Msaada wa ushauri kwenye Biashara yangu

Real polycarp

New Member
Dec 9, 2023
2
8
Habari za muda huu ndugu zangu me ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 24 naomba kushare hili wazo kwenu ili kupata Maoni tofauti tofauti yanayoweza kunisaidia.

Nina wazo la kufungua store niwe nauza mchele tu kutokea mikoani kwa bei ya rejareja kwa capital ndogo ambayo ninayo ambayo ni 1.5M.

Je, Kwa capital hii niliyonayo naweza ku running hii biashara nikianzia na kulipa rent ya frem, kununua vifaa (mzani etc) kuchukua mchele huko mikoani plus cost za usafirishaj Mpka kufika hapa Dar nilipo?
 
Huwezi apo baada ya Kodi utapata Kama kilo 500 Sasa na wwe uwe muuzaji wa jumla kweli?? utapoteza muda tu jaribu kufikri fursa zingine kijana
 
Hongera kuwa na wazo hilo la biashara Mkuu

Ila binafsi naona huo Mtaji wako wa 1.5M hautoshi

Ukichukua Mchele 500kg @1,700 =850,000
Usafiri labda Ls@60,000=60,000
Mzani 1@120,000=120,000
Fremu 100,000@miezi 6=600,000
Hapo hujalipa
~Leseni ya biashara
~Kodi

Binafsi nashauri bora hiyo hela ukanunue matunda na ufungue Banda uweze kufanya hiyo biashara ya matunda

Kama utaweza kafungue mabanda mawili Moja uza mwenyewe then lingine mwajiri Kijana akusaidie

DSM matunda ni ghali sana, ndizi moja tunanunua shilingi 300, parachichi shilingi 2,000, Chungwa shilingi 250

So ukijipanga vizuri unaweza kutengeneza Faida kubwa at low investment capital
 
upo maeneo gani?
ukiweza agiza mchele then uweke ndani tafuta mifuko pima kilo 20 each bag anza kutangaza kwenye whatsapp groups, fb huko yaani uwe na groups whatsapp kama mia hivi unakuwa unapost ila hakilisha ni ule super kwa mtaji huo na umri hu (huna majukumu makubwa) unaweza kutoboa ukiwa na nidhamu na pesa na kuipenda kazi yako


all the best dear
 
Back
Top Bottom