Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,563
- 5,249
Mnyonge The best 007 njoo utie neno huku
Ile trillion 1.5 iliendaga wapHebu tufungue macho mkuu..jama kafa na utajiri/mali gani?


Aliye kuwa anawatetea wanyonge kafa na utajiri mkubwaaa! Very big challenge.
Hebu tufungue macho mkuu..jama kafa na utajiri/mali gani?
Hata mimi sijui, nilichotaka kujua ni utajiri wa mwenda zake.Ile trillion 1.5 iliendaga wap
Ameondoka tajiri huyo wewe..kalaghabahoHata mimi sijui, nilichotaka kujua ni utajiri wa mwenda zake.
Nipe hata code mwamba!Jiongeze
Nipe hata code mwamba!
Daah umenikumbusha ule msemo aisee "Kataa kuwa kaa"Asilimia kubwa watanzania wana umaskini wa kichwa na wanasiasa ndio utukandamiza kwenye mambo mengi ambayo ni lazima wanadamu tuwe nayo
Mfano :gari si hanasa kwa maisha ya sasa au huduma lazima mwananchi kuwa nazo kama bima ya afya,mikopo,nyumba mfano NHC,fursa kwa vijana na n.k
Kwa vile wanyonge ndio group la wajinga wanao furahi wajinga wenzao.
Kuna msemo walipenda kutumia clouds fm ule msemo wa usikubali kuwa mdudu kaa,unajua kaa akiwa mmoja kwenye sufuria anaweza kujikomboa ila wakiwa wengi kujikomboa ni shida ndani ya sufiria kila kaa kuzuia mwenzake asitoke.
Wanyonge ni sawa na kaa
Wanyonge lazima wawepo wanasiasa wawatumieMnawasaidiaje hao wanyonge?
Msiwalaumu tu.
Watu wenye kipato cha chini ndo tunaweza kuwaita wanyonge, sasa huwezi kudai unawasaidia wanyonge kwa kuwabana wale wenye kipato cha kati, mfano watumishi wa umma, wafanyabiashara na wajasiriamali. Kwa sababu watu wa daraja la kati wakifanikiwa na kufanya matumizi ndo hapo kula ya wanyonge itapatikana, vinginevyo utajikuta unatengeza kundi moja kubwa la watu wanyonge tupu...
am afraid he is very very right. why?Uko sahihi..."kuna mzee mmoja aliwahi niambia mwaka jana kwa sasa yupo UK kwa mwanae anasema Maskini wana roho mbaya sana"....ilikua natoka Songea kurejea Dar
Tokea Awamu ya 3 na ya 4 haya makundi yalikuwepo na yalikuwa yakijitanua Magufuli kayakuta acheni kumkweza Dikteta uchwaraMachinga, Mama ntilie na Bodaboda jinsi walivyokuwa wanajitanua
Watu wenye kipato cha chini ndo tunaweza kuwaita wanyonge, sasa huwezi kudai unawasaidia wanyonge kwa kuwabana wale wenye kipato cha kati, mfano watumishi wa umma, wafanyabiashara na wajasiriamali. Kwa sababu watu wa daraja la kati wakifanikiwa na kufanya matumizi ndo hapo kula ya wanyonge itapatikana, vinginevyo utajikuta unatengeza kundi moja kubwa la watu wanyonge tupu...
Haya ni maneno yaliyofujwa kipindi cha utawala wa MagufuliMimi kiukweli huwa sikubaliani kabisa na hii falsafa ya wanaoitwa Wanyonge.
Ni kundi linalotengenezwa na watawala kwa maslahi ya watawala wenyewe.
Mfano, nchi za Africa,Tanzania ikiwemo,tulijengewa na wakoloni fikra na tukaikubali kwamba ni maskini ambao tunatakiwa kusaidiwa.
Hii iliwarahisishia sana kututawala kwa kutupa vimsaada ambavyo,kwa mawazo yetu finyu,tuliona ni msaada mkubwa sana kwetu na tukawa tunawakweza.Mpaka leo fikra hizo mbaya hazijatoweka miongoni mwetu.
Vivyo hivyo, Wanaoitwa Wanyonge wametengenezwa ili wawe mtaji wa wanasiasa kupata mamlaka.
Wanaoitwa wanyonge wakipewa nafuu fulani,hata kama ni haki yao ya msingi,hufurahi na kuwaona watoaji kama Mungu wao.
Kwa hiyo,namaliza kwa kuwataka wote wanaojiona wako kwenye kundi la wanoitwa wanyonge wajitambue na kujiona kuwa sio wanyonge na kama wanapatiwa nafuu yoyote na watawala wafahamu kuwa hiyo ni haki yao sio hisani.
Au ninasena uongo ndugu zangu?