Watu waliopata misaada ya aina hiyo ni wengi sio lazima kwenye viwanja bali kwa namna zingine. Hao ndio wanyonge wa Magufuli.
Swala la kupenda kuona wengine wanakwama halina uhusiano wowote na uongozi ni utamaduni na kiwango cha uelewa wa mtu.
Sifa kubwa ya mtu maskini ni kuamini kupata ni bahati na si jitihada. Na hiyo notion inakuwa kubwa zaidi kwenye hizi nchi zetu ambapo unakuta watu 200 wanagombea nafasi moja ya ubunge au udiwani. Akikosa huko basi anakata tamaa wakati kuna option zingine za kutengeneza maisha. Na anaepata nae saa zingine ata kama wenye wivu ni baadhi yeye anaamini wote waliokosa wanamuonea wivu especially kama uelewa wake ni mdogo.
Ndio matokeo yake watanzania ni watu wenye wivu sana na kujihami sana. Sio wanyonge tu ata makazini promotional ya mmoja inawekera wengine, that has to do with our embedded culture.
Why embedded culture? asilimia kubwa ya watanzania wanabaki na akili hizo (sio wote) ata ukiwatoa nje ya nchi.
Unaweza kumpeleka mtanzania ulaya, akapata makaratasi ya kuishi huko, shule bure mpaka elimu ya juu, kuna grants luluki za biashara ndogo sehemu zingine zisizo na malipo.
Wengi kwa uelewa wao mdogo awaangalii fursa zilizo wazunguka matokeo yake akiona mtu anaemjua anatusua anaanza wivu wakati na yeye ana fursa hizo hizo kwa sababu keshajijengea kupata ni bahati.
Kwa hivyo swala la wivu wa kushushana ni culture ya watu maskini kwa asilimia kubwa popote duniani; ila kwa watanzania is at different level, duh hawa jamaa noma.