu,kwa hadhi yako hutakiwi kuwa ivyo ulivyo nakushauri uende chuo chochote ukajieleze kwa mkuu wa chuo kwamba una PHD ila huna experience kwa iyo unaomba angalau usaidie kufundisha kwa kukulipa angalau laki 5 kwa mwezi au nne nia na dhumuni ni kupata experience ili iweze kukusaidia kusonga mbele..Fanya kazi angalau miaka 2 then baada ya hapo utakuwa mbali sana...Usiangaike kuomba kazi kwa njia ya kutuma CV..Au kama vipi nipigie niweze kukushauri kitu cha kufanya..Napenda sana watu wanaopenda kusoma..0776 880 270.
 
Sio kweli labda private tena za vichochoroni hata uwe proff kama hauna academic GPA ya 3.8 and above kamwe huwezi kuitwa lecturer wengi wao wanakuwa wanafanya kazi za administration tu au researchers au wanadaidia malecturers but chuo hakimtambui km lecturer hata udsm wapo ma Dr ambao wana 3.7 na kushuka ila hawafundishi na hawaruhusiwi ila wamepewa nafasi tu nyingine za uongozi au wanawasaidia au kufanya project pamoja na ma Dr wenzao.


Nakwambia hiviiiiii nimesoma na watu UDSM,walipata GPA 3.5 undergraduate,na wakapata kazi Tutorial assitants IFM,then wakasomeshwa masters nje UK etc,na saiv ni ma assistant lecturers..usinibishiee wewe ebo?unataka kunambia ma TA na Assistant lecturers woote wana GPA ya 3.8 undergraduate??ebo Kaulize Mzumbe mana nako wapo wenye below 3.8 GPA na saivi ni Assistant Lecturers na wanafundisha hadi MAsterz (baada ya wao kusoma masters)
 
Habari zenu ndugu zanguni,

Nimesoma B.A ya economics UD, kwa kuwa mzee wangu alikuwa ana kauwezo mdogo akanishauri nisome masters. Nilipokuwa nasoma Masters niliona tangazo la PhD scholarship ya DAAD-Germany, nikaomba kwa bahati nzuri nikapata hivyo baada ya kumaliza masters nikaenda kusoma Hamburg Ujerumani. Hivi sasa ninapoongea nina PhD ya business administration management na kwa bahati mbaya sana hamna tangazo la kazi wanalotaka mtu mwenye PhD asiye na experience hata kidogo, nimechanganyikiwa mpaka najuta kusoma.

Huu ni mwaka wa pili natafuta ajira, niliomaliza nao degree ya kwanza hivi sasa wana maisha mazuri namimi hali yangu haieleweki. Na wazazi uwezo wao kiuchumi umepungua sana hiyvo hawawezi kunipa hata mtaji nikafanye biashara, maisha haya jamani, sijui ninamfundisha nini mdogo wako anayenifata?

MKINIPA MAWAZO YA KUJENGA NTAWASHUKURU ZAIDI.

mkuu pole sana, lakini wewe sio wa kulaumiwa, bali pia wazazi wako, pia inaonyesha elimu uliosoma ya phd bado haijakusaidia vizuri, au ninawasiwasi nayo au haijakujenga kujiajiri. Ninachokielewa PHD umefanya research nyingi na unauzoefu nazo sana, so kwanini usitumie fursa hiyo kujiajiri kwa kuwasaidia MBA student wengi wanaoshindwa research kuandaa ukajipatia kipato

Mimi nilipokuwa Undergraduate mwaka wa pili UDSM nilipojifunza tu kozi ya business proposal nikaanza kula hela za wanafunzi wa MBA, leo hii nasoma MBA nafanya marketing research, MBA research na PHD research. tembelea https://www.facebook.com/GANGORESEARCH au hapa Home - BUSINESS & RESEARCH CONSULTANCY check project zangu

Okey hebu ni PM nikupe unitafute nikupe mauzoefu ujiajiri.
 
Back
Top Bottom