Hivi ni kwanini mwanaume akimzalisha tu binti dharau zinaanza

Mwanongwa

Senior Member
Feb 15, 2023
169
198
Habari wana jamii,hongereni kwa kuweza kuvuka mwaka salama.

Nina rafiki yangu wa kike anafanya kazi jijini Dodoma ameolewa na jamaa mmoja wa mkoani Mara, mahusiano yao yalikuwa good sana mwanzoni ila baada ya tu ya mwanamke kuzaa watoto wawili jamaa amebadirika sana.

Anamtolea mke wake maneno makali sana huku akimwambia kuwa mpaka kufikia pale hana ujanja maana hawezi kupata mume mwingine ambaye atakubari kulea watoto wawili.

Jamaa anaondoka home kama hajaacha mtu vile hatoi pesa wala nini.

Dada huyu amefika mwisho anaona bora kurudi kwao,Mpeni ushauri wana jamii
 
Huwezi kuthaminiwa usipojithamini, je anajitunza? Anavutia? Au ndo kisa amezaa analala na vijora vinanuka mikojo, nyumba inanuka mikojo na anataka mume atulie kisa amemzalia....

Ajipende, ajitunze, anukie Yani akipita barabarani akiwaambia watu ana watoto wawili wabishe....

Hakuna asiyependa vitu vizuri jamani, wanaume nao watu, Wanahitaji mapenzi na utulivu, sasa akirudi anakuta mke vululuvululu, mikelele ya watoto halafu asubuhi akuachie hela ya Kula🤣🤣🤣 Sometimes tunajisahau sana wamama.
 
Kabla ya kuingilia mahusiano yao au kutoa hitimisho, jaribu kujua story ya upande wa pili kwa sababu katikati ya hasira kila mtu hutoa neno la kumuumiza mwingine na huwezi jua huyo mwanamke ameshawahi kumtamkia au kumtendea mabaya yapi mwenzie.

Ila kama mwanaume ndio anazingua, bhasi huyo mwanamke ndiye anajua sababu gani zimemfanya abakie alipo ila kama sababu ni hofu tu ya kupata mtu mwingine. Muambie ajifunze kuondoa utegemezi wa kihisia kwa mtu, ajifunze kupenda na kufurahia maisha pasipo kung'ang'ana
 
Kama rafiki yako ameolewa na jamaa mwenyeji wa Mara..

Nataka nikwambiye wanaume wengi wanaotoka mkoa wa Mara sio waungwana especially kwenye mapenzi..
Hao wanapaswa waoae wao kwa wao na sio makabila mengineyo.

Nina majirani zangu wa kabila fulani kutoka mkoa huo aisee jamaa wanapiga na kunyanyasa sana wanawake zao..


Kwangu mimi kila mke wangu anapoongeza mtoto ndy nazidi kumpenda na kumthamini
 
Mpe poleee single mama wetu ajae mtaanii tuendeleee jamaa alipoishiaaa ..


Kataa NDOA
JamiiForums12049724.jpg
 
Maswali ya kuuliza.

1. Alitumia muda gani kumpa jamaa jibu,kumkubalia na hadi wakapeana mchezo?

2. Walikuwa na ratiba gani kipindi wakiwa ni couple yaani before hawajapeana ujauzito?

3. Wanawake huwa wanahisi wanaume wanawabadilikia ila kiuhalisia wanaume wanareact according to namna wanawake wanawatreat. Je akijitathimini kama mwanamke, anahisi namna ana mtreate mwanaume wake ni sawa na kipindi wakiwa bado wanaanza?

4. Ratiba ya kulea watoto huwa inafinya sana ratiba za mapenzi kati ya mume na mke. Je , rafiki yako amejaribu kuona namna mambo ya malezi yamefinya nafasi yake kama mke wa mtu kuspend time na mume wake?

5. Watoto huja na gharama na mabadiliko ya bajeti, je amejitathimini kuwa kama mzazi gharama za malezi na watoto hazijawaathiri wao kama wapenzi kwenye namna wanawasiliana?

6. Je, vipi eneo la kitandani, maana kupata watoto wawili huwa inabadilisha hata maumbile na msisimko wa kitandani, je, inawezekana kuwa bado anayo thamani ile ile kitandani au kuna vitu vimepungua?

Haya ni baadhi tu ya maswali, mengine nitayauliza baadae.
 
Naku
Kama rafiki yako ameolewa na jamaa mwenyeji wa Mara..

Nataka nikwambiye wanaume wengi wanaotoka mkoa wa Mara sio waungwana especially kwenye mapenzi..
Hao wanapaswa waoae wao kwa wao na sio makabila mengineyo.

Nina majirani zangu wa kabila fulani kutoka mkoa huo aisee jamaa wanapiga na kunyanyasa sana wanawake zao..


Kwangu mimi kila mkw wangu anapoongeza mtoto ndy nazidi kumpenda na kumthamini.
Nakupinga kwa asilimia kubwa
 
Nijuavyo mimi,hayo makabila yanayosemwa kwamba hayako romantic sio kweli,tunapaswa kujua tu kwamba shule zimeshafika kila kona sasaivi,kama walikua hawajastaarabika ilikua zamani sio sasa,
Ninachokiona mimi ni kwamba wanadamu tunaishi kwakutegemeana,hapo hapo kuna wakati kila mmoja anakua na uhitaji wa namna fulani kutoka kwa mwenzi.sasa ukumbuke wakati unahitaji inaashiria umesahauliwa kupatiwa mahitaji,sisi wanaume ndio viumbe pekee ambao tunaweza kulala na maumivu pale mwanamke anapokuzingua,sasa utavumilia ila mwisho wa siku ukichoka utatoka kusaka nje.hapo ndipo unapoonekana mbaya.wanawake wanakua bize sana wakiwa na watoto yani kama vile mwanaume anavyokua bize na kazi akirudi kachoka ila bado inabidi auwashe moto.
All in all kikubwa ni kuvumiliana tu hakuna namna.
 
Naku

Nakupinga kwa asilimia kubwa
Mkuu fatilia sana hawa wanaonyanyasa wanawake kwa kupiga na kuwadharau wanatoka maeneo gani?

Kuna baadhi ya makabila mwanamke hata awe na umri mkubwa kiasi gani hawezi fanana na mtoto wa kiume.

Mimi nina ushahidi wa jirani zng wa huko musoma/Mara ebwana jamaa wananyanyasa na kudhalilisha sn wake zao.

Mbaya Zaidi jamaa wameoa wanawake ambao ni makabila ya ukanda wa kaskazini.

Daily mayowe ya vipigo bila sababu..

Story ni kama huyo dada,,zinafanana
Jamaa amezaa watoto 2 na huyo mwanamke ambaye sio wa Mara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom