Nina maumivu makali sana kutokana na kupoteza muda kwenda mkoa mwingine kutoa mahari binti akajificha na kutoweka

Muyohza

Member
Dec 22, 2020
51
109
Mimi nina maumivu makali, yawezekana kutokana na machungu niliyonayo yatasababisha nisimlie kwa mpangilio usio sahihi

Ilikuwa Mwaka 2019 mwezi wa 8 nikaenda Mitaa fulan ya Dar as salaam.

Nikaonana na binti mmoja ambaye alionekana mtulivu, ikafika hatua tukawa wote kwenye mahusiano.

Baada ya miezi 6 Nikamshawish akaacha kazi kutokana na kazi alokuwa akifanya isingempendeza Mungu.

Nikampatia mtaji si vema kutaja kiasi, lakini haikuwa kidogo.

Akanipigia bajet ya kufungua duka la mchele wa jumla, magunia ya kuanzia yalikuwa 100 yaan tan 10, nikampa kwanza asilimia 80 ya mtaji husika, tukaendelea vema.

Mwaka huu mwezi wa 8 tukapanga mambo mengi mpaka siku ya kufunga ndoa

Tukamtafuta mshenga na kwenda kwao, tukaambiwa kifungua mlango ni ndama wawili na kinywaji, nadhani unaelewa kabila fulani linatozaga mambo hayo kwa gharama, ndama mmoja alithaminiwa kwa 500,000 hivyo wawili na kinywaji wakapokea 1.1M

Akaja kunitembelea mkoani kwetu hasa kipindi cha korona ambacho nimekuwa Tanzania kwa muda.

Tukapanga siku ya kuondoka kuelekea napoishi (sitaji ) atakabidhi Biashara yake kwa dada yake mmoja ambaye anafanya kazi kwenye kampuni ambayo inaelekea kufilisika, sikujali sana maana niliona bora maana nitaenda naye.

Tukapigana akapata pass ya kusafiria nikamuombea Utaratibu wa Visa kwa kutumiwa supportive document kutoka sehemu husika tukaenda wote ubalozini.

Baadaa ya kupata Visa tukapanga kwamba twende kwao kutoa mahari ambapo walisema ng'ombe 6 na kondoo 4 , cret 4 za bia , nikasema ntatoa cash almost 4 m lakini ningeanza na 75% yake,

Nika organize na wazazi na mshenga twende mkoani kwake, tumefika mkoani kwake katoweka kwao siku moja kabla ya mahari na send off ndani ya week husika, akawa anapigiwa anasema siko tiyari kwa ndoa Jambo lililoniuma sana, tumeshafika na kuingia gharama.

Nimepata hasara sana hata harusi tuliyopanga ifanyike tukalazimika kuahirisha,

wanawake wanawake wanawake,

Ilipofikia nimejuta sana kutofuata ushauri wa wazazi juu ya kuoa mbali,

Kwa sasa nikiingia kusaka tena sitafanya kosa,
Sitaoa Kabila nisilojua kiundani
Sitachelewa sana nitatafuta mwingine haraka,
Sitapenda Single mother mana alikuwa na mtoto wa Kiume mmoja,

Mtanisamehe, sitaoa mwanamke aliyelelewa na upande mmoja wa mzazi hasa mama, maana msemaji wa family alilegea sana kutatua hili.

Sitao mwanamke ambaye ana dada zake ambao wamezalishwa nyumbani tu, maana ana dada zake wawili wamezalishwa pale pale,
 
Single Mother? Alafu mahali milioni 4?? Kwelii?? Hii kama sio chai basi we jamaa ni LOFA la kutupwa, ni TAKATAKA kabisa, BURE kabisa
emoji35.png
emoji35.png
emoji35.png
emoji35.png
emoji35.png
emoji35.png
emoji35.png
emoji35.png
emoji35.png
emoji35.png
emoji35.png
 
Mleta Uzi hebu tulia kwanza, kunywa maji, sali kwa Imani yako upate amani ya moyo ulale, naona hasira zimekuamsha.

Halafu asiyejitambua mmoja asikufanye uwachukie wanawake wote wa Aina fulani.

Hakuna asiyeumizwa kwenye mahusiano, na hakuna kundi pekee ambalo lenyewe ndio limekamilika idara ya mahusiano, wote tumegawanyika wema na wabaya.

Omba Mungu Akupe mtu sahihi.

Kutafuta mwingine haraka sio suluhisho la muda mrefu, utatafuta kwa hasira, utamtumia huyo mwanamke mpya kujipoza maumivu uliyonayo kwa Sasa (hili hutaelewa kirahisi ,utajijibu hapana), utaoa haraka ili kumuonesha aliyekukimbia umepata Bora zaidi yake.

Ambacho hujui maumivu yakipungua au kuisha ndio utajua huyo uliyemuoa hakuwa sahihi na wakati mwingine Wala si chaguo lako.

Cha msingi tulia, jipe muda, hasira hamishia kwenye kazi.

Utapata mke sahihi kwa wakati sahihi. Epuka kuwezeka kiasi kikubwa kitachokuumiza kwa mwanamke ambae hujamuoa au hujazaa nae ili usijute.

Ukiamua kumsaidia Basi toa kama sadaka.

Kila la kheri
 
Nazani kosa lilianzia kwenye kazi uliyomkuta nayo ambayo uliona haimpendezi Mungu ukaamua kumuachisha...Nawaza tuu isije kuwa alikuwa anafanya ukahaba ukahisi atabadilika! btw pole ila utakuwa umepata darasa zuri jipe muda utapata atakae kufaa
 
Mkuu kwanza pole
Sema mimi Ningependa kujua kwani mama yako alikuambia nini kuhusu kuoa mbali?
Sema mkuu nyuzi kila siku haziiishu zikizungumzia kuhusu kutowekeza kwa mwanamke ambaye bado haujamuoa, sasa mbona wewe uliwekeza?

Huyo mwanamke hana wema, sema hebu tuambie kazi aliyokuwa anafanya ni kazi gani?

Isije ikawa mwenzako kashazoea kuruka ruka na wanaume wengine, alafu wewe ndio unataka umuweke ndani
 
Mkuu kwanza pole
Sema mimi Ningependa kujua kwani mama yako alikuambia nini kuhusu kuoa mbali?
Sema mkuu nyuzi kila siku haziiishu zikizungumzia kuhusu kutowekeza kwa mwanamke ambaye bado haujamuoa, sasa mbona wewe uliwekeza?

Huyo mwanamke hana wema, sema hebu tuambie kazi aliyokuwa anafanya ni kazi gani?

Isije ikawa mwenzako kashazoea kuruka ruka na wanaume wengine, alafu wewe ndio unataka umuweke ndani
Kwa kifupi Mwanamke ni Mmasai,
Alikuwa anafanya kazi Lounge moja Dar es salaam
 
Back
Top Bottom